Godwin umekosea sana na leo bahati nzuri nitakuelimisha vizuri!. Tatizo la Tanzania ni serikali.
Tanzania ingekua imeendelea sana kama serikali ingekuwa inatunga sheria tu hapa chini nitakupa kitu kimoja kimoja kwa undani
1. Viwanja: Nimeanza na viwanja kwasababu kwa uchumi kuendea unakiwa kuwa na "Land". Kwanza viwanja vya Tanzania si vya wananchi bali ni vya serikali! hivyo wananchi wa Tanzania wana pangisha viwanja vyao. Tatizo ni kwamba serikali si mtu hivyo kiongozi yeyote anaweza kuweka sheria zake na kubadilisha kwa manufaa yake binafsi wakati wowote. Pili vibadi vya viwanja vya Tanzania hata kama unahaki zote za kumiliki ni gharama na usumbufu wa hali ya juu kipewa kibali cha kiwanja kama unataka kujenga. Kuna wakati inachukua hadi miaka minne kupata kibadi nwakati una kila karatasi linalotakiwa. Ujenzi mfano ni muhimu sana kwa maendeleo kwani ukijenga unatumia mafuta, una nunua smenti, misumari, mbao, plastics, mabomba, wiya, unavuta umeme, makokoto, unaajiri wapimaji wa viwanja, unaajiri wajenzi, na mengineyo mengi. Hii yote inasadia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi lakini serikali inazungusha watanzania kucha kutwa kwenye vibali bila kuwa na sababu ya msingi. Pamoja na serikali kuzungusha watu Watanzania wamejitahidi kujenga bila msaada wowote wa serikali.
2. Umeme: Umeme ni mfano mwingine wa serikali kuwa na Tatizo. Serikali ingeachia kampuni binafsi zihusike kwenye umeme tatizo la umeme lisingekuwapo Tanzania. Ngoja ni kupe mfano wa state nyingine za hapa USA zinavyofanya. Step 1: Kunakuwa na kampuni kama ya Tanesco na inakuwa na lengo moja tu kusambaza umeme na kutengeneza. Step 2: Kampuni ya Tanesco inakuwa inanunua umeme kwa makubaliano fulani na kampuni ya tofauti zingine za majenereta, zingine za umeme wa jua, zingine za umeme wa upepo, gas n.k. mtu yeyote anayeweza kuuzia umeme Tanesco kwa kiwango fulani ambacho ni cha kimataifa aruhusiwe. Step 3: Tanesco inajitoa kwenye biashara ya wateja kama kutuma bill na kukusanya pesa na ziruhusiwe kampuni tofauti kufanya biashara hizo. Hii itapunguza mzigo mkubwa kwa Tanesco. Mfano mtu akiwa na bill naomba nitumie dollars ya $50 kwa mwezi basi ($20 ya Tanesco, $20 ya muuzaji wa umeme na $10 ya kampuni inayoshughulikia utumaji na upokeaji wa mapato kutoka kwa wateja). Ushindani huu utapunguza gharama na kuongeza umeme Tanzania. Tanzania inakuwa imetatua tatizo lililopo sasa la kununua majenereta!. Hili ni tatizo la serikali, mikataba mibaya ni tatizo la serikali. Umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.
Mikopo: Je kwa nini Tanzania mikopo ya bank ni zaidi ya 10%? ni kwasababu ya vitu vifuatavyo (1) Hatuna ID hivyo watu wa bank hawajui watu (2) Viwanja ni vya serikali hivyo huwezi kuweka rehani kwa muda mrefu kwani serikali wakati wowote inaweza kuchukua kiwanja cha mtu yeyote (3) Serikali-Serikali ili kukithi mahitaji inauza T-BILLS na Goverment Bonds. Serikali ya Tanzania rate inayotoa kwa hizi ni zaidi ya 7% na kawaida bank haziwezi kutoa mikopo kwa rate chini ya hapo kwani kama mwekezaji anaweza kuwekeza kwa serikali kwa 7% na ana uhakika wa kulipwa ni kwa nini anawekeze kwa mtu wa kawaida kwa kiwango hicho hicho wakati hana uhakika wa kulipwa!!! hivyo ukweli ni kwamba bank ni lazima zitoe kiwango cha juu zaidi. Hapa tena Tatizo ni serikali!
Miradi ya Uwekezaji: Uwekezaji wa Tanzania ni kichekesho serikali ikipata mwekezaji wa madini, mafuta, gas au hata mashamba wanawatoa watu kwenye maeneo ili kumpisha mwekezaji. Serikali bila kuhusisha wananchi inaingia mikataba ya siri eti kwa manufaa ya nchi. Wawekezaji wanawalipa wafanyakazi au wizara Dar. Watanzania ambao wamefukuzwa na kuchukuliwa viwanja hawapati chochote, jamii zao zinadidimia sana barabara hazijengwi, hakuna shule, hakuna maji n.k sana hapo serikali imewasadia vipi wananchi? Je si bora serikali ingewasaidia wananchi kuingia mkataba na hizo pesa zibaki pale.Sasa hapa tena serikali ni Tatizo ingetakiwa kuwasaidia watu badala ya kufanya mashamba ya watu kuwa mitaji ya mawaziri.
Kuna mifano mingi na sitanii nafikiria kuandika kitabu kwani nimeona watu wengi hawaelewi ubaya wa kuwa na serikali kubwa.