Kuchangia choo kunasababisha u.t.i kwa wanawake

Kuchangia choo kunasababisha u.t.i kwa wanawake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
images


Si kila mwanamke yuko huru kusema kuwa aliwahi kupata tatizo sehemu za siri. Karibu nusu ya wanawake wote walishapatwa UTI na wengi huwarudiarudia kiasi kwamba inakuwa kero. Nikianza na UTI, napenda tufahamu

maana yake kwanza, UTI ni kifupi cha maneno ya kiingereza Urinary Tract Infection (UTI), wazazi wengi wanaujua sana kwa sababu ya watoto chini ya miaka mitano husumbuliwa na ugonjwa huu. Maana halisi ya UTI kwa Kiswahili ni maambukizi katika njia ya mkojo.


Napenda wanawake wanosumbuliwa na UTI wajue kuwa njia ya mkojo sio njia ya uzazi. Wapo wanaofikiri kuwa uke una njia moja ya uzazi na mkojo. Hapana. Njia ya mkojo inaachana na njia ya uzazi mwanzoni tu mwa uke.

Uambukizo katika njia ya mkojo unapatikana kwa njia mbalimbali, tukiacha magonjwa ya kujamiiana, uambukizo

wa njia ya mkojo unasababishwa na bakteria waishio ukeni au kwenye utumbo wa binadamu. Bakteria waishio ukeni hawana madhara ukeni, lakini wakihama na kuingia kwenye njia ya mkojo husababisha matatizo.


Hii inaweza kutokea wakati wa ngono kwani wakati huo msuguano husababisha wale bakteria kutoka na majimaji na kufika kwenye tundu la mkojo na kuingia ndani. Wataalamu wanasema kuwa mwanamke anayefanya ngono

mara kwa mara anaweza kuwa na UTI zaidi ya yule asiyefanya. Bakteria pia wanaweza kuhama kutoka sehemu ya haja kubwa na kuingia kwenye tundu la mkojo.


Hutokea wakati wa kujisafisha na hasa kama mabaki ya kinyesi hubakia sehemu ya haja kubwa. Njia nyingine iwapo mwanamke atakuwa na tabia ya kubana mkojo kwa mda mrefu, kibofu cha mkojo kina misuli inayosadia

mwanamke asiende kukojoa anapobanwa na mkojo mpaka atakapokuwa tayari. Iwapo atahisi kukojoa na asiende baada ya muda mrefu, ataichosha misuli ya kibofu kiasi kwamba hata siku anayokuwa na mkojo akikojoa hautoki

wote na ule mkojo kidogo unaobaki kwenye kibofu huweka bakteria na kusababisha maambukizo. Dalili za UTI ni kujisikia kwenda haja ndogo mara kwa mara na utakapoenda unatoka mkojo kidogo tu. Utasikia mkojo ukichoma

wakati unatoka na mwisho utasikia maumivu makali. Ikiendelea unaweza kusikia maumivu ya chini ya tumbo na kiuno. Hata hivyo, kuna magonjwa mengine yenye dalili kama hizo na ni daktari atakayekusaidia kutofautisha.



Habari njema ni kwamba UTI inatibika kirahisi kwa antibiotiki, lakini unashauriwa kumuona daktari kabla ya kuzitumia kwani wakati mwingine kunywa maji mengi kunasaidia kusafisha njia ya mkojo. Unashauriwa kwenda

haja ndogo mara unapojisikia kufanya hivyo, yaani kutobana mkojo kwa muda mrefu sana, kuhakikisha unajisafisha vizuri baada ya haja kubwa na baada ya kufanya ngono.
AFYA YAKO KWANZA: KUCHANGIA CHOO KUNASABABISHA U.T.I KWA WANAWAKE
 
Asante Dr. MziziMkavu kwa elimu ya UTI kwa wanawake. Ila pia wako wanaume wanaugua UTI, wadogo kwa wakubwa. Nayo inasababishwa na kitu gani? Maana kwa hakika wanawake kwa maumbile yao wako wazi na wanaune siyo. Sasa wanaume wanapataje huu ugonjwa?
 
zamani kidogo UTI ilikuwa haijaenea kama sasa hivi kwa wanawake, na quality of life ilikuwa ipo chini kuliko sasa. je Unasemaje hapo? maana hata watoto wadogo hasa wa kike wanasumbuliwa sana na hii UTI, ENZI zile mimi sikuwahi kusikia UTI ni nini. nimekuja kusikia miaka hii ya utandawazi.
 
Mkuu MziziMkavu nadhani choo kizuri ni
cha kuchuchumaa na si kukaa.
 
Asante Dr. MziziMkavu kwa elimu ya UTI kwa wanawake. Ila pia wako wanaume wanaugua UTI, wadogo kwa wakubwa. Nayo inasababishwa na kitu gani? Maana kwa hakika wanawake kwa maumbile yao wako wazi na wanaune siyo. Sasa wanaume wanapataje huu ugonjwa?
[h=2]Dalili za ugonjwa wa UTI kwa wanaume[/h]
UTI ni nini ?

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea
(bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.

Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata

tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.
Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.

Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI


UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.


Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.

Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi
(risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi
(cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.

Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.
Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika


Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.


Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.cc.@
Zogwale

chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/392855-dalili-za-ugonjwa-wa-uti-kwa-wanaume.html#post5571926
 
Asante sana daktari kwa ufafanuzi. Kwahiyo ugonjwa wa u.t.i hauusiani na kizazi?? Maana nina mdogo wangu anaumwa ugonjwa huu mpaka sasa kashatumia dozi 3 tofauti tofauti anazopewa na daktari na kila baada ya kumaliza akienda kupima bado iko pale pale. sasa wenzie wanamwambia kuwa kama bado ipo inaweza kuharibu kizazi. Xa na mimi dada ake nashindwa kumjibu cz cjui kama ni kweli inamadhara hayo. ameshakata na tamaa. Naomba unihakikishie juu ya hilo na yeye pia nimtie moyo tafadhari doctor.
 
Dr. MziziMkavu asante sana kwa maelezo mzuri kuhusu UTI. Yote yamezingatiwa. Nichukue fursa hii kukushukuru kipekee kwa kutenga muda wako kutoa mada JF hasa za afya. Hakika nimejifunza mengi sana toka kwako. Keep it up mkuu.
 
Back
Top Bottom