Nitarudi kujua kinachosemwa na Babu DC!
Babu DC bwana
Kuna ile danganya ambayo lazima udanganye kwa kuwa umeulizwa but kutokusema kila kitu inaweza kuwa rahisi klama hujaulizwa. But ukiulizwa ni lazima ujibu bana
Hahahahahahahahahahha,
Yaani una manaa hapa utamwaga tu data...
Mkuu wa kaya (MK): Soulmate ulikuwa unaongea na nani mbona simu ilikuwa busy muda mrefu?
MJ1: Ni yule ex BF wangu wa USA. Kanipigia
MK: Anasemaje?
MJ1: Eti amenimiss sana...halafu anasema kuwa duuuu enzi zile tulitesa sana. Amenikumbusha jinsi tulivyoenda kujirusha Zanzibar baada ya kupewa zawadi ya birthday yake!...Yaani nimefurahi sana kwa kuwa tulikuwa hatujaongea muda mrefu!!
MK: Ok, msalimie sana.
MJ1: Poa soulmate, amesema atapiga tena J2!
.....
Babu DC!!
Hahahahhaahaha Nanu DC kwanza I do not entatain Exes! Pili ikitokea amenipigia definitely mazungumzo hayatokuwa ya aina hiyo, ni short and clear then hata kabla hajauliza nitakuwa nshajishtaki mwenyewe (na nlivyo mmbeya dah! yaani mdomo utakuwa wancheza hata kabla simu haijakatwa aisee)
Uongo una gharama, kwa watu wenye RAM ndogo na ubongo wa Mb 3 haufai!
Unaona sasa unavyojiingiza mwenyewe?
Hebu muulize mzee mwenzangu Asprin akukatia wasia kidogo!!
Kuna wanaume ambao kitendo cha kujishitaki ni sawa na suicide bombing!
Hii michezo nyie ione hivi hivi....Hakuna refa wala mchezaji anayeweza kujidai kuwa ni star!!
Babu DC!!
Hahahaha Babu DC umesema kweli uzuri ni mwelewa so most of the time ...Umbeya... wangu huwa haucost sana haha (Sijui najifariji tu!!)
Bahati mbaya Soulmate, browser yake imecrash I just wish angekuja afunguke hapa lol!
Hii mbaya sana........ Ila ulivyoiongea ni lazima kuna kichomi cha kweli moyoni tena chanzo ki karibu.....:screwy: .....hivi, unapokuwa unamdanganya mtu, bila 'woga' kwamba ANAJUA unamdanganya, ...kusudio lako huwa nini?
.....mimi bado sina tafsiri sahihi juu ya hili zaidi ya 'madharau' katika mapenzi. Au wewe waonaje? Mbu is only thinking ALOUD ....:what:
Nipeni maoni yenu waungwana...
Mwenyewe anauliza uongo na kudanganya mapenzini hakuepukiki? .... na ni wakati gani haifai kudanganyana na kusema uwongo?
Sasa tujibu mara ngapi dada?
Uongo ni muhimu sana pale ambapo utakusaidia kuepusha shari, kuleta heri na kuongeza dakika za kuishi hapa kwa duniani kwenu nyote!!
Umeelewa mjukuu wangu?
Babu DC!!
.....enhe, swahiba Dark City....kwanza habari za huko?
Ehh, umegusia suala la kudanganya 'live' ili kuepusha shari....nawe umejikubalisha.
Je? Huna haja ya kuthibitisha ukweli uujuao na unaouamini kwa uongo unaoambiwa dhahiri? E bana ee....am lost hapo.
.....:screwy: .....hivi, unapokuwa unamdanganya mtu, bila 'woga' kwamba ANAJUA unamdanganya, ...kusudio lako huwa nini?
.....mimi bado sina tafsiri sahihi juu ya hili zaidi ya 'madharau' katika mapenzi. Au wewe waonaje? Mbu is only thinking ALOUD ....:what:
Nipeni maoni yenu waungwana...
Majuzi umeona mwenyewe soulmate 'kanifumania' live kitandani kwetu...
Mwenyewe nilimtarajia arudi jumatatu, kumbe semina ilikatwa ruzuku, j'2 alfajr huyo....hodi mpaka chumbani.
Nimemwomba msamaha na samahani zote, kwani ningejua atarudi mapema, nisingemleta yule binti (aliyening'ang'ania aje kuona tunapoishi).... utetezi wangu unauonaje hapo?