HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
- Wabunge
- Madiwani
- Wenyeviti serikali za mitaa
Wabunge ambao hawajasoma hawana tija wala msaada kwa taifa na sababu ni kuwa hawaelewi miswada inayopelekwa bungeni, hivyo wao hukubaliana na kila kitu wanachoambiwa.
Madiwani kwenye Halmshauri wapo ambao hawawezi andika karatasi nzima lakini hao ndo wasimamizi wa mapato ya halmshauri zetu, je tutegemee nini?
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa hawa ndio wasimamizi wakuu wa Sera za Kielimi, Ardhi etc, makazi horera yamesababishwa na hawa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wao na Ofisi zao kwa Makusudi wamekuwa wakikubali mtu ajenge bila kupeleka Ramani na kuona kama yaenda au haiendani.
Hata kwenye Ripoti ya CAG imeonesha kuna wafanyakazi 740 ambao wapo kwenye vyeo wasivyo sitahili kuwepo.
Ukiangalia bungeni, wabunge wengi mule kazi yao ni kusifu na kuabudu badala ya kuongea mambo ya msingi kwa jamii.
NB: Tusipojirekebisha hakika Nchi yetu itapotea.