Nilisoma vitabu vya historia, kutokana na medical technology ya wakati huo, vifo kutokana na TB, malaria na magonjwa ambukizi mengine vilikuwa ni vingi sana.
Wa missionary waliokuja kueneza dini walijua kabisa wakienda Africa maisha yao yakizidi miezi mitatu ni kwa bahati na uwezekano wa kurudi kwao wakiwa hai ni mdogo sana. Hivyo walichonga mawe ya kuweka kaburini yakionyesha jina na tarehe ya kuzaliwa.
Hali hii ninaifananisha na kupangiwa kazi Kibiti kwa sasa hivi. Ukipata barua ya ajira inabidi uchonge na jiwe la kuweka kaburini uwende nalo.