SoC03 Kuchochea uchumi: Serikali iwastaafishe watumishi wa umma wenye miaka zaidi ya 50 na kuajiri vijana kuziba pengo hilo

SoC03 Kuchochea uchumi: Serikali iwastaafishe watumishi wa umma wenye miaka zaidi ya 50 na kuajiri vijana kuziba pengo hilo

Stories of Change - 2023 Competition

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Itungwe sheria ya dharura itakayofanya kazi kwa kipindi kifupi (yaani sheria ya mpito).
Kila mtumishi wa umma mwenye umri wa miaka 50 na kuendelea astaafishwe kwa lazima na nafasi yake aajiriwe mtumishi mpya kijana wa miaka 18- 45.

Ajira hizi za kuziba mapengo zisihesabiwe na kujumlishwa kwenye zile ajira za mwaka zinazotolewa na serikali. Kwa namna nyingine niseme neno ZISIATHIRI ajira zilizo kwenye bajeti kuu ya mwaka.
Hili litachochea maendelea na uchumi wa nchi kwa sababu hizi;

●Wastaafu watalipwa fedha ambazo zitaongeza mzunguko mitaani. Serikali itapata kodi kutokana na manunuzi mbalimbali yatakayofanywa na wastaafu na familia zao.
●Vijana watakaoajiriwa kuziba pengo la wastaafu watakwamuka na umaskini pamoja na familia zao na kuongeza mzunguko wa fedha mtaani.
● Kutaibuka viwanda vidogo na vya kati vingi , kuna Watanzania, wakiwemo baadhi ya watumishi wa umma wanapenda kuwekeza kwenye viwanda vidogo lakini hukwama kwasababu ya kukosa mitaji. Hivyo wapo kati ya wastaafu watakaowekeza kwenye viwanda vidogo na vya kati pindi tu wakilipwa mafao yao ya kustaafu. Hivyo sekta binafsi itakua na ajira kuongezeka.
●Kutaibuka hari mpya katika ofisi za umma kutokana na ujio wa vijana wasomi na wenye nguvu mwilini. Hivyo shughuli za maendeleo zitakwenda haraka.
MImi si mhanga wa ajira. Ni mtumishi mtiifu wa serikali kwa miaka 8 sasa, hivyo uzi huu sijipigii sebe nyuma ya ukuta.

Asante.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom