Hapa mtoa mada hujaelewa. Ni kweli zipo Phd za darasani na hizi ndio zinatambuliwa mradi zimetolewa na chuo kikuu kinachotambuliwa. Hizi ndio unaambiwa wahitimu wake ndio wanaweza kujiita Dr fulani bin fulani.
Taratibu za Phd za heshima 'causa honaria' huwezi kujiita Dr fulani bin fulani. Ila ukiandika jina lako ukipenda inakua hivi kwa mfano, Mr Fulani bin Pacheco PhD hons.
Kwa kawaida PhD za heshima kama zilivyo za kuandika thesis hutolewa na vyuo vikuu.
Sasa shida iko hapa, kuna matapeli wanaanzisha vyuo feki au mamlaka fulani huko ng'ambo wanajiandikisha kama chuo kwenye mitandao. Ukitafuta ithibati ya chuo utakuta ni utapeli. Hawa wanakuambia wanakupa PhD ya heshima. Watakufuata wenyewe kukuvisha joho na kukupa hiyo tuzo. Wataandaa shughuli kwenye hoteli au mahali popote wanaona panafaa. Cha msingi unalipia hela. Inaweza kua usd 2000 hadi 3000 hivi. Wakitangaza hiyo biashara watakueleza upeleke wasifu wako. Ndio utakuta kina taletale hamisi eti wamepromote muziki tanzania. Elimu yenyewe darasa la saba. Wengine wanaweza kua kina mzee mrema RIP, wabunge abood, msukuma etc etc.
Halafu kuna PhD wanapeana viongozi wa dini ya kikristo. Kila madhehebu ina vyuo vyake. Hawa nao kwa taratibu zao wanatumia tittle ya Dr lakini vyuo vyao na mfumo wa vyuo vikuu vya masomo ya kawaida vinatofautiana. Unaweza kumsikia mchungaji Dr so and so akizungumza hoja fulani kama wewe ni msomi unaweza kushangaa kama kweli huyu ni PhD holder.