Kucheza kimapenzi

Kucheza kimapenzi

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Kucheza kimapenzi





Katika moja ya misingi ya kujenga mahusiano kati ya mke na mume ni pamoja na mke na mume kuwa na muda wa kucheza pamoja.

Kabla hatujafika mbali hivi ni lini wewe na mume wako au mke wako mmekuwa na muda wa kucheza pamoja?

Kama ni ndiyo basi ubarikiwe na kama hukumbuki ni lini bado hujachelewa ndiyo maana umekuja kusoma hapa ili nikukumbushe.

Kucheza pamoja kwa mume na mke husaidia kujenga urafiki na ndoa kwani ndani ya kucheza kuna interest na vicheko na pia kucheza pamoja maana yake unajali (caring).

Kujenga mahusiano ni pamoja na mke na mume kuwa marafiki na kuwa marafiki ni pamoja na kuwa na muda wa ku-enjoy pamoja kwa kucheza na matokeo yake ni kila mmoja kumuhitaji mwenzake mara kwa mara kwa kuwa kuna kitu mnacho in common.

Tuache kucheza michezo mingine tuangalie kucheza kimapenzi.
Je, ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kucheza mchezo wowote wa kimapenzi (sexual play)

Kwanza, lazima muwe ninyi wawili tu.

Pili, mnahakikisha kuna kuheshimiana katika kuchagua mchezo mnaotaka kucheza.

Tatu, mchezo wenu hauwezi kusababisha maumivu kimwili, hisia na kukwazana kiroho.

Nne, mnahakikisha mchezo wenu una msingi katika mahusiano yenu.
Na tano hakuna kuingiliana kimapenzi (no genital union)

(A Husband Shares Common Interests with the Woman of His Dreams by Playing Together
 
Maisha yenyewe kisago kikali ukirudi kushughulika unakuwa umepigika vibaya vibaya hata hiyo tumbaku yenyewe unanusanusa kidogo na ukitaka kuongeza uvutie vutie...aaah maisha gani haya...ya chini ya dola moja kila siku...hata hizo ny****** zenyewe haziji.
 
Mchezo wa kimapenzi ambao ni bomba ni kombolela na kubebana mgongoni.🙂
 
Kwa kuwa umeleta shule basi ungetufundisha ni michezo ipi hiyo? kuliko kuishia kutuambia tu tucheze!
Njoo na mifano bwana!
 
haya mambo ni kwa wasio fikiria watakula nini kesho bali wanaowaza mipango ya miaka mingi ijayo
 
PDidy, michezo ya kimahaba ni mizuri sana... lakini ukiweza kwenda mbele zaidi mkaweza kuwa na zile evening brain teasers, darts, pool, table tenis, karata, watching sports or movie, scrabble, monopoly (coupled with good drink) utaona kabisa yoote hayo yanaandaa mazingira mazuri sana ya mapenzi mix na bedminton!!!

Tatizo nyumba zetu mazee, hata ukiachia ushuzi watoto wanasikia
 
Eh! Pretty unapenda kubebana mgongoni na kombolela eh! 😉
waswahili walisema, kula nanasi kwahitaji nafasi... sasa wenzangu namimi chumba kimoja, kitanda, kabati, stoool, meza na kila kilicho chetu humo humo... hilo kombolela utalichezaje? ukirusha mpira akishindwa daka mara puuu kabati la vyombo, glass mbili meng'emeng'e.
 
kwa kuwa umeleta shule basi ungetufundisha ni michezo ipi hiyo? Kuliko kuishia kutuambia tu tucheze!
njoo na mifano bwana!

mpwa watu wazima awamezeshwi yote mengine tunaenda google.com
 
waswahili walisema, kula nanasi kwahitaji nafasi... Sasa wenzangu namimi chumba kimoja, kitanda, kabati, stoool, meza na kila kilicho chetu humo humo... Hilo kombolela utalichezaje? Ukirusha mpira akishindwa daka mara puuu kabati la vyombo, glass mbili meng'emeng'e.

hiyooo ndio cheers yenyewe yawezekana mligonganisha cheers mara ya mwisho siku ya harusi
 
Hapa michezo ya mapenzi anayelenga huyu nadhani ni vile kutekenyana tekenyana, maana huwa inaleta vicheko vya hapa na pale.
 
waswahili walisema, kula nanasi kwahitaji nafasi... sasa wenzangu namimi chumba kimoja, kitanda, kabati, stoool, meza na kila kilicho chetu humo humo... hilo kombolela utalichezaje? ukirusha mpira akishindwa daka mara puuu kabati la vyombo, glass mbili meng'emeng'e.


Hilo nalo neno!!!!!!
 
Hapa michezo ya mapenzi anayelenga huyu nadhani ni vile kutekenyana tekenyana, maana huwa inaleta vicheko vya hapa na pale.

Hapo ndio penyewe. Ila inategemea unatekenywa nini. Lol!
 
Duu michezo kweli muhimu ila naomba angalau ututajie aina ya michezo ili tukaiapply, sabab....
 
Hapa michezo ya mapenzi anayelenga huyu nadhani ni vile kutekenyana tekenyana, maana huwa inaleta vicheko vya hapa na pale.

Kutekenyana si ndo mtaishia kumegana? Point no 5 hapo juu anasema hakuna kuingiliana kimwili!
 
Back
Top Bottom