Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Houth walikubali kupokea kipigo kutoka kwa ndege za Marekani na jumla ya watu 59 kufa. Asubuhi yake na wao wakatangaza kuzirushia makombora 18 na droni meli za kivita za Marekani zilizokuwa karibu yao.
Si kawaida kwa nchi ya Marekani hasa chini ya Trump kukaa kimya muda mrefu baada adui zake kutangaza kuishambulia kama inavyotokea huko bahari nyekundu baada ya Houth kutangaza kuzishambulia meli zake za kifakhari za kivita.
Sababu zinaweza zikawa nyingi na mojawapo ikawa ndiyo ya kweli zaidi.Kwanza ni kuwa meli hizo mojawapo imedhurika na shambulio hilo jambo ambalo uwezekano ni mdogo.
Jengine ni kuwa Marekani imeona inapata hasara kubwa bure kwa kupiga kwa hasira wakati adui anayepigwa ana silaha zenye kuleta hasara za bei rahisi ambazo siku inayofuata anazirusha tena.
Bila kufika mwisho wa sababu hizo, nyengine ni kutokana na Houth kupandisha mori wa vita na kupiga marufuku meli zote za Marekani na Israel kukatisha maeneo ya bahari nyekundu na malango ya Mandeb na Hormuz.
Hili ndilo linaloweza kuwa sahihi zaidi kwani Marekani imeona itakuwa ni ngumu zaidi kuendeleza ugomvi na Houth kwani hawataweza kulizuia.
Wakati huo huo afisa wa mambo ya nje wa Houth amesema vita na Marekani ndio kama vimeanza na kwamba wala hawatorudi chini mpaka Israel iache kuipiga Gaza na kuzuia misaada inayosubiri kuingia huko,na mpaka hapo Marekani nayo itakapoacha kuwashambulia.
Afisa huyo wa Houth amesema hawawezi kuacha hata wakiambiwa na Iran kwani wao wanajiamulia mambo yao wenyewe.