Kudai Katiba Mpya kuna kosa gani kisheria?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Hivi polisi hawa ambao ama kwa makusudi au hawaelewi kitu, kudai katiba mpya kuna kosa gani kisheria?

Hivi unapomkamata mtu ambaye anadai kitu ambacho kimeruhusiwa kisheria utakua unaelewa nini?

Au ukampiga mtu na kumuua au kumuumiza sababu tu amedai katiba mpya ambayo ni haki, ukifunguliwa kesi mahakamani utaponea wapi?

Unachochea na kiongozi wa kisiasa ambaye yeye maisha yake ya kisasa ni mafupi kuliko nafasi yako wewe kwenye utumishi
 
Hawa polisi ni vijakazi na watumwa tuu.. Wanatekeleza maagizo toka juu.. Na huko juu kuna nguvu nje ya mfumo ambayo haitaki kabisa kusikia habarj za katiba mpya.

Hizo nguvu zimetajirika na kufanya uchafu mwingi kupitia udhaifu wa katiba ya sasa..wana hofu kubwa na katiba mpya kwakuwa kama ikija basi future zao na mirija yao ya upigaji na unyonyaji itakatwa milele na pengine wengine kufilisiwa.

Hivyo hawa ndio wafadhili wa uovu wote wanaofanyiwa wote wanaoongoza mapambano ya kudai katiba mpya
 
Nyamaza ndugu yangu, utaitwa gaidi sasa hivi kwa kutaja tu neno 'katiba'
Ukipeleka kesi mahakamani kuhoji 'TOZO' nayo unaambiwa kuwa wewe sio raia!
 
Hivi polisi hawa ambao ama kwa makusudi au hawaelewi kitu, kudai katiba mpya kuna kosa gani kisheria?

Hivi unapomkamata mtu ambaye anadai kitu ambacho kimeruhusiwa kisheria utakua unaelewa nini?....
Cha msingi ni kudai katiba mpya kwa kufuata sheria na si kuhamasisha vurugu.
 
C mmeshaambiwa mtulie kwanza uchumi utengenezwe.! Kiburi cha chadema ndo matokeo ya yote haya
 
hakuna mtu aliyekamatwa kwa kudai katiba mpya mnakosea sana kuhusisha mtu anayeleta fujo akakamatwa na mtu kukamtwa kwa kudai katiba ni vitu viwili tofauti mtu akidai kwa utulivu hakuna atakayemkamata
 
Hivi polisi hawa ambao ama kwa makusudi au hawaelewi kitu, kudai katiba mpya kuna kosa gani kisheria?

Hivi unapomkamata mtu ambaye anadai kitu ambacho kimeruhusiwa kisheria utakua unaelewa nini?...
Hata kufanya mkutano wa hadhara wa kisiasa hakuna kosa kisheria, lakini haifanyiki
 
Hivi polisi hawa ambao ama kwa makusudi au hawaelewi kitu, kudai katiba mpya kuna kosa gani kisheria?

Hivi unapomkamata mtu ambaye anadai kitu ambacho kimeruhusiwa kisheria utakua unaelewa nini?....
wanaogopa CCM itatoka madarakani
 
C mmeshaambiwa mtulie kwanza uchumi utengenezwe.! Kiburi cha chadema ndo matokeo ya yote haya
Magufuli alisemaje kuhusu katiba? Ulishawahi kuona ansigusia tangu alipoingia madarakani pamoja na kwamba aliahidi kumalizia mchakato? Maneno ya Mama yana tofauti gani na ya Magufuli?

Nikuambie ndugu yangu hakuna katiba iliwahi kupatikana kirahisi hivyo.
 
hakuna mtu aliyekamatwa kwa kudai katiba mpya mnakosea sana kuhusisha mtu anayeleta fujo akakamatwa na mtu kukamtwa kwa kudai katiba ni vitu viwili tofauti mtu akidai kwa utulivu hakuna atakayemkamata
hakuna mtu aliyekamatwa kwa kudai katiba mpya mnakosea sana kuhusisha mtu anayeleta fujo akakamatwa na mtu kukamtwa kwa kudai katiba ni vitu viwili tofauti mtu akidai kwa utulivu hakuna atakayemkamata
Wewe haupo nchi hii, kuvaa tu T-shirt iliyoandikwa tu katiba mpya ni kosa.
 
siyo kweli mkuu hebu tuweni waungwana tusikuze mambo kwa kiasi hicho hatujafikia hapo angalia ya uganda na nchi zingine utajiona sisi bado sana hatujafikia ukatili huo
 
hakuna mtu aliyekamatwa kwa kudai katiba mpya mnakosea sana kuhusisha mtu anayeleta fujo akakamatwa na mtu kukamtwa kwa kudai katiba ni vitu viwili tofauti mtu akidai kwa utulivu hakuna atakayemkamata
Kudai kwa utulivu unatakiwa udaije?
 
Hivi polisi hawa ambao ama kwa makusudi au hawaelewi kitu, kudai katiba mpya kuna kosa gani kisheria?

Hivi unapomkamata mtu ambaye anadai kitu ambacho kimeruhusiwa kisheria utakua unaelewa nini?...
Mkuu,
1. Kosa la kwanza ni kueneza corona.

2. Kosa la pili, katiba mpya inapoteza muda wa kuinua uchumi.

3. Kosa la tatu mchakato huo ni ugaidi.
 
Jeshi letu ninaamini linafanya kazi kwa 'pressure' kubwa kutoka kwa watawala.Hufanya kazi kwa 'maagizo' kutoka kwa wakubwa hata kama ni ya hovyo na hayana mantiki. Unaweza kukuta pia maagizo hayo hutoka kwa 'parallel government' ambayo ina nguvu kubwa kuliko Serikali halali iliyopo madarakani.
 
Hawa polisi ni vijakazi na watumwa tuu.. Wanatekeleza maagizo toka juu.. Na huko juu kuna nguvu nje ya mfumo ambayo haitaki kabisa kusikia habarj za katiba mpya...
Sahihi kabisa.Utendaji wa hiyo nguvu nje ya mfumo ni mfano wa genge la Mafia au Yakuza kule Japan.
 
Back
Top Bottom