swalehe de wise
New Member
- Oct 12, 2017
- 2
- 4
KUCHELEWA KWA MAAMUZI YA KESI.
Kuchelewa kwa kesi ni hali ambayo kesi inachukua muda mrefu Zaidi kuliko ule muda uliowekwa kisheria. Kwa Tanzania tatizo hili bado lipo kwa kesi za madai na jinai na kuna sababu nyingi zinachangia kuwepo na tatizo hili, zikiwepo, uchunguzi wa ushaidi kuchukua muda mrefu mara nyingine hata Zaidi ya miaka minne, pia uchache wa majaji na miundombinu ya mahakama kama vyumba vya mahakama kuwa vichache, kwa mfano mahakama kuu ya Tanzania inapokea mashauri mengi, pia inapokea rufaa kutoka mahakama ya wilaya na mkoa na mabaraza. Jamiiforums mnamo tarehe 19 mwezi wa 6 mwaka 2020 waliliripoti habari ikimuhusisha Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma ambaye alikuwa akisisitiza mahakama zinapaswa kumaliza kesi mapema na wakishindwa watu wanaweza kutumia njia nyingine ambazo ni kinyume na sheria ikiwepo kutumia rushwa. Kuchelewa kwa kesi huathiri Zaidi jamii na hivyo tatizo hilo linapaswa kutatuliwa ili watu waweza kupata haki zao ndani ya wakati.
NYANJA ZINAZOATHIRIKA KUTOKANA NA KUCHELEWESHWA KWA KESI KATIKA JAMII.
Nyanja ya Kiuchumi / biashara.
Katika kesi za madai inapotokea kesi inachukua muda mrefu bila kufika maamuzi husababisha kuyumba kiuchumi au kibiashara kwa mfano mtu amefungua kesi akidai upande mwingine umlipe deni lake, kuchelewa kwa kesi humuathiri mtu huyo kwasababu kiasi anachokidai inawezekana ndo kiasi anachokitegemea katika biashara yake.
Haki za binadam.
Kuchelewa kwa kesi huathiri sana haki za binadam kwa mfano mtu anatuhumiwa kwa kesi ya mauwaji na hilo kosa halina dhamana, hivyo hukaa maabusu hata kwa miaka Zaidi ya mitatu akisubiri uchunguzi wa tukio ukamilike, na hata hivyo Ushahidi unaweza kukamilika na mahakama ikaamua mtuhumiwa hana hatia, na ukumbuke mtu huyu kashakaa mahabusu Zaidi ya miaka mitatu akiwa hana uhuru wa kufanya lolote. Mfano Mashekhe wa Uamsho wamekaa Zaidi ya miaka mitano mahabusu na mwisho wameonekana hawana kesi ya kujibu.
Demokrasia.
Tanzania ina mfumo wa vyama vingi hivyo kuna chama tawala na vyama pinzani, kwa maana hiyo inapotokea mwanasiasa yoyote anapokamatwa kwa makosa kama ya Ugaidi ambapo kosa hilo halina dhamana hivyo humfanya aendelee kukaa mahabusu mpaka pale mahakama itakapo amua kuwa ana hatia au la. hivyo wanasiasa kukaa mahabusu huathiri sana demokrasia kwasababu wakiwa mahabusu wanakosa tena ule uhuru wa kukosoa ama kutoa maoni yatakayo jenga nchi katika misingi ya maendeleo.
Mahusiano / Mapenzi/ Ndoa.
Kuchelewa kwa maamuzi ya kesi muda mwingine husababisha mahusiano au ndoa kuweza kuvunjika katika jamii. Ikiwa kwenye kesi za madai kama mtu anacheleweshewa kesi yake na kiasi anachodai kama kingetoka mapema angeweza kusaidia familia yake akiwemo mkewe, hivyo muda mwingine husababisha kuvunjika kwa mahusiano au ndoa kutokana mwanaume kushindwa kutimizia mahitaji muhimu katika familia. Pia kwenye kesi za jinai mtu anaweza kukaa mahabusu muda mrefu akisubiri uchunguzi ukamilike na hivyo kakaa mahabusu muda mrefu bila dhamana hupelekea mahusiano na wapenzi wao au wake zao kuvunjika kwasababu watu hao huchoka kusubiri hivyo huamua kutafuta mahusiano mapya.
NJIA ZA KUMALIZA TATIZO LA KUCHELEWA KUMALIZIKA KWA KESI NA JINSI JAMII ITAKAVYO FAIDIKA NA MABADILIKO.
Mabadiliko katika sheria.
Sheria zetu zimetoa ukomo wa kesi kuisha ikiwemo kesi za madai lakini sheria zetu zimekuwa kimya kuongelea ambapo inapotokea ukomo ule unapo pitilizwa na kusababishwa kesi kuchelewa Zaidi. Sheria zinapaswa kurekebishwa hapo na kujumuisha kifungu kipya kitakacho elezea ukomo ukipitiliza nini kifanyike.
Pia sheria zetu zinapaswa kuongeza kifungu kingine cha sheria ambacho kitaweza kuanzisha tasisi huru ambayo itaweza kufatilia kesi zinazo chelewa na kama kuna uzembe wa aina yoyote iweze kuwachukulia hatua wahusika.
Pia sheria zinapaswa kutambua haki za binadam ikiwemo kuwapa dhamana watu ambao wanakumbwa na makosa kama uhujumu uchumi na mauwaji. Sheria zinapaswa kuheshimu uhuru wa mtu kuendelea na shughuli zake kabla ya kufikwa na hatia.
Kwahiyo, kama sheria zitaboreshwa katika hizo pande tatu, tatizo na kuchelewa kwa kesi linaweza kuwa historia na jamii wanaweza kufurahia Zaidi kupata haki zao kwa wakati na hiyo itafanya jamii kuwa na Imani Zaidi na mahakama.
Sheria kuwa somo kwanzia shule ya msingi na sekondari.
Baadhi ya kesi huchelewa kutokana tu na watu kukosa uelewa kabisa katika maswala ya kisheria na mahakama, hivyo ni vyema mitaala ya shule zetu ikaongeza maswala ya elimu ya kisheria. Mitaala inaweza kufundisha vitu vya kawaida vya kisheria ambavyo havitawachanganya wanafunzi, kwa mfano umuhimu wa kusema ukwel unapokuwa mahakamani ili mahakama iweze kuamua mapema maamuzi yake kuliko kuizungusha mahakama kwa uongo ambapo hufanya kesi kuchukua muda.
Kuongeza Majaji .
Ni muhimu kwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuliangalia vizuri hili swala, nchi yetu bado inahitaji Zaidi majaji ili kuweza kusaidia haki kupatikana ndani ya wakati, hivyo ni muhimu Zaidi majaji kuongezwa.
Kuboresha miundombinu ya mahakama.
Miundombinu ya mahakama ikiwemo majengo inapaswa kuboreshwa Zaidi kwa kuongeza vyumba Zaidi vya kusikilizia kesi. Hii itaenda sambamba Zaidi ma uongezwaji wa majaji, na mwisho itasaidia kesi kuisha kwa wakati na jamii itaweza kupata haki zao mapema.
Kuanzisha mahakama kuu mikoa yote Tanzania.
Serikali inapaswa kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kujenga majengo ya mahakama kuu Tanzania kwa mikoa yote ambayo bado hakuna kwa mfano Singida hakuna mahakama kuu hivyo inabidi wananchi wenye uhitaji wa mahakama hiyo kuifata mpaka Dodoma, hivyo kufanya mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma kuwa na mashauri mengi zaidi . pia watu wengi wanakosa haki zao kwa kutokuwa na uwezo wa kifedha kuja kusikiliza kesi zao kwa umbali huo. Hivyo kama mahakama kuu zitaongezwa kwa mikoa yote ambayo hamna basi tatizo la kuchelewa kwa kesi halitakuwepo tena na hivyo jamii itaweza kupata haki zao kwa wakati.
HITIMISHO. Jamii yetu inahitaji Zaidi haki tena haki inayopatikana kwa wakati hivyo kama marekebisho hayo yatapata nafasi ya kufanyiwa kazi basi jamii yetu itafurahia haki kwa wakati na haya yatakuwa mabadiliko makubwa sana kwa kumaliza tatizo la kucheleweshwa kwa kesi katika nchi yetu na haki za watu kupatikana ndani muda.

Upvote
2