Kudondosha risiti ya huduma ya choo kumeniponza

Cendy

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
1,250
Reaction score
2,309
Wakuu habari za humu jukwaani
Leo wakati nikiwa safarini naenda maeneo Fulani huko tarime nilipita stand ya musoma niliingia chooni kutoka nikalipia nikapewa list ya sh mia tatu hatua mbili nikaindondosha ile list [emoji24] [emoji24] [emoji24] tatizo sio kudondosha list tatizo nikashikwa kwa kuchafua mazingira ya stand [emoji35] [emoji35] [emoji35] hawa wakurya jomoni kidogo waniue bure ilibidi niwabembeleze nikawapa 30000 kwa hiyo nimeenda chooni kwa 30300[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] wale wadai picha, picha hiyo hapo

the great
 
Ushaingizwa cha kike hapo mzazi.. Ila pole sana siku nyingine uwe makini
 
Hata ukija Manispaa ya Moshi uwe makini sana Cendy huku faini ni elfu 50!
Moshi hata ukitupa ganda la vocha, makohozi au uchafu mwingine hata kukojoa njiani unakamatwa!
Lakini naona kama Moshi inapoteza usafi wake wa zamani, sijui ni wageni wengi au wenyeji nao wameanza 'uswahili'. Moshi ya sasa si kama ya zamani kwa usafi
 
Lakini naona kama Moshi inapoteza usafi wake wa zamani, sijui ni wageni wengi au wenyeji nao wameanza 'uswahili'. Moshi ya sasa si kama ya zamani kwa usafi
Sheria imepungua makali kumbe! Labda inategemea na baraza la madiwani na mkurugenzi wao wanavyofuatilia usafi huo
 
Hata ukija Manispaa ya Moshi uwe makini sana Cendy huku faini ni elfu 50!
Moshi hata ukitupa ganda la vocha, makohozi au uchafu mwingine hata kukojoa njiani unakamatwa!
Wakuu niliona hii miatatu ya list isinipe shida daa kumbe naenda kwenye shida jomoni

the great
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…