SoC02 Kudhibiti usugu wa dawa za kutibu magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na kuvu (Fangasi) Tanzania

SoC02 Kudhibiti usugu wa dawa za kutibu magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na kuvu (Fangasi) Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

vigilance

Member
Joined
Dec 15, 2016
Posts
5
Reaction score
4
KUDHIBITI USUGU WA DAWA ZA KUTIBU MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA BAKTERIA NA KUVU (FANGASI) TANZANIA.

Usugu(Upinzani) wa dawa ni hali ambayo vijidudu kama bakteria na fangasi kuzishinda dawa ambazo zimeundwa kuziharibu na hilo husababisha mtu kushindwa kupona ugonjwa fulani unaosababishwa na bacteria au fangasi, Usugu wa dawa hutokea kiasili lakini matumizi mabaya ya dawa yanachochea kuongezeka kwa usugu wa dawa.

Bakteria ni viumbe hai ambavyo hatuwezi kuviona kwa macho ya kawaida bali kwa kutumia kifaa maalumu cha maabara kinachoitwa hadubini.

Fangasi ni viumbe vya yukariyoti ambavyo huweza kusababisha magonjwa katika mwili wa binadamu.

Antibiotiki ni dawa ambazo zimetengenezwa kuua au kuzuia ukuaji wa bakteria.

Viuavijasumu ni dawa zinazoua au kusimamisha ukuaji wa fangasi wanaosababisha magonjwa.

Upinzani katika fangasi dhidi ya dawa za kutibu fangasi unaweza kujitokeza ikiwa mtu atatumia dawa hizo vibaya, kwa mfano mgonjwa akihisi ana dalili za ugonjwa wa fangasi iliyojirudia(huenda aliwahi pata hizo dalili kipindi kilichopita na alienda hospitali akapewa dawa fulani), sasa kutokana na zile dalili kujirudia akaamua asiende hospitali akaenda kununua dawa bila kupata ushauri wa daktari, anaweza akapewa dozi ambayo ni ndogo ukilinganisha na tatizo alilonalo hivyo hiyo dozi ndogo inafubaza fangasi kwa mda mfupi lakini baada ya mda wataibuka na kusababisha ugonjwa kua mkubwa zaidi kwa kua dozi ilikua ndogo hivyo wale fangasi walishindwa kufa na kwa kua waliizoea hiyo dawa wakatengeneza njia nzuri ya kuipinga isiwadhuru, ugonjwa ukirudi tena itakua vigumu kutibu kwa kutumia hiyo dawa hata ikitumika kwa dozi iliyo sahihi.

Pia upinzani katika bakteria unaweza kutokea wakati mgonjwa anapotumia antibiotiki za wigo mpana (dawa ambazo hutumika kutibu mgonjwa anayeshukiwa kua na maambukizi ya bakteria lakini kundi la bakteria halijulikani au anaposhukiwa kuambukizwa na vikundi vingi vya bakteria), antibiotiki za wigo mpana zina nguvu kubwa katika matibabu lakini zinaweza kuharibu bakteria wazuri ambao tunaishi nao katika miili yetu ambao wana faida kubwa katika mwili wetu ikiwewo kupambana dhidi ya bakteria hatari, hivyo bakteria hatari watakua na nafasi ya kua na upinzani mkubwa dhidi ya antibiotiki.

Pia upungufu wa bacteria wazuri hutengeneza mazingira mazuri kwa ukuaji wa fangasi aina ya Candida ambae husababisha maambukizi ya candida.

ATHARI ZA USUGU WA DAWA
Upinzani wa vijidudu dhidi ya dawa husababisha mgonjwa kukaa kwa muda mrefu hospitalini kwa sababu mgonjwa hulazwa ili apate uangalizi maalumu ili aweze kutibiwa vizuri lakini kukaa mda mrefu huongeza gharama za matibabu na kibaya zaidi huongeza kiwango cha vifo.

NJIA ZA KUZUIA USUGU WA DAWA.
Kuongezeka kwa ukinzani wa dawa huchangiwa na matumizi mabaya ya dawa na udhibiti mdogo wa maambukizi.

Ili kuzuia na kudhibiti upinzani wa dawa tunapaswa kufanya yafuatayo;
  • Tukiumwa twende tukapime tujue tatizo ni nini, tuepuke kununua dawa bila kufanya vipimo hilo litasaidia sisi tuweze kutumia dawa iliyo sahihi na kuepuka ugonjwa kujirudia baada ya kumaliza dawa tulizoandikiwa.
  • Tuepuke kutumia dawa alizoziacha mtu ,kuna tabia ya wagonjwa wengine akijihisi amepata nafuu anaacha kumeza dawa na hivyo kubakiza dawa ndani hilo linafanya yeye asitibu vizuri ugonjwa wake na pia hushawishi mtu mwingine akiumwa kutumia zile dawa alizobakiza nahilo huchangia pia usugu wa dawa kwa kua kwanza atakua anatibu kitu asichokijua na pili atatumia dozi isiyo kamilli
  • Daima tufuate ushauri wa wahudumu wa afya tunapotumia dawa, ushauri huo utatusaidia kutumia dozi sahihi na kwa mda sahihi na hilo litapunguza maambukizi yanayojirudia
  • Tuzuie maambukizi kwa kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji safi kabla na baada ya kula, baada ya kutoka chooni , baada ya kumbadilisha mtoto aliyejisaidia na kabla ya kuandaa chakula. Kunawa vizuri mikono ni njia nzuri ya kuzuia magonjwa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa sababu tunaponawa vizuri tunapunguza uwezekano wa kusambaza vijidudu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine na hivyo kuepusha kupata magonjwa.
  • Tujitahidi pia kunywa maji safi na salama yaliyochemshwa na kuchujwa au yaliyowekwa dawa za kuua vijidudu vinavyoweza kuwepo katika maji ya kunywa hilo litasaidia kuepuka kupata magonjwa yanayoambukiwa kwa njia ya maji.

MAONI KWA WATAALAMU WA AFYA NA SERIKALI KWA UJUMWA
Usugu wa dawa ni janga la dunia nzima si Tanzania pekee na serikali yetu na wataalamu wetu wa afya wanajitahidi kutoa elimu nzuri kwa wananchi juu ya janga hili ambalo linazidi kuongezeka na lisipozingatiwa linaweza kusababisha kua kubwa zaidi na kusababisha madhara makubwa baadae.

Maoni yangu kuhusu hili ninaomba wataalamu wa afya na serikali kwa ujumla kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa wananchi kwa kua watu wengi hawalijui janga hili kubwa la usugu wa dawa .

Elimu itolewe sehemu za mjini ambako kuna urahisi wa mtu kujinunulia dawa katika duka la dawa lolote, hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wajue athari za kutumia dawa bila kupata ushauri wa mtaalamu wa afya, lakini pia vijijini elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa na hasa jinsi ya kujikinga na magonjwa kwa kutumia njia mbalimbali zilizoorodheshwa hapo juu hasa kujitahidi kutumia maji safi na salama na matumizi mazuri ya vyoo ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza.

Pia napendekeza kuwe na siku maaalumu angalau kila baada miezi michache kuwe na uelimishaji kwa wananchi jinsi ya kutumia vizuri dawa za kutibu magonjwa mbalimbali au kuwe na machapisho ambayo yanaweza kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kwa mfano katika ofisi za vijiji mbalimbali tunakopata matangazo mbalimbali yakibandikwa pia makala fupi za kusisitiza matumizi sahihi ya dawa itakua rahisi zaidi kwa wananchi angalau kupata uelewa kuhusu kile kinachoendelea katika ulimwengu kuhusu hili janga la dunia nzima.

MWISHO KABISA NIPENDE KUSEMA KINGA NI BORA KULIKO TIBA..
 
Upvote 4
SOC2022..Karibuni kusoma chapisho langu tuweze kuelimika zaidi.
 
Back
Top Bottom