Baraza la Mitihani Tanzania (Necta)
limesema usahihishaji wa mitihani ya
kidato cha nne uliofanyika Novemba
mwaka jana, umekamilika. Hatua hiyo
inafuatia baadhi ya wanafunzi
waliomaliza kidato cha nne kuwa na
shauku ya kutaka kufahamu
walichovuna kutokana na kukaa
darasani kwa miaka takribani minne.
Kwa mujibu wa Katibu mtendaji wa
Necta, Dk Charles Msonde amesema
kuwa usahihishaji umekamilika na
baraza lipo katika uchambuzi wa
kuyapanga na yatakapokamilishwa
watayatangaza.
Aidha, Katika kipindi cha miaka miwili
mfululizo, mwaka 2012 na 2013, Necta
ilitangaza matokeo ya kidato cha nne
mwishoni mwa Februari na mwanzoni
mwa Machi.
Katika hatua niyinge muhula wa
masomo kwa kidato cha tano huanza
Julai, huku mwezi Machi na Aprili
mchakato wa kuwapangia shule
hufanyika wakati Mei na Juni hutumiwa
kwa maandalizi ya kuripoti shule
wanafunzi waliofaulu mtihani huo.