Kudharau P&L: Hii ndio sababu ya biashara nyingi kufa

Kudharau P&L: Hii ndio sababu ya biashara nyingi kufa

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Katika andiko hili napenda kuzungumzia kuhusu kitu kinaitwa Profil and Loss statement (P&L) kwa wahasibu.

Kwa wenye ujunzi kidogo wa Uhasibu wanaelewa maana ya P&L na umuhimu wake katika biashara.

Kwa ufupi P&L ni taarifa ya fedha ya biashara katika kipindi fulani kwa kuchanganua Mapato na Matumizi ya Biashara ili kupata Kiasi cha faida iliyopatika.

Taarifa hii ni muhimu sana katika biashara na inaweza kokotelewa kwa siku, wiki, mwezi na hata mwaka kulingana na aina ya biashara, kiwango cha mzunguko wa Fedha na mfumo wa usimamizi na uendeshaji.

Tofauti na kuwa na asset/Mali nyingi katika biashara, P&L inakuonesha kwa hakika kabisa iwapo biashara yako inaenda vizuri au la.

Ili nielewe vizuri nitoe mfano rahisi wa mtu ambaye anamilik duka la reja reja ambaye analipa kodi ya TZS 50,000 kwa mwezi na ana mtaji wa TZS 500,000 na ana mauzi ya TZS 400,000 kwa mwezi na faida yake kwa bidha ni 20% katika hali kawaida unaweza ukafikiri biashara ya huyu bwana ama iko vibaya au iko vizuri kutegemea na jinsi utaiangalia.

Ukiiangalia katika ukwasi inaweza kuwa vizuri ila katika mfumo wa faida na hasara (Profit and Loss ni biashara kichaa) kwa nini?

Kwa sababu kwa mauzo yake ya TZS laki 4 faida yake ni 80,000 na akitoa kodi ya TZS 50,000 anabaki na elfu 30 ambayo haiwezi kumlipa mfanyakazi, kununua umeme na gharama zingine.

So ili aweze kupata faida ya TZS 300,000 kwa mwezi lazima awe na mauzo yasiopungua TZS 1,500,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na TZS 50,000 kwa siku. Ili aweze kuuza mauzo hayo kwa siku lazima awe na angalau mtaji wa TZS milioni 6.

Kwa ni akiwa na Mtaji chini ya hapo inamaana hatakuwa na inventory ya kutosha na hio inaweza kuathiri huduma kwa wateja wake na kuvuruga biashara yake.

Kwa kuandika hivi simaanishi kwamba biashara ya duka haina faida na watu wasifanye hapana, na wala simaanishi kwamba lazima mtu awekeze TZS milioni 6 ili atengeneza faida ya laki 3 kwa mwezi hapana.

Ninataka kuonyesha umuhimu P&L na inavyoweza kukupa picha ya Muelekeo wa Biashara yako.

Kama nilivosema P&L inaonesha Mapato - Matumizi = Faida/Hasara kutegemea iwapo mapato ni makubwa au ni madogo.

P&L ni kama alarm katika bishara yako ambayo inaweza kukwambia ubane matumizi, uongeze uwekezaji, ufunge biashara n.k.

Bila kuwa na P&L unaweza kujikuta unapoteza muda ktika biashara na huoni unachopata.

Ili kuwa na P&L unaweza kutumia mfumo wa kukotoa wakati wa manunuzi ili kufahamu faida tarajali/Expected margin.

Kwa kufanya hivo unakuwa unajua kabisa kwamba kila nikiuza 10,000,2000 ni faida 8000 ni mtaji so ukitaka kufanya manunuzi unatumia mpaka 8000 na ukitaka kufanya matumizi mengine unatumia mpaka 2000 na ukitaka kukuza mtaji unaweza ku reinvest ile 2000 yako.

Jambo la muhimu ni kujua kwamba faida ipo na imetumika badala ya kuhis tu kwamba ipo mpaka siku unajikuta huna mzigo wala hela unaanza kutafuta mchawi.

Ukiwa na P&L utajua kama unapata HASARA, UNAIBIWA, UNA MATUMIZI MABAYA N.K.

Jambo la muhimu ni wewe kujua kwa hakika kabisa iwapo biashara yako ipo au unapoteza muda

Kufanya biashara bila kuwa na P&L ni kupoteza muda.

Biashara nyingi zinakufa kwa sababu wamiliki hawatazami eneo hili kwa umakini na matokeo yake wanapoteza mitaji yao yote kwa sababu ya kukosa maarifa

Iwapo unahitaji mfumo rahisi na nafuu wa kutunza kumbukumbu za biashara yako pamoja na kukupatia hesabu na taarifa muhimu kama P&L na Balance Sheet pamoja na uwezo wa kuetengeneza invoices na receipt nzuri basi wasiliana nasi kwa msaada.

Iwapo unahitaji huduma za Bookeeping-utunzaji wa kumbukumbu kwa maduka ya reja reja, jumla, hardware, maduka ya dawa, maduka ya spare za magari, maduka ya spare za pikipiki, hotel, bar Migahawa nk kwa gharama nafuu pia unaweza kuwasiliana nasi.

Huduma zetu zinapatikana kwa njia ya mtandao na tunaweza kukutembelea na kufundisha wafanyakazi wako kutumia mifumo ya kihasibu.

NB: Hatutoi huduma za Kihasibu ila tunaweza kukuunganisha na wataalamu iwapo unahitaji huduma hizo.

Karibu tuwasiliane kwa email:masokotz@yahoo.com
 
Back
Top Bottom