Mwana wa Nuru
JF-Expert Member
- Dec 3, 2012
- 589
- 412
Wapo wenzetu ambao kila wakisikia madai ya katiba mpya, wanadhani tunataka kùgombea na kuchaguliwa au kuchagua tu. Hawaachi kusema tuna uchu wa madaraka ilhali wao ndo ving'ang'anizi wakubwa, ruba na kupe wa madaraka.
Yawapasa wajue kuwa katiba, mbali na masuala ya uchaguzi, inahusu haki na wajibu wa kila raia, watawala na watawaliwa; mamlaka na wajibu wa serikali, bunge na mahakama kama nguzo kuu za dola na uendeshaji wa taasisi anuai za nchi.
Kwa mfano, suala la mtu kuwa na mamlaka ya kumsweka ndani mwingine bila sababu ni ukiukwaji wa haki zetu raia na tumeshaona watu jana Sabaya wa Hai ambaye alitumia nafasi yake kupora watu mali zao na kufanya ujambazi na mauaji.
TUNATAKA KATIBA MPYA!