Kuchangia au kutokuchangia? Hilo ndilo swali..

Kuchangia au kutokuchangia? Hilo ndilo swali..

Ninasikitika kuwa ukombozi wetu unaonekana bado uko mbali sana. Na hii inatokana na wengi wetu kukumbatia tabaka hili la kifisadi aidha kwa maslahi binafsi au kutojua kuwa tunatumiwa kutekeleza matakwa yao. Siku zote naumia ninapoona jamii iliyobahatika kufurukuta na kuruka vizingiti vyote na kuelimika bado haioni kama tuna tatizo ambalo tunatakiwa kulishughulikia kwanza ndipo mengine yote yafuate. Tatizo hilo ni CCM. Inafaa CCM iondoke kwanza ndipo tuanze kuunda Taifa Huru la Tanzania. Uwepo wa CCM unaturudisha katika ukoloni. Jamii ya wasomi imebaki kuwa ya kibinafsi ya kila mtu kujali maisha yake. Kama tungekuwa na mawazo mema ya nchi hii tungefanya kila njia tuwang'oe hawa walioteka uhuru wetu.

Na kwa kutaka ufahari au sifa za kijinga kuna watu watatuma SMS nyingi tu, lakini hawezi kutoa msaada hata wa dawati moja kwa watoto wanaosoma wakiwa wamekaa kwenye vumbi mavumbini sio sakafuni.
Wangekuwa na aibu hata wasingethubutu kuanzisha hiyo kampeni. Ni kama wanatutukana vile..
 
Text messages zinatumwa (sijui kama ni random au wanatarget watu fulani, mimi nimepata moja) kuombwa kuchangie CCM. Sijui hii ina effect gani kwa kampeni na ushindi wa kishindo CCM.

Hapa ndipo ninapoona umashuhuri wa kudesa. Yaana wanaCCM wamedesa strategy/ies za kampeni ya Obama, na wanataka kuitumia one to one. Wamesahau kuwa uelewa na jinsi siasa kwa Wamarekani na WtTanzania ni tofauti. Tuwe wabunifu, kiasi kwamba ikifikia kudesa iwe kwa akili na maarifa.
 
Hivi watu na akili zenu mnafikiri jambo hili ni halisia poleni nawasikitikia sana hizo bil. 40 zipo tayari na ziada juu, changa la macho hilo unahangaika na ki-ndoo chako cha maji kupeleka mto Rufiji, jamani hivi elimu mliyosoma madarasani ikowapi? hiyo sh 500 mnunulie mtoto wako daftari atakusaidia baadae.
 
........ jamani hivi elimu mliyosoma madarasani ikowapi? hiyo sh 500 mnunulie mtoto wako daftari atakusaidia baadae.

Sidhani wengi wa waliosoma madarasani watachangia; hawa wengi wao ndio ambao hawajajiandikisha kupiga kura na kwa wale waliojiandikisha, huwa hawaendi kupiga kura.

Wengi wa watakao/wanaochangia ni wale waliosoma chini ya mti; huu ushauri wako hawatausoma kwani wengi wao hawatumii intanet, kama wanajua kutumia computer.

Nini kifanyike, civic education. Nani afanye, mimi na wewe. Lini, wakati ni huu. Wapi, huko vijijini.
 
Sidhani wengi wa waliosoma madarasani watachangia; hawa wengi wao ndio ambao hawajajiandikisha kupiga kura na kwa wale waliojiandikisha, huwa hawaendi kupiga kura.

Wengi wa watakao/wanaochangia ni wale waliosoma chini ya mti; huu ushauri wako hawatausoma kwani wengi wao hawatumii intanet, kama wanajua kutumia computer.

Nini kifanyike, civic education. Nani afanye, mimi na wewe. Lini, wakati ni huu. Wapi, huko vijijini.
Ujumbe wangu unakuhusu na wewe unayetumia internet, hata mimi nimesoma chini ya mti si lazima wa kijijini hata hivyo sizungumzii kura nazungumzia sms kwa vile asilimia kubwa ya simu ziko mjini vijijini hakuna network.
 
watakaochangia ndio wasomi zaidi nchini, maprofesa, wafanyakazi na wanufaika wengine wa mfumo wa utawala wa kifisadi.
 
Bado sijaona umuhimu wangu kuchangia hata senti moja ...Big No
 
Kama wangefanya hivi ili kuchangia huduma za maendeleo tungewaona wa maana! Haiingii akilini kuwa eti CCM ndio sasa wanatafuta pesa za kampeni, zile hardtop wanunua kwa pesa gani? hayo magari mengine 26 waliokwisha agiza wanmetumia pesa gani? hili ni changa la macho! wameisha kwapua pesa wanatafuta cover tu, ili wakiulizwa waseme eti ni michango ya wanachama! mtakao changia mjue michango yenu itakuwa posho za mamia ya wajumbe wa kampeni! Ama kweli wajinga ndi waliwao! alisema JK ( yule original-Julius Kambarage) kuwa...." Mtu mwerevu akikushauri kitu cha kijinga nawe ukakubaliana nae, basi atakudharau sana..." CCM wameshauri mashabiki wao na wanachama kitu cha kijinga kuchangia pesa za kampeni ambazo tiyari wanazo, sasa mkichangia ......
 
hapa niwe muwazi hata kwa bunduki sichangi
Hii ni janja tu ili watuibie waseme zimechangwa na wananchi
EPA inafichwamo humo
 
Sipendi kukata tamaa katika kuona mabadiliko ya ustawi wa taifa hili. Ila kwa hili la CCM tena chini ya uenyekiti wa Raisi wa nchi kuchangisha kiasi cha Tsh 40bn kwa ajili ya kampeni tuu za uchaguzi ni lakukatisha tamaa na kuonyeshaa ni jinsi gani taasisi hii (CCM) ilivyolewaa madaraka ya umma wa tanzania.

Naomba wana Jf tusichokee katika kuelimishanaa ubovuu wa serikali ya CCM na kuhamasishaa mabadiliko ya kweli mpaka kieleweke. Itatuchukua muda, ila tutafikia mabadiliko hayoooo.
 
hili tangazo limetoka wapi?

nimemaindi sana, katu sichangii
 
kauli mbiu ya CCM mwaka huu ni ipi. hii ya maisha bora kwa kila mdanganyika naona imekamimilika. Fair competitition Commission (FCC)inabdi waingilie kati kiasi ambacho CCM wanatakiwa wachangiwe kwa ujumbe ni Tsh 20 au 50 na vyama vingine iwe 500 na zaidi.
 
Imefika wakati badala ya CCM kuchangia maendeleo sasa wao ndio wanataka kuchangiwa ili waendelee LOL makubwa, na wananchi hatujiulizi tunachanga hizo mia tano tano ili watununulie kofia ya mia mbili.
 
Naombeni mniekeze jinsi ya kublock sms za CCM kwenye sim yangu nikiona tu CCM kwenye inbox yangu siku imearibika.
 
I HATE CCM!
...and politics...

I advise you to hate CCM but not Politics; You can not avoid politics as long as you live. If you hate politics how can we avoid being ruled by CCM?
 
Bora wachangishane wenyewe wasiguse hela zetu za kodi au BoT.

Mi naona sawa tu maana hiki ni chama na wenye mapenzi nacho wachangie kama tunavyochangia harusi na misiba ya ndugu zetu. Cha msingi wasilete vifyatavyo;

1. Wasianzishe EPA mpya kwa ajili ya uchaguzi.
2. Wasilazimishe watu kwenye mashirika ya umma na vijijini kuchangia kwa lazima
3. Wasichote hela serikalini au hazina
4. Wasitumie magari au vyombo vingine vya Serikali kufanyia kampeni au kutumia muda wao kazini kufanya hivo badala ya ujenzi wa taifa
5. Waweke wazi at least kwa wanachama wao kiasi cha pesa walichopata na matumizi yake

Je vyama vingine navyo viseme wapi vinategemea kupata hela zao za kampeni ni vema vyote viwe wazi. Hii ni hatua nzuri kwa CCM tofauti na uchaguzi uliopita ambapo hawakusema walitoa wapi hela na baadae nyingine kupotea BoT (EPA???)

Mzee, hujasikia kuwa EPA namba 2 imeshatokea kupitia zile pesa za STIMULUS PACKAGE ambazo JK alizianzisha mwaka jana na kuzitetea Bungeni? SOma Raia Mwema la JAna utaona jinsi yale Makampuni ya Makada yalivyozidishiwa mapesa, unadhani lile zidisho litapelekwa wapi? Mwenye macho haambiwi tazama. EPA namba 2 ilishachongwa tangu mwaka jana pale Bungeni na ilichongwa kwa makusudi kabisa chini ya ushawishi wa Mkulu mwenyewe. Hadi sasa BoT na Serikali wanajing'ata, wameshindwa kutoa majibu.
 
Angalau kwenye sms hamuwaoni; mpango wa pili utakuwa kwenye fundraising ambapo watafanya kwenye mahoteli makubwa na watu ambao mnafikiria wameerevuka watakuwa wa kwanza kushinda kuichangia CCM.. kimsingi michango yenu ni ni ya kuiwezesha CCM iendelee kutawala vile ilivyo; haisaidii kuleta mabadiliiko ndani ya CCM bali itakuwa ni ya kuendeleza tu uwezo wake wa kutawala kwa namna ile ile, sera zile zile na kupitia watu wale wale.
 
View attachment 9465
Siyo swali gumu na wala siyo swali la mtego hata kidogo Jibu lake ni rahisi kweli kwani halihitaji uwe msomi wa elimu ya anga za mbali au uliyebobea katika sayansi ya Fizikia ya Nyota kuweza kutoa jibu lake. Ni swali ambalo kila mwana CCM anatakiwa awe na jibu lake na kila Mtanzania kuamua vile vile kulijibu.

Mwishoni mwa juma Rais Kikwete alizindua utaratibu wa kuchangia Chama cha Mapinduzi ili kiweze kushiriki vizuri uchaguzi mkuu na kushinda ili iweze kuongoza taifa letu kwa miaka mingine mitano. Katika uzinduzi huo lengo lao ni kuweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 40 ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali ambayo yatafanikisha lengo hilo la kufanya vizuri kwenye Uchaguzi. Fedha hizi zikishakusanywa zitatumika:

- Kununua magari 60 kwa ajili ya kampeni
- Kununua pikipiki 170
- Baskeli 23,000
- Kukodi helikopta na ndege
- Matumizi mbalimbali ya makabrasha ya kampeni na uchaguzi

Ili kuweza kuchangia kwa njia ya simu mwana CCM au Mtanzania anayekiunga mkono Chama cha Mapinduzi anatakiwa atume neno "CCM" kwenda Namba 15377 ambapo atakuwa amechangia Shs 300, akituma neno "CCM" kwenda 15388 atakuwa amechangia Shs 500 na akituma neno "CCM" kwenda 15399 atakuwa amechangia Shs. 1000. Ni wazi kuwa CCM itatumia mbinu nyingine mbalimbali kuweza kufikia lengo hilo. Sasa tunajua ni kiasi gani kinahitajika, kitatumika vipi, na namna gani kuweza kuchangia. Baada ya kuyajua hayo hatuna budi kujiuliza kama tuchangie au tusichangie.

Kabla ya kuchangia jiulize!
Kwa vile najua watu wengi ambao ni mashabiki wa CCM watakuwa tayari kuchangia kwa sababu "Rais kasema" na kwa sababu wanataka chama chao kiendelee kutawala na wapo wengine ambao hawataki kusaidia upinzani ukomae na hivyo wako tayari kuunga mkono CCM basi nimeona ni vyema kujitolea kuwasaidia watu hawa ambao wana fedha na vitu mbalimbali ambavyo wako tayari kuviweka kwenye miguu ya CCM kujiuliza maswali kadhaa ambayo wakijibu ndiyo kwa yote mawili inawapasa watoe michango yao.

Hii inatafsiriwa vipi katika sheria mpya ya uchaguzi?
 
Back
Top Bottom