KERO Kuchelewa kwa Madaktari kutoa huduma Muhimbili, wengi wanaanza kuhudumia wagonjwa saa 5 Asubuhi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

lagon

Member
Joined
May 17, 2018
Posts
7
Reaction score
19
Nimekuwa nikihudhuria Muhimbili kwa takribani mwezi sasa. Ukweli wagonjwa wanachukua muda mrefu sana kumsubiria Daktari afike. Madaktari wengi wanaanza kusikiliza wagonjwa kuanzia SAA TANO asubuhi wakati kuna watu wamefika toka saa kumi na moja asubuhi.

Nashindwa kuelewa wanakuwa wapi alafu ni almost wote, wachache wanaingia clinic ya saa kumi na mbili na nusu ila wale wa saa tatu utawaona saa tano na wakifika wala hawana masiwasi wataanza na watu wao kwanza wanaowajua mpaka uje uitwe mwenye namba ni saa sita huko.

Haya ni mateso na manyanyaso kabisa. Sahivi kila mtu anajiamulia mambo tuu atakavyo jisikia.
 
Wakifungua maduka mikao ya pwani saa 12 alfajiri , wataitwa wavivu .
 
1. Daktari anapanga bunju.
2. Mke anafundisha Tandael, hivyo mume anampeleka shule.
3. Watoto wanasoma Kawe-Ukwamani, Doctor inabidi kumpeleka mtoto.
4. Daktari anaendesha Vitz Plaz ya mkopo, kwa siku anasimamishwa na Traffick zaidi ya mara nne.
5. Gari haina kimuli-muli, daktari anapisha wenye vimulimuli akifika muhimbili kachelewa anakuta waliopita na vimulimuli walikuwa wanawahi hospitali na ndio wamesababisha daktari kuchelewa maana aliambiwa apishe msafara.
6. Akiifika inabidi anywe chai maana hata wewe ulikunywa ndio ukaja hospitali, sasa nani alaumiwe?

USHAURI: - Madaktari ndio walikuwa wanapaswa kuwa watu wa kwanza kupewa magari maalum, VX-V* za mwaka wa mbele na vingora ili kuwahi dharura!

Kupanga ni kuchagua.
 
uvivu tuu na upuuzi, mkurugenzi naye fala tuu
 
Kwa dunia ya sasa, jitahidi sana kuilinda afya yako kwa gharama kubwa uwezavyo; daktari bingwa huwezi kumpangia muda, anajipangia mwenyewe. Kwa fani zingine sawa, ila kwa hawa wenye hizi fani za kusogeza uhai wa watu mbele, ni ngumu kuwadhibiti.​
 
Kwa dunia ya sasa, jitahidi sana kuilinda afya yako kwa gharama kubwa uwezavyo; daktari bingwa huwezi kumpangia muda, anajipangia mwenyewe. Kwa fani zingine sawa, ila kwa hawa wenye hizi fani za kusogeza uhai wa watu mbele, ni ngumu kuwadhibiti.​
Bora uwasemee madaktari, tena ukute specialist, woii!
 
Akili ya mtu mweusi haijawahi kubadilishwa na elimu ya kimagharibi! Tukishapata madegree tunarudi kwenye default settings!

Kwani idara gani au sehemu gani kuna efficiency na effeciveness tukiacha udaktarini?
 
Bora uwasemee madaktari, tena ukute specialist, woii!
Kwa huu ulimwengu wa kibepari, tujitahidi sana kula vitu vya asili ili kulinda afya zetu, ili kupunguza kasi ya kuhudhuria gereji (hospitali) mara kwa mara.
 
Kwanza pole
Mimi sio daktari ila naomba nichangie hoja, nilipata ajali ya pikipiki 2023 nikapata right elbow dislocation. Baada ya kutibiwa haspitali mbalimbali ikanilazimu nipelekwe MOI. Mwanzoni niliona madaktari wanachelewa sana kutoa huduma ila nilipozidi kuhudhuria kliniki niligundua kuwa Hawa madaktari wanafanya kazi kubwa sana. Kunawakati anatakiwa kliniki saa 3 asubuhi kabla ya hapo yupo chumba Cha operation, kunawakati yupo na madaktari wanafunzi nk. Hawa madaktari wanafanya mambo mengi nyuma ya pazia ambayo wagojwa hawayajui. Sio tu kuchelewa sikunyingine unaweza kwenda kliniki ukaambiwa daktari hajatoka oparesheni, amekutana na complications huko uje siku nyingine utakayopangiwa.

Ukweli ni kwamba lengo la mgonjwa yeyeto akienda hospitali anahitaji atibiwe kwa haraka Ili apone ila tusiwalaumu sana Hawa madaktari kunakitu wanafanya. Nakumbuka daktari wangu alikuwa Dr. Nchimbi pale MOI yule mtu Mungu ampe Mema ni dokta na nusu. Kwa namna mkono wangu ulikuwa sikuwai amini kama nitaweza kuutumia tena maishani Leo Niko safi nafanya Kila kitu.
 
daktar wa afya yako ni wew mwenyewe hao wengine wapo kibiashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…