Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

4. Leo tumeona barua ambayo Zito na watu kadhaa wameandika barua World bank kuhusu tanzania kunyimwa msaada wa billion 500 kusaidia masuala ya elimu..umeona response ya mkuu wa nchi amesema tuwapuuzeni tu hao.
Ingekuwa ndiyo Lisu kaandika pangechimbika...Je Zito ni nani?
Nakushukuru sana kwa kuiandika hii, kwa sababu nilianza kukutilia mashaka na mada yako hii.

Haya tuendelee...
 
blindspot,

Mkuu Blindspot, una hoja au huna hoja, lakini hustahili kupuuzwa.

Ni mada inayostahiri kupimwa kwa kina. Ngoja nitafakari haya mazito uliyoweka hapa, tena kwa mpangilio mzuri kabisa.

Lakini..., hata Lissu kaingizwa mkenge, au.... Hakutahadharishwa na chama chake?

La kushangaza zaidi, ni huu uvumilivu iliokuwa nao timu nzima ya mtu asiyependa kuhojiwa chochote..., kulikoni hapa?

Na kwa upande wa pili; anayoyaandika na kuyazungumzia Mh Zitto ni mambo makubwa sana kiasi kwamba yanaweza 'kuupuzwa' tu kwa sababu wanajua anachofanya...HAPANA, sio rahisi kiasi hicho.

Mh Zitto anachimbua hasa. Hii sio gelesha tu ya kuwaweka watu usingizi.

Mkuu 'Blindspot' bado unayo hoja ya kujibu. Bado hujashawishi vya kutosha. Mwaga mtama zaidi.

Kwa hapo ulipoishia, wewe mwenyewe unaweza kuwa sehemu maalum ya kuwalaza akili watu, ukiwa upande wa hao wanaopigwa mawe. Huu mchezo unahitaji akili kubwa kuutambua eti!
 
ZZK aligombea ubunge this time anangukia pua. Labda sujui atapenyea wapi? Kwanini alipakimbiabl Kigoma kaskazini baada ya kuwa Mbunge for 10 years?

Safari hii ZZK atagombea Urais huku akijua anafeli; na kura zake wala hazitafika nusu ya Kura za Dr. Slaa 2010.

Kwa kuwa ZZK ndiye flag career wa ACT Wazalendo kwenye Urais maana yake hawezi kugombea ubunge hapo hapo na nafasi yake atabakia Kiongozi Mkui wa ACT maana hata ubunge sidhani kama atapata kwa Kigoma.
Bare in Mind CCM ya sasa wana a lot of strategies za kushinda na kwenye ushindi wa good straregist, the end justifies the means huo ndio mwendo ambao uliwasaidia akina Trump kuwa Rais US 2016 na Bush kuwa Rais wa US 2000.

ZZK hata leo uchaguzi uitishwe Kigoma; atashangaa kashindwaje. Tukumbuke jimbo la Buyungu, akina ZZK walipigwa kwa "mikakati" na wakabaki wanabung'aa.

Era ya ZZK bungeni has come to and END. JPM kwa jinsi alivyo huwa hanaga degree ya tolerance kwa mtu kama ZZK.

Labda muujiza utokee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe siyo "mwenzao"?

Seif siyo "mwenzao"?

Lipumba siyo "mwenzao"?

Cheya siyo "mwenzao"?

Walioanzisha vyama vyote vya upinzani siyo "wenzao"?

Kifo cha CCM kitatoka CCM kwenyewe na kutokea kwa hao hao wenzao.

Siasa ni mchezo mbaya sana.
 
Maneno meeengi lengo kutuaminisha CHADEMA ndio chama cha viongozi Malaika.

Jiwe walilolikataa waasi limekuwa jiwe tena.


Mwambie Yericko na Mnyika watunge hekaya nyingine ya kumpoteza huyo MZITTO.


Unamaoni gani kuhusu Zito kuwa nyoka
 
Bado haujajibu swali kwann Zito asumbiliwi. Zito anavujisha mangapi.. kwann nguvu kubwa wanapewa chadema
Duh Mkuu Blindspot, nijibu mara ngapi na nimeishakujibu kuwa Zitto anaikosoa serikali kwa kutumia hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu, yuko makini sana kwenye kuchagua maneno yake na kauli zake, hivyo hawana pa kumshikia.

Mfano Tundu Lissu alipobaini kuna gari linamfuatilia, aliitisha press conference na kutangazia umma, kisha akatulia, angekuwa ni Zitto, angeanzia kuripoti kwanza polisi na kunakohusika, kisha kufanya press conference, unadhani wasiojulikana wangeendelea kumfuatilia?.

Wapinzani wengine wengi wanaingia matatizoni kutokana na uropokaji, Zitto ni mjengaji hoja mzuri na ni strategist.

Chadema, ukimuondoa Zitto na Prof. Kitila Mkumbo, haina kabisa ma strategists.

Angalia mfano mwingine huu wa Zitto alipotuhumiwa kupika data, msikilize anachosema



P
 
Pascal Mayalla, Mimi sijakuelewa, Strategist kwa maana ipi! Kupambania wananchi, kupambania chama chake au kuhakikisha mlo wake?
Binafsi mimi hapo juu sina jibu lolote na inawezekana kweli njama za kuhakikisha uliyesema ni jiwe kweli kweli zikafanikiwa kumuweka madarakani kwa hila au mabavu na wabunge wake wa kutosha.

Lakini Pasco unadhani ujinga na unyonge wa Watanzania kuporwa haki yao ya kuweka viongozi watakao itadumu hadi lini? Na jee mwisho wa hao wanao ipoka utakuwa wa aina gani?

Tumeona nchi zilizokuwa na nguvu kubwa na watawala wenye nguvu zikiyeyuka kama barafu na hao "maJiwe" wakiingizwa kwenye ma crusher na kugeuka kokoto au vumbi.

Tukumbuke, hata wanajeshi, polisi, mgambo na sungusungu nao ni wananchi wapiga kura na wanaweza kuchukia.
Watawala wasijione wana strategic bora sana kupora utashi wa raia wakaishia kuangua kilio mitaroni kama Gaddafi ambaye sio tuu alikuwa na nguvu Libya, bali Afrika nzima alikuwa na kauli.
Ni ushauri tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
blindspot,
ulichokisema kwenye hili bandiko lako ndiyo hasa lengo la chama chetu (CCM).... kwamba hakikisha mpinzani aliye imara zaidi hawi tishio kwa kumdhoofisha asiunganishe nguvu na wapinzani wenziwe.

so, tunapanda mbegu ya mashaka kati ya mpinzani imara vs wenziwe ili wasiaminiane kwa kumnyanyasa aliye imara zaidi na kutowagusa wale wengine!

hichi ndicho sisi CCM tunakifanya ili Chadema wasiimarike kwa kuunganisha nguvu na wapinzani wengine kama ACT.

kwa hiyo mleta mada wewe ni ama kada mwenzetu au la sivyo basi hujang'amua (ni ignorant wa) janja ya chama chetu!
 
Unamaoni gani kuhusu Zito kuwa nyoka
Nimsaliti tangu tukiwa pale mlimani ni mbinafsi pia na hatufai kuwa rais wa nchi hii. Uzuri na utamu wa uchaguzi mkuu ukizingatia watu walivyopinda sasa hivi hautabiriki asije akajidanganya mtu kuwa itakuwa mteremko kwa wanasiasa kupenyeza na kuuchukuwa ubunge mwezi wa 2020
 
Zitto sio nyoka bali ni strategist

P
Nakubaliana nawe 100%
 
Back
Top Bottom