Wana JF, Tukiangalia mambo yanavyokwenda unaweza kuona kuwa kama katiba haitaweka utaratibu maalum wa kuteuliwa watoto wa vigogo kuwa Mawaziri pamoja na nyadhifa nyingine muhimu kitaifa tunaweza kujikuta katika muundo wa familia za Kifalme bila kutarajia.
Kwa mtazamo wangu nadhani ni vyema Katiba ikaelekeza wazi kuwa mtoto wa Raisi mstaafu hawezi kuchaguliwa kuwa waziri kutoka chama hicho hicho kimoja katika kipindi chini ya miaka ishirini tangu baba yake atoke madarakani. Kuzingatiwa kwa taratibu kama hiyo kutaondoa sana uwezekano wa Maraisi kupendelea familia zao wazi wazi.
Tutafakari zaidi