Kudai Tanzania na China zilikuwa sawa miaka ya 60 Kiuchumi ni kujidanganya

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Wengi wamekuwa wakitoa hadithi kuwa Tanzania na China miaka ya 60 zilikuwa sawa kiuchumi. Kwangu mimi sikubaliani na hilo hata kidogo kwani masikini mwenye kopo akiomba na masikini mwenye mipango inayosubiri kutekelezwa, kamwe hawa hawawezi kuwekwa kundi moja.

Sisi uchumi wetu umekuwa wa kutojali Rasilimali zetu tulizonazo, bali tunategemea zaidi kushika makopo na kuomba misaada huku Uchina wao uchumi wao unategemea mipango yao na utekelezaji wake.

Hivyo miaka ya sitini yawezekana tulionekana kuwa sawa kwa macho lakini Uchina ilikuwa na mipango na sisi hatuna, hivyo walikuwa matajiri wakubwa zaidi yetu.

Kumbuka utajiri hauanzii kwenye tangible things bali kuwa na mipango mizuri.
 
Hiyo clarification yako kua utajiri ni ni pamoja na mipango ya baadae Umeipata wapi? Na pengine iko supported na mfano upi labda?

Mfano, kijana yuko chuo anasomea kozi Fulani yenye mshahara mkubwa kama akimaliza tuseme miaka miwili kutoka sasa. Ingawa yuko Chuo anasoma kwa shida lakini mipango yake ni kuja kuajiriwa kwenye hiyo fani na anafanya vizuri kimasomo.

Je kijana huyu utamuita tayari ni tajiri sawasawa na yule ambae tayari ameshaajiriwa na anafaidi matunda ya ajira yake kwa kua na kipato kizuri na maisha mazuri?
 

kwa maelezo ya mtoa ukifikiria tu au ukiwa na mipango ya kuwa Tajiri wewe tayari ni Tajiri,nafikiri mtoa mada anatoka Arusha mkoa wenye mabilionea wengi.

Kwa mtindo huu wengi matajiri
 
Nafikiri mleta mada ana hoja hapa. Nilienda Japani ambapo baadhi ya watu wanadai eti ilikuwa sawa na TZ miaka ya 70, katika makumbusho yao walionyesha kuwa walikuwa tayari na Manoari za kivita miaka ya 1940's wakizitumia kuvamia China na Mongalia. Pia walisherehekea miaka 200 tangu wajenge reli ya kwanza hiyo ni mwaka ya 2005. Treini ya mafuta kama tunazotumia sisi hivi sasa iliendeshwa kwenye Reli kuazimisha sikukuu hiyo na kwa mara ya kwanza niliona wajapani wakiacha kazi zao kushangaa treini hiyo iliyokuwa ina engine inayotoa moshi, kama mimi nilivyoshangaa siku ya kwanza nilipopanda Treini yao ambayo ndani ni kama ndege ama zaidi ya ndege.

Hivyo baadhi ya hadithi za wanasiasa si za kweli, cha muhimu tuangalie wenzetu walifanyaje? na sisi tufanye huku tukitumia strategy ya "Frog leaping" yaani kuacha baadhi ya hatua walizopitia kwa kadri tutakavyoona inafaa.
 

Mfano wa Japan ya miaka ya 1970s hapa hauingii kwa sababu soon Vita ya Dunia ilipoisha na Japan kupata hasara kubwa ikiwemo ile issue ya miji ya Hiroshima na Nagasaki, Japan iliamua kujikita na Kujiimarisha kwenye Sekta ya Viwanda ili ku-recover economical damages iliyopata, hivyo ilishaendelea zamani hata kabla hatujapata Uhuru.
 
Reli ya tazara wamejenga wachina ilikuwa ni miaka mingapi toka tupate uhuru? hivi beijing ya 1961 na dar ya 2000 unaweza ringanisha kweli! watu wanatakiwa wawasome wanasia na kubaki na kamsemo ka jk, mbayuwayu
 
Mleta hoja hauko sahihi, Rudi upya kusoma historia ya china economic revolution. Hiyo mipango unayoizungumzia haipo.

Chairman Mao alipoingiza Cultural revolution ikapelekea vifo zaidi ya wachina million arobaini. Kwa sera hiyo huwezi kuendelea au kuwa na wazo zaidi ya serikali.

Maendeleo china yamekuja baada ya mtu anaitwa Deng Xiaping, baada ya mao kufa. Pamoja na kuteseka hdi kufungwa jera lkn alipokuja kubadli sera maono na mipango alipoongoza china.kabla ya hapo china iliendelea kukumbatia sera za kipuuzi. Watu wakaanza kumiliki viwanda,watu wakaanza kutoka,vipaji vikakuzwa. Boom ya majengo china. İnasemekana gwanzuu ilizidiwa hata na dsm miaka ya sabini lkn baada ya economic revolution miaka ya tisini na themanini mwishoni leo ni jiji la kutisha.

Hatuna excuse ya umasikini wetu. Soma history mkuu. We need critical juncture. Revolution ya kiuchumi ilitokea ndani ya chama tawala rafiki zake na CCM. Hii inawezekana hata kwetu.

Mimi naamini mtu mmoja hapa nchini anaweza kubadili kabisa muelekeo wa safari ya hii meli inayoelekea kusikojulikana. İnaweza kuwa wew au mimi.
 
Nadhani haukumuelewa vizuri kwa mfano wako huo wa mtoto aliye shuleni, maana yake ni kwamba wakati huo uchina ilikuwa tayari na mipango ya maendeleo ya uchina tofauti na Tanzania mfano halisi ni pale Tanzania ilipo omba kupewa msaada wa kujengewa reli na wachina kwa mantiki hiyo uchina tayari walikuwa wameimalika kimipango na kimikakati
 

Hii story ya Japan bila shaka ni ya kutoka vijiwe vya kahawa. Unajua kuwa Japan ni moja ya mataifa yaliyopigana kikamilifu vita ya pili ya dunia 1939 hadi 1945? ilikuwa ikipambana na mataifa makubwa kabla haijamalizwa na mabomu ya atomiki ya Hiroshima na nagasaki. Kwa hiyo unaweza kupata picha Japan ilikuwa wapi kiuchumi miaka ya 1940 sahau kuhusu 1970
 

Mimi nafikiri hukusoma nilichokiandika bali umekurupuka kuchangia ama umekunywa kiroba, kwani mimi napinga hoja kuwa Japani ilikuwa sawa na TZ miaka ya sabini kwa kutoa mifano kitu ambacho unaungana nacho lakini unasema ni story ya kwenye kahawa! hiyo +/- 1940 (1940's) nimeiandika kuwa tayari walikuwa na manoari za kivita inayoonyesha kuwa walikuwa na uchumi mkubwa wakati huo lakini labda wewe hukuiona hiyo hoja unakuja kuirudia hapa
 
Kuna umasikini unatokana na kudumaa kwa uchumi. Na umasikini unaotokana na sababu ya nchi au jamii kutokuwa na maendeleo.

Uchumi wa China ulidumaa kwa sababu ya vita vya ndani na siasa mbovu. Lakini nchi ilikuwa tayari na chachu zote za maendeleo.

Tanzania ni nchi isiyo na maendeleo.
 
Wenzetu miaka hiyo walikuwa wanajenga madaraja ya kuvuka bahari ya barabara na reli zenye urefu wa kilomita zaidi ya 30, yaani ni sawa na kutoka pemba hadi unguja, sisi huku kidaraja cha kigamboni kinatushinda cha mita 500
 

Acha kashfa ndugu. Yes narudia ni story ya vijiwe vya kahawa,post gani kuna mtu kaandika kuwa Tanzania ilikuwa sawa na Japan 70's? watu wanazungumzia China wewe unatoa mfano mfu wa Japan ndiyo maana nikakupa 'nyongeza' ya facts hizo ili siku nyingine hata usifikiri kutoa mifano irrelevant. Umenielewa mzee wa 'viroba'?
 
Hata mimi najua kuwa inayoongelewa ni China bali kwa kuwa sina data za kutosha za China miaka ya nyuma nikaona nitumie mfano ambao unaendana wa japani kwani nilijionea mwenyewe "facts" hizo ndiyo maana nikaandika kama nilivyoandika. Uwe unasoma vizuri kabla ya kudandia hoja.
 

Japan is irrelevant in this context whatsoever. Conversation closed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…