Elections 2010 Kucheki vitambulisho vya kupigia kura

Elections 2010 Kucheki vitambulisho vya kupigia kura

Mugerezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2007
Posts
456
Reaction score
10
WanaJF naamini wengi wetu kama si wote tutakuwa tumejiandikisha kupiga kura. Lakini kuna huu utaratibu uliowekwa wa kwenda kucheki kama majina yetu yapo. Tafadhari nendeni mkakague kama majina yenu yapo kwenye orodha iliyobandikwa mapema au kwenye tofuti ya NEC www.nec.go.tz kuna utaratibu pale wa kujua kama uko ukoregistered au hapana. Bonyeza hii link The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage.

Tufuatilie ili tuweze kufanya mabadiliko ya ukweli siyo ya maneno tu.
 
Kuna vichekesho kibao mwaka huu.

Mie nimeambiwa siwezi kupiga kura ka sababu fomu yangu imefutwa. Na nikiangalia kitambulisho changu kipo na nimeingiza namba kwenye web site kimenipa data zangu zote.

sasa sijui ni mchezo gani huu kutupunguza wapiga kura.

Ok nimepeleka malalamiko kwa mtendaji wa kata upanga mashariki anashughulikia.
 
La my wife...halipo kwenye makalatasi waliyo bandika tangu juzi tunafatilia ili waliangalie kwenye daftari walicho mjibu jana ni kwamba wako busy, wakamshauli aandike namba 3 aache nafasi kisha aandike namba ya mpiga kura na atume kwenda namba 0753123179 akafanya hivyo hakupata sm yoyote lakini nimelitafuta kwenye tovuti yao nimepata details zote je anapswa kufanya nini baada ya hapo...
 

Mbona kuna namba kwenye daftari hazina maelezo na ziko tupu kabisa bila maelezo ya mtu yoyote tazama namba hizi hapa:-

19272311

19272348

Namba za namna hii zipo nyingi sana, hizi namba nimezipata ofisi ya serikali Buguruni chama.

Nahisi kwenye kupiga kura hizi namba zitatumika, na kwenye daftari litakalotumika kwenye vituo tayari wamejaza majina ya watu.

Mawakala wa vyama, tafadhalini kagueni vitabu kwa kulinganisha na namba zilizowekwa ukutani ambazo hazina majina.

 
Back
Top Bottom