Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kudekezwa ni kusikilizwa zaidi, kupewa kila unachoomba hata kama sio cha msingi. Kutoambiwa lolote pindi unapokosea na huendana ukaribu sana baina ya mdekezaji na mdekezwaji.
Kudekezwa ni kusikilizwa zaidi, kupewa kila unachoomba hata kama sio cha msingi. Kutoambiwa lolote pindi unapokosea na huendana ukaribu sana baina ya mdekezaji na mdekezwaji.
cdhan kama tafsiri yako inaukweli ndani yake! Naona kuna haja ya kureview the standard swahili dictionary kwa ufafanuzi zaidi. Otherwise kudeka kuna raha hasa unapopata mtu wa kukudekeza!
kwa tafsiri yangu binafsi
1. kudeka ni tabia ya mtu kujilegeza, kujiona hawezi kufanya/kupambana na vitu vigumu wanavyofanya wengine,
mfano mwanamke mjamzito anapokuwa na mtu wa kuweza kufanya kila kitu kwa ajili yake basi anajiligeza na kudeka
2. kudekezwa. hali ya mtu kufanyiwa kila kitu na watu wengine yeye akiwa anaweza kufanya
mfano mtoto anayefuliwa kufuli zake na kumpikia ile hali ana umri wa miaka 20 hawezi hata kuosha chombo alicholia chakula ni kudekezwa
hata mwanaume anayefuliwa kufuli lake na mkewe pia anadekezwa
Je, mtu ambaye amekuwa akijitegemea mwenyewe tokea umri wa miaka 18. Anaishi mwenyewe tena mbali na wazazi wake, anajilipia bills zake mwenyewe. Ambaye kwa kiasi kikubwa (kuanzia mwaka wa pili chuoni na kuendelea) kajisomesha mwenyewe. Kila alicho nacho kajitafutia mwenyewe kwa juhudi, bidii na nidhamu zake mwenyewe. Ambaye wazazi wake wanampenda kwa dhati na bila masharti, na yeye anawapenda vivyo hivyo. Mtu huyo unaweza kusema anadeka/ kadekezwa?
cdhan kama tafsiri yako inaukweli ndani yake!
kudekezwa ni lazima uwe na mtu wa karibu kukudekeza. Anaweza kuwa mzazi au mpenzi. Ukaribu wa hapa sio lazima wa kuonana ana kwa ana. Unaweza kuwa mbali na ukadeka.
Unaweza kunipa mfano au mifano ya mtu anayejitegemea na ambaye anadeka?Watu wanaojitegemea haimaanishi hawawezi kudeka ingawa mara nyingi watu wanaodeka sana huwa ni wazito kuanzisha maisha yao ya kujitegemea halafu mara nyingi sio wepesi wa kufikiri na kufanya maamuzi.
Vizuri sana.
sijui nikudekeze ili uelewe vizuri! Lol.
hivi kudekezwa/kudeka ina maanisha ''spoiled''?
Anyways,kudekezwa nadhani kuna maana mbili tofauti:
1 Maana nzuri (positive)-kusikilizwa,kupewa raha,kupewa priority etc. some kind gestures and whatever else.kwa ujumla ni kuoneshwa upendo wa hali ya juu kidogo
2 Maana mbaya (negative)-kutokuwajibishwa.mambo ya kujifunza majukumu ya kijamii na kujitegemea ni ya muhimu,kuakosa ni kudekezwa kubaya.mume anaweza kufuliwa kufuli na mkewe (hata mume kumfulia mkewe,raha ya kudeka ni kudekezana banaa:welcome🙂.kudekezwa kubaya ni sawa na kuharibiwa,manake mwisho unakuwa hujitambui kuwa jamii inategemea nini kutoka kwako katika nafasi tofauti.ndo unakuta jitu haliwezi hata kushukuru au kusalimia!
hivi kudekezwa/kudeka ina maanisha ''spoiled''?
Mtu anayedeka ama kudekezwa anaweza kujitegemea? Au hawezi na kila apatapo kashida hata kawe kadogo namna gani atakimbilia kwa baba na mama au yeyote yule anayemdekeza?