kucheka ni dawa

nlambaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
372
Reaction score
76
Leo nimesikia kupitia kipindi cha BBC asubuhi kuwa huko Kenya kumeazishwa club za kucheka ambapo wapo hukusanyika na kucheka kwa masaa kadhaa. Mwenye hiyo club alihojiwa na kudai kuwa kucheka ni dawa na inawezesha kurefusha maisha ya watu, kitu ambacho naomba kusaidiwa na wana JF ni kama jambo hilo ni kweli na pia kama kunatofauti kati ya kucheka na furaha. Yaani kucheka tu hata kama huna furaha kama wanavyofanya kwenye hiyo club kunasaidia katika maisha yetu haya yaliyo jaa stress nyingi. Nawasilisha.
 
kweli, daktari wangu alinipa dozi ya kucheka dakika moja mara tatu kwa siku. Nina miaka 9 sijaugua homa yeyote ile
 
cheko dawa mdau,ukishacheka moja kwa moja furaha inakuja by default,,,ni sawa na huzuni na kulia
 
Ukicheka mapafu yanapanuka hivyo kurahisisha mzunguko wa oxygen.
 
kucheka kunasaidia sana kufanya relaxation ya muscles na hivyo unakua mwenye afya zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…