Kuchaguliwa kwa watoto wa Maraisi wastaafu kuwa Mawaziri ni jambo linalohitaji utaratibu kikatiba

Kuchaguliwa kwa watoto wa Maraisi wastaafu kuwa Mawaziri ni jambo linalohitaji utaratibu kikatiba

Kwani misingi ya katiba kumruhusu Rais kuteua watu kwa nafasi kama anavyoona yeye ni ipi??..Kwa kukusaidia ni kwamba Rais ili atawale lazima awe na timu ya watu anaowaamini na kwa mfumo wa sasa wa katiba hii ni kutoka ndani ya BUNGE(naongelea mawaziri)...nafasi alizopewa ni kwa maslahi ya taifa kabisa...umewahi kujiuliza vipi kama wabunge woote wangekuwa wa CHADEMA na RAIS ni wa CCM?? Kungekua na serikali hapo???
>>>Pili Rais ni taasisi na sio mtu mmoja...na kwa taarifa yako JK pale ni kama spika tu ya kuongea lakini WENYE NCHI WAPO NA HUWEZI KUWAJUA...kwa hiyo kuhoji kwa nini wanateuliwa maswahiba au ndugu na watoto kwa misingi ya kikatiba ni sawa na kuhoji kwa nini binadamu anatakiwa awe na miguu miwili lakini kuna watu wanazaliwa na mguu mmoja...

Basi hiyo taasisi mwelekeo wake siyo makini hata kidogo katika uongozi na mustakabaliwa taifa kwa ujumla. Na inaonyesha wazi kuwa wahusika kwenye hiyo taasisi inayoruhusu mambo haya inakitu nayo inafaidi au inachuma. Imekwisha onyesha wazi mwelekeo wa kufanya kazi siyo kwa maslahi ya Taifa bali ya hilo kundi lao. Kukubali hayo ni sawa na kutetea na/au kutukuza udhaifu.
 
... Elimu ya watoto wa viongozi wetu ni elimu ya kifisadi na haikuzigatia haki ya Watanzania kwa ujumla.
Ukifatilia karibia watoto wote wa vigogo wamesomeshwa nje ya nchi' kana kwamba hapa Tanzania hakuna sehemu kunapatikana hizo nyanja walizosomea.

Huwezi kupinga ufisadi mmoja (wa viongozi kuchaguana familia zao) kwa kutumia ufisadi mwingine (wa kunyima Watanzania haki zao za kikatiba).

Ufisadi ni nini? ku suspend katiba si ufisadi?
 
Hivi ni vitu vidogo? Nadhani vidogo unavijua aisee, usijifanye kuwa huvijui. Kumchagua mke wako hivyo ni vidogo kwa taifa. Tuko karibu sana kwa taarifa yako kuelekea kwenye mfumo wa kifalme. CCM ikitawala tena miaka hamsini nakuhakikishia watakaokuwepo watakiri jambo hili. Jambo lolote linalohusu taifa haliwezi kuchukuliwa kuwa dogo kwa kuwa tu unataka mambo yawe kama yanavyokupendeza or in your favor.
Tunataka michango mizuri hapa siyo dharau Mkuu.
Naona umeanza kutoka povu badala ya kujadili hoja....
Kwa misingi ipi umpokonye Rais uwezo wa kuteua timu ya watu inayomfaa ili hali ktiba inamruhusu?? Kwa misingi ipi katiba inamruhusu Rais kuwa na mamlaka ya kuteua watu anaoona wanamfaa??? Si kwa maslahi hayo hayo ya taifa???...
Nikuulize tu swali rahisi..ikitokea Rais wa CCM yuko madarakani na kuna nafasi ya uwaziri mkuu iko wazi na majina mawili yaliyopendekezwa ni RIDHIWANI(mtoto wa RAIS) na la DR SLAA(MCHAPAKAZI HASWAA) unadhani kwa maslahi ya taifa ni nani angefaa kuwa waziri mkuu??
 
Mkuu hapa ndipo haswa linapotokea wazo. Ufahamu kuwa watoto wao lazima watapata elimu nzuri ndani na nje ya nchi na tunajionea wenyewe kuwa hawana nia mathubuti za kuboresha elimu kwa wote. Kwahiyo kitakachotokea ni kwamba basi hakuna atakayeweza kuwa kiongozi kama hajatokea moja ya hizo familia? Maana ndizo zenye elimu nzuri kutoka shule na vyuo vya hali ya juu. Angalia hata mikopo kwa vijana inavyozidi kubanwa.
Tena nielewe vizuri sijamaanisha tuwakatae bali isiwe ni kitu cha moja kwa moja kama ilivyo sasa, mithili ya utawala wa kifalme. Utaratibu uwe kwamba aweze kuteuliwa na Raisi anayekuja baadaye sana ambaye si rahisi kwa baba yae kuwa alichangia moja kwa moja kwenye uchaguzi wa huyo Raisi aliyeko madarakani.

Sasa hivi hili linaelekea kuwa tatizo la class.

Kwa sababu viongozi hawa wameozana familia mpaka upinzani. Crossbreefing "chief" families.

I can see the Mwapachu, Bomanis, Mbowes, Nyereres, Magenis, Makanis etc sitting at one family reunion.

Sasa hapo hata ukisema vote CHADEMA tuondoe mtindo huu itakuwa trial and error tu.

CHADEMA kwenyewe kuna manung'uniko ya watu kupeana vyeo kifamilia.

This is a morality and cultural thing. You can't legislate these matters.

Your best bet is to educate the masses.
 
Basi hiyo taasisi mwelekeo wake siyo makini hata kidogo katika uongozi na mustakabaliwa taifa kwa ujumla. Na inaonyesha wazi kuwa wahusika kwenye hiyo taasisi inayoruhusu mambo haya inakitu nayo inafaidi au inachuma. Imekwisha onyesha wazi mwelekeo wa kufanya kazi siyo kwa maslahi ya Taifa bali ya hilo kundi lao. Kukubali hayo ni sawa na kutetea na/au kutukuza udhaifu.
Kama wao hawana majukumu ya kuchagua ni sera zipi wafanye nazo kazi kwa nini kuwalaumu kuwa haina faida?? Wananchi ndio wa kuwalaumu maana wao wana jukumu la kupima ni chama gani na kwa ilani gani kinadaa kukabidhiwa uongozi..
 
Naona umeanza kutoka povu badala ya kujadili hoja....
Kwa misingi ipi umpokonye Rais uwezo wa kuteua timu ya watu inayomfaa ili hali ktiba inamruhusu?? Kwa misingi ipi katiba inamruhusu Rais kuwa na mamlaka ya kuteua watu anaoona wanamfaa??? Si kwa maslahi hayo hayo ya taifa???...
Nikuulize tu swali rahisi..ikitokea Rais wa CCM yuko madarakani na kuna nafasi ya uwaziri mkuu iko wazi na majina mawili yaliyopendekezwa ni RIDHIWANI(mtoto wa RAIS) na la DR SLAA(MCHAPAKAZI HASWAA) unadhani kwa maslahi ya taifa ni nani angefaa kuwa waziri mkuu??

Hapa nazungumzia muundo wa katiba mpya siyo hii uipendayo ya sasa.
 
Kama wao hawana majukumu ya kuchagua ni sera zipi wafanye nazo kazi kwa nini kuwalaumu kuwa haina faida?? Wananchi ndio wa kuwalaumu maana wao wana jukumu la kupima ni chama gani na kwa ilani gani kinadaa kukabidhiwa uongozi..

Hapa nazungumzia katiba mpya na ikimaanisha kusiwewpo na mwanya wa namna hili kwa chama chochote kitakachokuwa madarakani.
 
Tanzania imekuwa too much, watoto wa akina mwinyi, kawawa, makamba, kahama, karume, jumbe, thabit kombo, malima, kikwete, getrude mongela, nnauye, mhita, sokoine bado sijasikia.

Sokoine mbona alikuwapo ubalozini Washington DC.

My first impression was he was a smart fellow with a common touch, no airs. But thats beside the point.

Ile list ya BOT ndo ilikuwa balaa. Mie nisingekubali kufanya kazi pale kama ningekuwa katika ile set.
 
Sasa hivi hili linaelekea kuwa tatizo la class.

Kwa sababu viongozi hawa wameozana familia mpaka upinzani. Crossbreefing "chief" families.

I can see the Mwapachu, Bomanis, Mbowes, Nyereres, Magenis, Makanis etc sitting at one family reunion.

Sasa hapo hata ukisema vote CHADEMA tuondoe mtindo huu itakuwa trial and error tu.

CHADEMA kwenyewe kuna manung'uniko ya watu kupeana vyeo kifamilia.

This is a morality and cultural thing. You can't legislate these matters.

Your best bet is to educate the masses.

In order not to apply the trial and error method we need to see how this issue can be addressed in our new constitution.
Tunaweza kuja fika pahala tukajaona katika hili CCM walikuwa na nafuu. Itatuchukua muda gani kutoka hapo?
 
Hapa nazungumzia katiba mpya na ikimaanisha kusiwewpo na mwanya wa namna hili kwa chama chochote kitakachokuwa madarakani.
Inawezekana mianya kama hii katiba mpya ikaiziba ... lakini Kwa mwenendo wa sasa wa ukusanyaji maoni ulivyokua watu wanakesha kulumbana mambo yasiyo ya msingi kama UDINI na mambo ya uchinjaji...unategemea mianya kama hii isiwepo?? Nimewahi kutoa maoni yangu kwenye jukwaa moja la kisheria pale CHUO KIKUU MLIMANI ya kwamba ni kwa nini mahakama ikawa chini ya wizara ya SHERIA na katiba ambayo ni sehemu ya EXECUTIVE PARTY of the government a,bayo iko chini ya WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA na chini ya wziri mkuu na chini ya makamu wa raisi na chini ya rais??Ili hali MAHAKAMA inatakiwa iwe na nguvu sana na BUNGE na EXECUTIVE...na nkawauliza kwa nini BUNGE haliko chini ya wizara yoyote?? hawakunipa majibu...cha ajabu hata kwenye maoni yao ya katiba hili sikulisikia likitamkwa zaidia ya kulilia tu RAIS apunguziwe madaraka ya kuteua majaji.. CHADEMA walipoomba BUNGE maalumu la katiba walikua na maana pana sana hasa ya kuziba mianya kama hii(maana bunge la katiba huongozwa na wanasheria waliobobea katika masuala ya katiba)...lakini kwa uelewa finyu wa watanzania wakawaona sio..sasa usitegemee mianya kama hii itazibwa
 
Katiba ya nchi haiwezi kuongelea vitu vidogo namna hii...haya ni mambo ya kwenye sera na ilani...siku katiba ya nchi ikianza kuongelea mambo ya hovyo kama haya ujue hanuka tena taifa hapo...hebu tafuta nakala ya katiba uone mambo yanayozungumziwa humo ndani...kama huna ni PM nikutumie soft kopy....

Unafuatilia maoni ya wananchi wa kawaida kuhusu katiba mpya?

Kuna mambo mengine wanasema yanachekesha ingawa issue serious.

Watu hawaijui katiba ya sasa, hawajui tofauti ya katiba na sheria, wanataka katiba I define mpaka nguo za ndani.

Halafu unakuta jitu kama Mzee Lubuva. AG wa siku nyingi. Waziri wa sheria anayejua umuhimu wa separation of church and state katika nchi iliyo religiously volatile kama yetu, anataka habari ya mungu kwenye katiba.

Ukiona Jaji Lubuva anasrma hivyo inabifi usamehe kwa mpigo tu makosa ya laymen.

Ndiyo haya ya kutaka kuzuia watu haki zao za kikatiba.

Kitu kuwa kwenye katiba ni lazima kiwe na air of being necessarily definitive. Ama sivyo watupie wananchi waamue.
 
Tanzania imekuwa too much, watoto wa akina mwinyi, kawawa, makamba, kahama, karume, jumbe, thabit kombo, malima, kikwete, getrude mongela, nnauye, mhita, sokoine bado sijasikia.

... Kama mambo yataendelea hivi! Itafika wakati sera ya Mtwara ichukue nafasi yake.
Viongozi wetu wameanza kuleta tawala za kifalme' hali ikishakuwa mbaya wanaanza kulalamikia wananchi.
 
In order not to apply the trial and error method we need to see how this issue can be addressed in our new constitution.
Tunaweza kuja fika pahala tukajaona katika hili CCM walikuwa na nafuu. Itatuchukua muda gani kutoka hapo?

The constitution is a high level, big picture, primary law of the land.

Constitution ukianza kuiingiza kwenye detail za nani anastahili kuwa mbunge na nani hafai usha I butcher.

Ushatengeneza matabaka mawili ya Watanzania. Huwezi tena kusema Watanzania wote ni sawa wakati wengine hawaruhusiwi kuongoza kikatiba.

Ushaiminya demokrasia ya wananchi kumchagua wanayemtaka. Umepunguza wigo wa direct democracy.

Elimisha wananchi wajue kuchagua viongozi on the merit rather than pedigree. Fundisha watu egalitarianism. Itakuwa huna haja ya ku fiddle na katiba.
 
Huwezi kupinga ufisadi mmoja (wa viongozi kuchaguana familia zao) kwa kutumia ufisadi mwingine (wa kunyima Watanzania haki zao za kikatiba).

Ufisadi ni nini? ku suspend katiba si ufisadi?

... Ni Aina yoyote ya matumizi mbaya yasiyokubalika mbele ya jamii
 
Inawezekana mianya kama hii katiba mpya ikaiziba ... lakini Kwa mwenendo wa sasa wa ukusanyaji maoni ulivyokua watu wanakesha kulumbana mambo yasiyo ya msingi kama UDINI na mambo ya uchinjaji...unategemea mianya kama hii isiwepo?? Nimewahi kutoa maoni yangu kwenye jukwaa moja la kisheria pale CHUO KIKUU MLIMANI ya kwamba ni kwa nini mahakama ikawa chini ya wizara ya SHERIA na katiba ambayo ni sehemu ya EXECUTIVE PARTY of the government a,bayo iko chini ya WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA na chini ya wziri mkuu na chini ya makamu wa raisi na chini ya rais??Ili hali MAHAKAMA inatakiwa iwe na nguvu sana na BUNGE na EXECUTIVE...na nkawauliza kwa nini BUNGE haliko chini ya wizara yoyote?? hawakunipa majibu...cha ajabu hata kwenye maoni yao ya katiba hili sikulisikia likitamkwa zaidia ya kulilia tu RAIS apunguziwe madaraka ya kuteua majaji.. CHADEMA walipoomba BUNGE maalumu la katiba walikua na maana pana sana hasa ya kuziba mianya kama hii(maana bunge la katiba huongozwa na wanasheria waliobobea katika masuala ya katiba)...lakini kwa uelewa finyu wa watanzania wakawaona sio..sasa usitegemee mianya kama hii itazibwa

Hili nalo (kubagua Watanzania katika mafungu) kuwekwa kwenye katiba ni sawa na gumzo la uchinjaji.

Too fine a detail. Too indefinite.

Suppose tunakubali.

Tuanzie wapi tuishie wapi? Watoto wa marais na mawaziri? Manaibu waziri je? Vipi makatibu wakuu na wakurugenzi? Mabalozi? Au tufanye wote waliowahi kukaa Oysterbay na Masaki wapigwe ban? Upanga napo vipi mbona pamekaa kidosi?

Pretty sure soon tutajikuta tunapoteza focus kama mauaji yaliyofuata Ufaransa baada ya mapinduzi ya kumuondoa Louis XVI 1789 - 1799.

Tuanzie wapi tuishie wapi?

Watoto wa "nje" je kina Nape na William?

Watoto wa kufikia je kina Peter?

Watoto wa ku adopt je kina Kipi?

Watoto wa wake wa pili kina Salama?

Mashemeji je kina Ernie? Wanaweza kushikishwa mikoba ati.

Na vipi kama mtoto anajishtukia alibambikiwa baba ambaye si wake?

Wajukuu kina Judy wanahusika? Vipi wakwe waliooa na kuolewa katika familia hizi kama kina Sabina?

Nyumba ndogo kina mama Mary nazo? Zihesabiwe? Tukiziacha tunaweza kuacha loophole.

Where exactly do you draw the line? And why there, not a step further?

Na tutahakikishaje kwamba mtu baki hawezi kufanywa mtoto wa mkulu baada ya kuwa waziri?

Tunarudi kwenye voter education, merit based appointments and culture of responsibility.
 
... Ni Aina yoyote ya matumizi mbaya yasiyokubalika mbele ya jamii

Basi hata kutaka kunyima Watanzania uwezo wa kikatiba kuongoza kwa sababu ya ajali ya nasaba ni ufisadi.

Kumkubali mtu ashike cheo kwa sababu ya nasaba na kumkataa mtu asishike cheo kwa sababu ya nasaba ni pande mbili za sarafu ile ile.

Kimsingi unafanya maamuzi kwa kuzingatia nasaba. Kitu ambacho ni kibaya. Whether unampendelea mtu apate ofisi au unamnyima nafasi mtu asipate ofisi ni detail tu. The essence is the same. Kihesabu wanasema the magnitude of the vector is the same. The difference is not fundamental. Just direction.

Sasa huwezi kukataa upendeleo kwa mujibu wa nasaba kwa kuleta exclusion kwa mujibu wa nasaba kikatiba.

Utakuwa kama unasema "hawa wazungu wa Afrika Kusini wametutawala sana, hatutaki ubaguzi wa rangi. Sasa ili kuondoa ubaguzi wa rangi, tuwapige marufuku wazungu kugombea nafasi za uongozi".

Utachekesha.
 
Umesema ukweli.
Theoretically republic but practicall monarchy!

Sent from my BlackBerry using JamiiForums
 
Back
Top Bottom