Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Pasco, mimi naomba uniruhusu tu nikuoneshe (siyo kwamba nakutukana, hapana) jinsi mambo mengine unayoyasema siyo tu kwamba ni ridiculous lakini hata kwa akili ya kawaida they dont make sense at all. Unaanza hivi;
Uliposema hivyo nilikuwa nina matumaini kwamba unasema kweli lililo moyoni mwako na kama ni hivyo unapoongezea hili;Mkuu Mbalinga, nakubaliana na wewe kuwa Chadema is doing a good thing and a right thing, kuleta matumaini mapya.
Kwanza, hivi hao Watanzania unaowasema na wewe uko miongoni mwao ama ni swali la ninyi na sisi. Hilo ni moja lakini kubwa zaidi unadai unataka uone mbadala wa CCM kwanza, ndio uipe likizo CCM... sasa swali hilo litawezekanaje ndugu yangu? Unajua wazi kabisa kuwa Chadema haina dola, hawakusanyi kodi na sera inayotumika nchini ni ya CCM. Huo mbadala utauonaje? Kwenye kukosoa? Kwenye kupinga? Kwenye kulalamika? Kwenye kudai? Kwenye kuelimisha? Mbona hayo wanayafanya sana tu...hii labda ingewezekana kwa nchi za wenzetu kama Marekani ambako kuna Governors wa States ambao huchaguliwa na wananchi na si lazima watokane na chama tawala. Kwetu hapa hata huyo mbunge wa Chadema anaweza kutiwa ndani kwa amri ya kada wa CCM mkoa.Watanzania wanahitaji kwanza kuona mbadala wa CCM, ndipo tuipe likizo CCM, tuwapeleke Chadema ikulu!.
Hapa tena unajikanganya hata usieleweke, unapimaje uwezo wa timu ambayo hata kuingia uwanjani bado. Hiyo Chadema itategemewa kutekeleza aina gani ya ahadi huku sera zinazotekelezwa ni za chama tawala. Nilifikiri ungeweza kuipongeza Chadema kwa kuibana CCM hadi kuna wakati sera zake imebidi chama tawala iziige ingawaje hilo hawawezi kulikubali wazi wazi. Pasco ingekuwa kwamba huko nyuma Chadema waliwahi kukamata dola, hapa labda ungepata hadidu rejea lakini mmmh!Hili la kusema tutafanya hiki, tutafanya kile, ndio CCM ways with lots of promises zilizoishia kuwa empty promises.
Ni kitu kimoja tu kilicho kweli hapa, nacho ni jinsi CCM wanavyotuahidi kila baada ya miaka 5 (kama walivyotoa ahadi karibu mia moja mwaka 2010) lakini utekelezaji ni sifuri. Sasa hapa lawama unazozitoa kwa Chadema ni zipi? Ni ahadi gani walitoa na kama walitoa na hawakupewa nafasi ya kutekeleza lawama zinatoka wapi? Kwa kweli hizi zako ni reasoning masikini ambazo zinaweza kutolewa tu na watu wasio na uelewa wowote serikali yetu inavyoendeshwa. Ombi langu kwako ni kwamba tujaribu kwa pamoja kuondokana na huu woga wa Tanzania bila CCM...hii tabia ndio inamsukuma mtu kama wewe Pasco kuwakumbatia watu kama EL eti mradi tu ni wana CCM, inasikitisha sana.Chadema nao wakiahidi, elimu bure, afya bure, mfuko wa sementi elfu tani, tutaondoa umasikini, bila kusema how, unakuwa hujaonyesha mbadala wowote kwa CCM, nazo ni ahadi tuu kama CCM wanavyotuahidi kila baada ya miaka 5!.Pasco.