Kudai Katiba Mpya kuna kosa gani kisheria?

Kudai Katiba mpya ni sawa na kutaka kuitenganisha CCM na dola..hili halitakubalika hata kidogo.
 

Polisi hawana tofauti na wauwaji hawa:

Singida: Walimu mbaroni kwa kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 5

Bila kukomaa nao, haisaidii.
 
Nyamaza ndugu yangu, utaitwa gaidi sasa hivi kwa kutaja tu neno 'katiba'
Ukipeleka kesi mahakamani kuhoji 'TOZO' nayo unaambiwa kuwa wewe sio raia!
KWA KWELI waTz tumewachoka madhalimu wa chama kikongwe kinachojiona kuwa kina hatimiliki ya nchi na taifa lililo letu sote.
Hata hao wanaonekana kuunga mkono udhalimu wao, wengi wao wanaongozwa na hofu inayotokana uoga, ujinga, njaa na pia unafiki uliyokolea.
Fidel Castro, aliyeongoza mapinduzi ya Cuba, alikuwa mtoto wa mmoja wa matajiri wakubwa. Baba yake alikuwa kabaila mwenye umiliki wa mashamba na ardhi eneo kubwa.
Fidel angeweza kuwa mnafiki na kuungana na uongozi dhalimu wa kifalme kufaidi matunda ya udikteta na unyonyaji, lakini yeye na mdogo wake wa kiume, hawakuendekeza roho ya njaa wala tamaa kama Dadaye, kwani alijaaliwa kuwa mpenda haki JASIRI.
Sasa safari YETU ndio imeanza, TUTAFIKA tu kwenye katiba mpya ya wananchi. VIKWAZO vilivyopo ni sehemu tu ya majaribu, hatutachoka.
AMEN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…