Wananchi wa Kata ya Nyatwali waliamuriwa na Serikali kupisha eneo hilo ili pawe mapito ya wanyama pori mpaka Ziwa Victoria na wanyama waweze kuchunga na kunywa maji kwa urahisi. Wananchi walifanyiwa tathmini ya maeneo yao, mali zao na sasa imekwishapita mwaka moja na nusu tangu kufanyika kwa tathmini hiyo. Kama ilivyo sheria ya ardhi ni kuwa tathmini ikifanyika na ikapita miezi sita bila malipo basi waathirika wanatakiwa wafanyiwe tathmnini upya au walipwe nyongeza ya 7%. Hivyo wananchi wa Nyatwali wanastahili nyongeza ya asilimia 7% pindi watakapolipwa vinginevyo suala hili litapelekwa mbele ya sheria ili wananchi hawa wapate haki yao kama sheria ya ardhi inavyotamka.