Kudhibiti wizi mabandani (kuku, ng'ombe, mbuzi nk)

Kudhibiti wizi mabandani (kuku, ng'ombe, mbuzi nk)

spray

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
277
Reaction score
241
Wiki hii kuna vibaka wameiba sana ng'ombe na mbuzi nahisi mambo ya sikukuu, hebu tushauriane ni njia zipi unaweza kutumia kudhibiti wizi mabandani, na kama una experience yoyote pls iweke tuelimike wote.

Last wk kuna mdau wa kilimo aliniacha hoi aliponiambia hapo kabla walimuibia sana mazao yake,alitumia kila mbinu aliyoweza hakufanikiwa, alichofanya ni kuweka pembe za ng'ombe kuzunguka shamba lake la hekari kumi akazivalisha kitambaa chekundu, hapa ni mwaka wa pili sasa vibaka hawajakanyaga tena shambani kwake hahahah..., watu wana vijimbinu sana...

Nawasilisha
 
Wezi wanarudisha sana maendeleo nyuma, shambani kwangu waliniibia mikungu ya ndizi zaidi ya 30 nami ngoja nitumie hyo mbinu ya kuzungushia mapembe yawezekana ikanisaidia...
[emoji48] [emoji48] [emoji48] [emoji48] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi siibiwi hata siku moja.

Atakayeniibia kesho yake atarudisha alichokiiba muda ule ule alioiba alichoiba, kisha nichague adhabu ya kumpatia.

Hakika.
 
Mbinu ya jamaa kuweka pembe imenikumbusha tukio moja.
Mwezi wa sita 2017 nikiwa na dingi mdogo yeye ndo alikwa anaendesha gari tulikamatwa na trafiki Gongo la Mboto mwisho, gari ilikuwa na makosa kibao tukapaki pembeni kabisa kwenye vumbi. Trafiki akamuandikia dingi, basi wakati anaondoka dingi akazoa mchanga pale aliposimama trafiki na kuuweka mfukoni. Da! Trafiki akarudi fasta akamuomba dingi wazungumze yaishe akamrudishia fedha. Baadae namuuliza dingi ndo nini vile anasema ulikuwa mkwala tu.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom