Kuchukua gari car Yard DSM vs kuagiza kutoka nje, budget - aina ya gari

Kuchukua gari car Yard DSM vs kuagiza kutoka nje, budget - aina ya gari

Kufuatiliwa ni lazima na utapigwa maswali ya kutosha,lazima uwe na maelezo ya hiyo ela namna ilivyopatikana,yote ayo ni kwa ajili ya kuzuia money laundering,otherwise ingekua ni easy tu watu kutakatisha fedha
Acha kumtisha mwenzako, watu wanaagiza scania 100 kwa mkupuo, watu wanaagiza yutong 40 kwa mkuouo, kuna mwamba kaagiza howo 300, itakuwa vx ya mil 400? Achen roho za kimaskini
 
Boss wafanyabiashara wengi wa magari ya yard hapa bongo ni makanjanja sana. Wanauza magari yaliyotumika mda mrefu japan au yaliyopata demage kubwa ambao kule wanayanunua kwa bei karibu na bure. Wakiyaleta huku wanayakarabati lakni pia wanacheza na odometer kurudisha nyuma milege gari ionekane imetembea km kidogo.

Lkn pia biashara ya magari yard ni ngumu sana saivi so wanachofanya wanakodisha sana magari kwenye misiba, harusi, misere ya mtu binafsi kwa malipo na muda maalum. Niliwahi kukodi rav 4 moja yard nikaitumia wiki mbili then then nikairudisha ikawekwa tena sokoni.

Ili kununua gari ya yard nzuri inabidi uwe na utaalam kweli kwelk au fundi unayemjua anayeyajua magari ili usipigwe. Na ukiridhika na gari lipa na kuondoka nalo siku iyo iyo usiache ilale hard watabafilisha spea.

Angalizo. Sio wote ila ni wengi.

Kuhusu kulipa ml 400 keshi gari ya 0 km na usumbufu wa TRA kwa kweli sijui maana binafsi aijawahi agiza v8 ya hela iyo wala sipo kwenye system za TRA mkuu.

Ila kama huna haraka na gari bora uvumile tu hozi wiki sita fata process zote chombo kinatua bandari ya salama.

Nashindwa kutoa changamoto za kuagiza coz siku hizi system za kuagiza kuna usalama mkubwa sana. Labda meli ikizama au kuibiwa baafhi ya vifaa vya ndinga bandarini
Kuvumilia ni nyepesi kama inakuwa gari yako ya upili! Gari ya kwanza ni ngumu mno kuvumilia
 
Nashukuru sana wataalam kwa michango yenu, nafanya maaamuzi kwa kuzingatia maoni yenu
 
Back
Top Bottom