Leo nimesikia kupitia kipindi cha BBC asubuhi kuwa huko Kenya kumeazishwa club za kucheka ambapo wapo hukusanyika na kucheka kwa masaa kadhaa. Mwenye hiyo club alihojiwa na kudai kuwa kucheka ni dawa na inawezesha kurefusha maisha ya watu, kitu ambacho naomba kusaidiwa na wana JF ni kama jambo hilo ni kweli na pia kama kunatofauti kati ya kucheka na furaha. Yaani kucheka tu hata kama huna furaha kama wanavyofanya kwenye hiyo club kunasaidia katika maisha yetu haya yaliyo jaa stress nyingi. Nawasilisha.