Kudai Katiba Mpya kuna kosa gani kisheria?

Kudai Katiba Mpya kuna kosa gani kisheria?

Kudai Katiba mpya ni sawa na kutaka kuitenganisha CCM na dola..hili halitakubalika hata kidogo.
 
Hivi polisi hawa ambao ama kwa makusudi au hawaelewi kitu, kudai katiba mpya kuna kosa gani kisheria?

Hivi unapomkamata mtu ambaye anadai kitu ambacho kimeruhusiwa kisheria utakua unaelewa nini?

Au ukampiga mtu na kumuua au kumuumiza sababu tu amedai katiba mpya ambayo ni haki, ukifunguliwa kesi mahakamani utaponea wapi?

Unachochea na kiongozi wa kisiasa ambaye yeye maisha yake ya kisasa ni mafupi kuliko nafasi yako wewe kwenye utumishi

Polisi hawana tofauti na wauwaji hawa:

Singida: Walimu mbaroni kwa kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 5

Bila kukomaa nao, haisaidii.
 
Nyamaza ndugu yangu, utaitwa gaidi sasa hivi kwa kutaja tu neno 'katiba'
Ukipeleka kesi mahakamani kuhoji 'TOZO' nayo unaambiwa kuwa wewe sio raia!
KWA KWELI waTz tumewachoka madhalimu wa chama kikongwe kinachojiona kuwa kina hatimiliki ya nchi na taifa lililo letu sote.
Hata hao wanaonekana kuunga mkono udhalimu wao, wengi wao wanaongozwa na hofu inayotokana uoga, ujinga, njaa na pia unafiki uliyokolea.
Fidel Castro, aliyeongoza mapinduzi ya Cuba, alikuwa mtoto wa mmoja wa matajiri wakubwa. Baba yake alikuwa kabaila mwenye umiliki wa mashamba na ardhi eneo kubwa.
Fidel angeweza kuwa mnafiki na kuungana na uongozi dhalimu wa kifalme kufaidi matunda ya udikteta na unyonyaji, lakini yeye na mdogo wake wa kiume, hawakuendekeza roho ya njaa wala tamaa kama Dadaye, kwani alijaaliwa kuwa mpenda haki JASIRI.
Sasa safari YETU ndio imeanza, TUTAFIKA tu kwenye katiba mpya ya wananchi. VIKWAZO vilivyopo ni sehemu tu ya majaribu, hatutachoka.
AMEN
 
Back
Top Bottom