Kuchukua gari car Yard DSM vs kuagiza kutoka nje, budget - aina ya gari

Kuchukua gari car Yard DSM vs kuagiza kutoka nje, budget - aina ya gari

sisi ni ndugu

Senior Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
121
Reaction score
136
Habari za jioni wataalam.

Msaada wa ushauri, kuna budget ya 15M nahitaji toyota ya kuzugia mjini, napendelea sana toyota premio isiyozidi 1500cc , je ni nzuri au unashauri nichukue aina gani? Je utaratibu mzuri ni kuagiza au kwenda yard kujichagulia?

Naomba ushauri wenu wataalam.
 
Najua iyo pesa inakuwasha inataka gari leo kesho. Ila kuwa na subira agiza nje bàada ya miezimiwili unasukuma ndinga saaafi. achana na hizi za yard
Mkuu naomba kidogo utoe prons and cons za both yard and nje ukiagiza ndinga yako.

Naomba ili tujifunze wengine.pia Nina swali lingine ivi mfano naagiza zero mileage Kama hizi V8 afu nalipa kesho 400M Tzs.

Je, sitafuatiliwa na serikali kuhusu mapato yangu TRA labda hiyo hela nimeipataje.

Hii imekaaje mkuu Kama unao utalaamu ufanunuzi tafadhali
 
Mkuu naomba kidogo utoe prons and cons za both yard and nje ukiagiza ndinga yako. Naomba ili tujifunze wengine.pia Nina swali lingine ivi mfano naagiza zero mileage Kama hizi V8 afu nalipa kesho 400M Tzs...
Boss wafanyabiashara wengi wa magari ya yard hapa bongo ni makanjanja sana. Wanauza magari yaliyotumika mda mrefu japan au yaliyopata demage kubwa ambao kule wanayanunua kwa bei karibu na bure. Wakiyaleta huku wanayakarabati lakni pia wanacheza na odometer kurudisha nyuma milege gari ionekane imetembea km kidogo.

Lkn pia biashara ya magari yard ni ngumu sana saivi so wanachofanya wanakodisha sana magari kwenye misiba, harusi, misere ya mtu binafsi kwa malipo na muda maalum. Niliwahi kukodi rav 4 moja yard nikaitumia wiki mbili then then nikairudisha ikawekwa tena sokoni.

Ili kununua gari ya yard nzuri inabidi uwe na utaalam kweli kwelk au fundi unayemjua anayeyajua magari ili usipigwe. Na ukiridhika na gari lipa na kuondoka nalo siku iyo iyo usiache ilale hard watabafilisha spea.

Angalizo. Sio wote ila ni wengi.

Kuhusu kulipa ml 400 keshi gari ya 0 km na usumbufu wa TRA kwa kweli sijui maana binafsi aijawahi agiza v8 ya hela iyo wala sipo kwenye system za TRA mkuu.

Ila kama huna haraka na gari bora uvumile tu hozi wiki sita fata process zote chombo kinatua bandari ya salama.

Nashindwa kutoa changamoto za kuagiza coz siku hizi system za kuagiza kuna usalama mkubwa sana. Labda meli ikizama au kuibiwa baafhi ya vifaa vya ndinga bandarini
 
Mkuu naomba kidogo utoe prons and cons za both yard and nje ukiagiza ndinga yako. Naomba ili tujifunze wengine.pia Nina swali lingine ivi mfano naagiza zero mileage Kama hizi V8 afu nalipa kesho 400M Tzs...
Kufuatiliwa ni lazima na utapigwa maswali ya kutosha,lazima uwe na maelezo ya hiyo ela namna ilivyopatikana,yote ayo ni kwa ajili ya kuzuia money laundering,otherwise ingekua ni easy tu watu kutakatisha fedha
 
Habari za jioni wataalam. Msaada wa ushauri, kuna budget ya 15M nahitaji toyota ya kuzugia mjini, napendelea sana toyota premio isiyozidi 1500cc , je ni nzuri au unashauri nichukue aina gani? Je utaratibu mzuri ni kuagiza au kwenda yard kujichagulia?? Naomba ushauri wenu wataalam
Nenda yard kanunuwe gari acha miluzi mingi, mimi naelewa kote kuagiza na kununuwa Bongo.
Uko Japan kwenyewe usipotumia kampuni ya maana unaletewa gari tofauti na uliyowekewa picha mtandaoni.
 
Kifupi hakuna tofauti ukinunua japan au bongo zote zitabakia kua refurb cars . Kinacho bakia ni wewe na mahitaji kwa muda stahiki.

Sema usinunue kwa madalali ata kama ni mpya, gari inatoka japan na kilometer 160,000 ikifika bongo iyo gari inaoshwa vizuri,polish safi afu kilometre zinarudisha 65,000
 
Boss wafanyabiashara wengi wa magari ya yard hapa bongo ni makanjanja sana. Wanauza magari yaliyotumika mda mrefu japan au yaliyopata demage kubwa ambao kule wanayanunua kwa bei karibu na bure...
Thank you be blessed ndugu.

Ninashukuru mno mno mno mno Tena mno mpaka nakosa Cha kukupa ama kuongea Ila Sina zaidi ya neno thank you.
 
Kufuatiliwa ni lazima na utapigwa maswali ya kutosha,lazima uwe na maelezo ya hiyo ela namna ilivyopatikana,yote ayo ni kwa ajili ya kuzuia money laundering,otherwise ingekua ni easy tu watu kutakatisha fedha
Thanks mkuu. Mana watanicheki tra nilicholipa Kodi ni kidogo ama hakiendani na hela nayomiliki
 
Duu Nina Imani mapato hayalingani kabisa.
Punguza ujanja ujanja sasa mkuu, na lipa kodi kama inavyostahili, kwa sababu ipo siku utakamatwa na hautakuwa na pa kutokea, utajikuta unapoteza vyote ulivyonavyo...kama wanavyosema za mwizi ni arobaini, ipo siku tuu
 
Anzia kule juu wao utajiri walio nao unalingana na mapato TRA kweli. Cheki mtu anamiliki ten bilioni halafu huko TRA hata hajalipa nusu bilioni ifike
 
Habari za jioni wataalam. Msaada wa ushauri, kuna budget ya 15M nahitaji toyota ya kuzugia mjini, napendelea sana toyota premio isiyozidi 1500cc , je ni nzuri au unashauri nichukue aina gani? Je utaratibu mzuri ni kuagiza au kwenda yard kujichagulia?? Naomba ushauri wenu wataalam
Mkuu nenda beforeward chagua gari unayoitaka omba invoice,nenda office zao hapa Dar uende na copy ya invoice lipa watumie Japan. Gari itachelewa kama miezi 2 kwa Sababu ya paper works na shipping time, ila utasave around 2m kuliko yard
 
Habari za jioni wataalam. Msaada wa ushauri, kuna budget ya 15M nahitaji toyota ya kuzugia mjini, napendelea sana toyota premio isiyozidi 1500cc , je ni nzuri au unashauri nichukue aina gani? Je utaratibu mzuri ni kuagiza au kwenda yard kujichagulia?? Naomba ushauri wenu wataalam
Tatizo la yard wana tabia ya kurudisha kilometa za gari nyuma,inaoshwa safi. Ukiiona unasema ipo vizuri kumbe watu washatembelea hapa bongo muda sana.

Watu hua ndio wanafanya hizo kazi za kurudisha kilometa nyuma, kua makini na wabongo
 
Back
Top Bottom