Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Pasco, mimi naomba uniruhusu tu nikuoneshe (siyo kwamba nakutukana, hapana) jinsi mambo mengine unayoyasema siyo tu kwamba ni ridiculous lakini hata kwa akili ya kawaida they dont make sense at all. Unaanza hivi;
Mkuu Mbalinga, nakubaliana na wewe kuwa Chadema is doing a good thing and a right thing, kuleta matumaini mapya.
Uliposema hivyo nilikuwa nina matumaini kwamba unasema kweli lililo moyoni mwako na kama ni hivyo unapoongezea hili;
Watanzania wanahitaji kwanza kuona mbadala wa CCM, ndipo tuipe likizo CCM, tuwapeleke Chadema ikulu!.
Kwanza, hivi hao Watanzania unaowasema na wewe uko miongoni mwao ama ni swali la ninyi na sisi. Hilo ni moja lakini kubwa zaidi unadai unataka uone mbadala wa CCM kwanza, ndio uipe likizo CCM... sasa swali hilo litawezekanaje ndugu yangu? Unajua wazi kabisa kuwa Chadema haina dola, hawakusanyi kodi na sera inayotumika nchini ni ya CCM. Huo mbadala utauonaje? Kwenye kukosoa? Kwenye kupinga? Kwenye kulalamika? Kwenye kudai? Kwenye kuelimisha? Mbona hayo wanayafanya sana tu...hii labda ingewezekana kwa nchi za wenzetu kama Marekani ambako kuna Governors wa States ambao huchaguliwa na wananchi na si lazima watokane na chama tawala. Kwetu hapa hata huyo mbunge wa Chadema anaweza kutiwa ndani kwa amri ya kada wa CCM mkoa.
Hili la kusema tutafanya hiki, tutafanya kile, ndio CCM ways with lots of promises zilizoishia kuwa empty promises.
Hapa tena unajikanganya hata usieleweke, unapimaje uwezo wa timu ambayo hata kuingia uwanjani bado. Hiyo Chadema itategemewa kutekeleza aina gani ya ahadi huku sera zinazotekelezwa ni za chama tawala. Nilifikiri ungeweza kuipongeza Chadema kwa kuibana CCM hadi kuna wakati sera zake imebidi chama tawala iziige ingawaje hilo hawawezi kulikubali wazi wazi. Pasco ingekuwa kwamba huko nyuma Chadema waliwahi kukamata dola, hapa labda ungepata hadidu rejea lakini mmmh!
Chadema nao wakiahidi, elimu bure, afya bure, mfuko wa sementi elfu tani, tutaondoa umasikini, bila kusema how, unakuwa hujaonyesha mbadala wowote kwa CCM, nazo ni ahadi tuu kama CCM wanavyotuahidi kila baada ya miaka 5!.Pasco.
Ni kitu kimoja tu kilicho kweli hapa, nacho ni jinsi CCM wanavyotuahidi kila baada ya miaka 5 (kama walivyotoa ahadi karibu mia moja mwaka 2010) lakini utekelezaji ni sifuri. Sasa hapa lawama unazozitoa kwa Chadema ni zipi? Ni ahadi gani walitoa na kama walitoa na hawakupewa nafasi ya kutekeleza lawama zinatoka wapi? Kwa kweli hizi zako ni reasoning masikini ambazo zinaweza kutolewa tu na watu wasio na uelewa wowote serikali yetu inavyoendeshwa. Ombi langu kwako ni kwamba tujaribu kwa pamoja kuondokana na huu woga wa Tanzania bila CCM...hii tabia ndio inamsukuma mtu kama wewe Pasco kuwakumbatia watu kama EL eti mradi tu ni wana CCM, inasikitisha sana.
 
Pasco,hakuna watu unaweza kuwa pm walau waje kuokoa jahazi hapa?(wale wasiotoka nje ya mada)maana linazama mazima mkuu,sasa sijui utaanza na lipi,unahitaji msaada!ninaamini kuna watu mnashare hizi ideas,kwanini usiwe muungwana uwa pm waje hapa kuchangia ili mjadala uende vyema na chadema wapate ushauri?I'm just sayin...
 
Last edited by a moderator:

Mkuu, una hakika kuwa CHADEMA itarekebisha hayo yote uliyotaja au unapiga debe kwa sababu tu wewe ni mshabiki wa CHADEMA? Jamani SUMU HAIONJWI!
 
Mkuu, una hakika kuwa CHADEMA itarekebisha hayo yote uliyotaja au unapiga debe kwa sababu tu wewe ni mshabiki wa CHADEMA? Jamani SUMU HAIONJWI!

Mkuu hivi siyo "mama yoyo"?I stand to be corrected!

BTW una uhakika umeiquote post uliyokusudia?maana uliyoiquote haizungumzii marekebisho yoyote,bali "sababu za kuipigia chadema kura",tafadhali rudi nyuma ukaangalie kama uliquote bandiko ulilokusudia.Kama bado ndo hilo,basi hukumsoma uliyemquote na kumwelewa,either kwa makusudi,ama bahati mbaya,ama pengine kwa uelewa wako,umejibu kitu kingine kabisa kisichohusiana na bandiko lake.
 
Hivi chadema itashinda kwa kura za kina nani? wachagga? wako wangapi nchi hii?
"Ukiona chama kinazungumzia ukabila au udini ujue kimefilisika kisiasa, hakifai na kinakaribia kufa" - JK Nyerere
Zomba, mimi si mchaga wala Mkristo lakini navutiwa na sera za CHADEMA. Nimechunguza huounaoitwa uchagga na ukristo na nilipobaini ni taarabu tu za CCM nilichukua hatua. Tupo wengi tu; njoo huku Shinyanga, Mwanza, Mara, Mbeya, Songea, Iringa na sasa Mtwara; kote huko wanaishi wachagga? Zomba usitulazimishe kuamini wewe ni mpumbavu usiyefahamu ni nini kimewapeleka watu CHADEMA. Hata sisi tulikuwa CCM tena makada zaidi yako lakini, kutokana na madudu yaliyomo CCM mapenzi yale yalitutumbukia nyongo na ndiyo maana tumebadilika. Najua wewe kamwe hautabadilika kwa sababu ni mmoja wa wale waliosheheni huko na ambao CCM imewakumbatia..... Huwezi zisoma alama za nyakati kwa vile umefunikwa na blanketi zito la unono wa ufisadi wa CCM. Pole!
 

Kamanda yupi huyo? naomba jina lake.
 
JAmani sera ya chadema ni ya mlengo wa kati kwa maana ya ujamaa kiasi na kibepari kiasi inamaana chadema namna ya kukusanya kodi ya nchi watajikita kuwajibisha makampuni makubwa zaidi na namna ya struggle dhidi ya raslimali na utaifa itakuwa ni kwa nguvu ya ziada lakini katika kutumia raslimali chadema watakuwa kijamaa zaidi na ndio maana wanachukizwa na watu kukoswa madawa watu kukoswa makazi,elimu kuwa na matabaka na viwanda vya umma kuuliwa na PRIVATIZATION sasa inakuwaje mtu kila leo anasema chadema hawajaonesha wakiiingia madarakani watafanya nini!!
 

TEHE! TEHE! HII BAHARI UNAIJUA AU UNATAKA KUISUMBUA MAHAKAMA. Just to help you.


Actus Reus Non Facit Reum Nisi Mens Sit Rea: (Latin): conviction of a crime requires proof of a criminal act and intent. (Evidence is weighted not counted) N.B weighed is a primary school english(SHULE ZA KATA) in law.


AdProximum Antecedens Fiat Relatio Nisi Impediatur Sentintia(Latin): relative words must ordinarily be referred to the last antecedent, the last antecedent being the last word which can be made an antecedent so as to give a meaning.
 
Tujirekebishe kwa nini? Hizi ni thread za kijuha na kizuzu kweli.
Mkuu Shardcole, chakula umepikiwa, umepakuliwa, umewekewa mezani, umelishwa na kijiko mpaka mdomoni, kazi yako ni kutafuna tuu na kumeza, hutaki tema!. Unataka mpaka utafuniwe?!. Haya nimekutafunia kwa update 1st post, sasa its up tu you kumeza au kutema!.
"Majuha na mazuzu ni wale wasioweza hata kutafuna wenyewe, na hata wakitafuniwa, kumeza nako ni issue, wataishia kutema, au kutapika!.
 
Halafu kumbe unachaguwa za kujibu?acha hizo wewe.Rudi ujibu maswali.Kama huwezi sema tuendelee na mengine.
I'll leave no stone unturned!, utaratibu wa kuyajibu, niliuweka kule nyuma, na play both ways, "first come first served" na "last in first out"!, hivyo nitakufikia na nitakujibu!.
P.
 
Nimegundua humu jamvini chadema mipewa ushauri mnakuja juu, hata kama una manufaa na chama chenu kwanini? nashindwa kuelewa! ni mtu gani asotaka kushauri? hii ni ishara ya chama kibaya! hivi mtafika kweli?
Mkuu Mkonowatembo, umeona eh!?.
Halafu wasipofika hiyo mikele watakayopiga!, mara hawamtambua mshindi halali, mara wasuse na kutoka nje, lakini chai walikunywa tena with smilling faces!. Sasa ndio tunawaeleza rasmi hatutaki kuja kuliliwa kwa kushindwa kupokea ushauri!.
 
Mkuu Only83, mimi kazi yangu ni mwandishi wa kujitegemea na nimejibobesha kwenye siasa. Siitegemei CCM wala Chadema, au chama chochote kuendesha maisha yangu kiasi kwamba unadhania nasubiria shilingi itaangukia upende upi ndipo nichague!. Ila pia miiko ya taaluma yangu, inanitaka nisiegemee upande wowote na hivyo ndivyo nilivyo, siegemei upande wowote!. Ofisi za CCM Lumumba huwa nakwenda, pale Mtaa wa Ufipa yalipo makao makuu ya Chadema pia huwa nakwenda, na makao makuu ya CUF buguruni pia hufika na kote huko hufika kutekeleza majukumu yangu bila kuegemea chama chochote!.

Nilipoendesha kipindi cha "Kiti Moto" sikupendelea upande wowote, na soon nitapandisha program nyingine ambayo haitaegemea upande wowote!.

Naomba nikiri udhaifu wangu, ni kusema ukweli kupindukia na kusema ukweli huku, kumeisha nicost sana kwenye maisha yangu lakini ndio ukweli wenyewe!. Just imagine una mke wako wa ndoa, shetani anakupitia, unachepuka kidogo, mke anaambiwa, unakiri kuchepuka, anafungasha anaondoka ndoi imeishia hapo!, mnasuluhishwa anakaa kata kata kisa ulikiri, kwenye vikao vya usuluhishi wazee wanakushauri next time kanusha, hata kama ni kweli, kataa kata kata!. Mimi nilisimama na ukweli and paid the price!.

Hili la CCM kuchokwa ndio ukweli wenyewe!, na hili la Chadema haijajipanga, nalo ndio ukweli wenyewe na hili angalizo ninalowapa humu, kuwa Chadema isipobadilika, Ikulu mtaishia kuisikia tuu!. Huu ni ukweli mchungu ila ndio ukweli wenyewe!.

Mashabiki wa Chadema humu, wanajiaminisha kila unaye wakosoa lazima ni CCM, na hivyo ndivyo hata wewe unavyoamini!. Endeleeni kubeza huku siku zinasogea, by the time you realize the truth, it might be too late too little time to do things right!.
P.
 
Mkuu Mkandara, naamini ujumbe huu umewafikia!. Naamini kabisa 100% chini ya 100%, hakuna kiongozi makini wa Chadema, atayezipuuza hoja zako!, usibabaishwe wala kufadhaishwa na upinzani tunaupata humu jukwaani kwa ukosoaji wowote wa Chadema, wengi wa hawa wanaotupinga ni wapambe tuu na wengine ni "wapambe nuksi", maadamu sauti tumepasa na tumesikika, tumetimiza wajibu wetu, utekelezaji ni mambo yao ya ndani!.
Nashauri kama ni kelele kwa sasa zimetosha, tuweke kalamu chini na kuendelea na maisha!.
P.
 
Hivi chadema itashinda kwa kura za kina nani? wachagga? wako wangapi nchi hii?

Wewe zomba tumeshakujua...unajaribu kufanikisha aliyekutuma, thread zako zote ni za uchochezi wakikabila na kidini na nia yako uwatoe watu kwenye mada halisi. Pole sana kwa hili wala sikujibu....na nashauri watu wawe makini na jinsi unavyochangia.
 
Mkuu BAK, lengo la tendo la ndoa kwa mujibu wa mafundisho yote ya dini zote na jamii zote, was ment lifanywe ndani ya ndoa!. Lakini kabla tendo hilo halijafanyika, lazima kwanza umtafute umpendae, umpende, umpose, ndoa ifungwe ndipo ufaidi matunda ya ndoa!.

Sasa mambo yamebadilika, watu hutanguliza kwanza kufaidi "tunda" ndipo ndoa ije au isije kabisa!. Sasa wakati wa kumtafuta mchumba, ni lazima umto..ze ili akubali. Njia na mbinu mbali mbali hutumika na wakati mwingine hata ahadi ya ndoa, ili tuu upate "ridhaa", ugaiwe lile tunda ule ufaidi!. Na ukisha gaiwa tunda, ama kupata ulichokitaka, " the end justfies the means" hivyo njia zozote za ulizotumia zinakuwa justified!.

Wale wanawake waliokukubalia kukupa tunda kwa ahadi zako na kuja kujikuta kumbe walidanganwa, hakubatilishi ridhaa zao kuwa waliridhia wenyenyewe na hivyo wewe ulilipata tunda "kihalali" na kulimega na kula!.

Hivyo ndivyo siasa, mpiga kura ndiye "mrembo" wetu. Ushindi, kushika madaraka na kutawala ndilo "tunda" letu na zile kampeni za uchaguzi ndiko kuto..za kwetu!. Kama ilivyo kwa wanawake, wako wale wanaochia tunda kwa ofer tuu ya soda na chips kuku, vivyo hivyo wako wapiga kura watoa ridhaa zao kwa ile shibe ya siku moja!. Kama walivyo wanawake wanaoachia kwa ujira kidogo wa hongo iwe ya pesa, vijizawadi zawadi an ahadi zozote, nitakujengea nyumba, nitakununulia ndege, nitakuoa etc, ili mradi ridhaa imepatikana, vivyo hivyo wapiga kura wametoa kura zao kwa ridhaa zao baada ya kupatiwa chochote, iwe ni t-shirt na kofia, iwe ni ahadi za kweli za maisha bora kwa kila Mtanzania, au ni ahadi za uongo, at the end of the day, kinachotafutwa ni kura, na zikishapatikana, zina "justfie the means"!

Kuhusu zile zinazopingwa mahakamani, hizo ni sawa na rape cases au under age!.
Hivyo hata kama CCM, walichakachua, walidanganya, walihonga, waliiba na kufanya kila mbinu, anayetangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, anakuwa ni "mshindi halali" na kama unakumbukumbu nilipandisha thread ya kulaani kumtambua kuwa its a "mistake" na "wastage of time" na nilipandisha thread hii!.Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.
Uhalali wa ushindi wa urais ni tangazo la NEC, nani kashinda, na likisha tangazwa huo ndio "uhalali" ninaozungungumzia, bila kujali mbinu zilizotumiwa, safi, chafu, za kimafia, kuchachuwa, mshindi ni mshindi "halali"
"The winner takes it all, the looser standing standing small"-Abba.

P.

P.
 
Mkuu Kisugujira, kama nikweli, lisemwalo lipo, na kama halipo linakuja, basi sisi ndio tumesema na tusubirie hiyo 2015 tushuhudie!. Kuomba tutaomba ila sio kwa kukesha, kwa maana tunaijua siku ni Jumapili, tarehe 25, October, 2015 na tunaijua saa ni kuanzia saa 12:00 asubuhi (labda katiba mpya ibadili)!.
P.
 
mtoa mada hajaweka waz CDM ibadilikke kwalip, we unaweza ukaambiw badilika na hujawekwa waz na ukabadilika sijui utabadilika kwa lip? achen kukurupuka.
Mkuu IBRAAH, nimeupdate ile 1st post!.
 
Mkuu Msemaji Ukweli, nimwaambia Chadema ili waingie Ikulu ile 2015, lazima kwanza mambo mawili yafanyike.
1. Wabadilike
2. CCM isimsimamishe yule mgombea!.

Sasa Chadema, hata wakibadilika vipi, kama 2015 CCM itamamisha "yule" mgombea, then Chadema inapigwa chini kwa kishindo na bila huruma, ngoma inakuwa ni CCM tena. Hili nimelisemea hapa!.Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then ...

P.
 
Pasco Naomba unifumbue macho zaidi.
Umesema kwa sauti kubwa sana, VIONGOZI WA CHADEMA WANATAKIWA KUBADIRIKA" nimekusikia pia vizuri sana kwamba wanatakiwa "KUFANYA MAMBO YAO KWA USAHIHI" Naomba mifano tafadhali.
Mkuu Sangarara, nime update 1st post.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…