Kuchonga jiwe la kuweka kaburini

Kuchonga jiwe la kuweka kaburini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nilisoma vitabu vya historia, kutokana na medical technology ya wakati huo, vifo kutokana na TB, malaria na magonjwa ambukizi mengine vilikuwa ni vingi sana.

Wa missionary waliokuja kueneza dini walijua kabisa wakienda Africa maisha yao yakizidi miezi mitatu ni kwa bahati na uwezekano wa kurudi kwao wakiwa hai ni mdogo sana. Hivyo walichonga mawe ya kuweka kaburini yakionyesha jina na tarehe ya kuzaliwa.

Hali hii ninaifananisha na kupangiwa kazi Kibiti kwa sasa hivi. Ukipata barua ya ajira inabidi uchonge na jiwe la kuweka kaburini uwende nalo.
 
Aisee hali ya huko sio kabisaa, sijui hao watumishi wa serikali na polisi wanaishije jamani!!
 
Watumishi Waliouawa tangu mwanzo ni polisi na hao serikali za mitaa, wengine hawaguswi,inaonekana kama hawahusiki na mkasa unaoleta mauaji,
 
Kila mtu atakufa ila kabla hujafa lazima ulipie dhambi zako.
Natarajia wahusika watakamatwa
 
Demands za wauwaji sijui ni nini waweke wazi mbona al shabab Al Qaeda wote wanasema labda tatizo litaisha
 
Kama wewe si mwenyeketi,mtendaji,mjumbe wala askari,Maisha ya kibiti yako safii tuu
 
Minikipangiwa huko namwambia mzee wangu anigawie kabisa urithi wangu nikafariki nikiwa nishautafuna
 
Back
Top Bottom