Wanabodi, Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is nothing to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...
- Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
- Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama vile ni mbali, unless wamsimamishe their one and only jewel!.
- Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakiichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
- Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, sasa wameichoka, hivyo uchaguzi wa 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
- Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
- Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
- Kama uchaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
- ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema!.
- So far so good, Chadema is doing a good job kwa sababu M4C is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
- Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kuzifanyia kazi hizi hoja na tatu mkubali kubadilika!.
Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.Kwa wale wapenzi wa Chadema, for sure, Uchaguzi wa 2015, Chadema inaweza kabisa Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If "Itabadilika" and provided that CCM haitamsimamisha yule mgombea wangu!. Japo ni vema kuwa na great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best na kama Chadema haitabadilika, you better get prepared for the worst kwa sababu 2015 itakuwa ni CCM Tena!.NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.Naomba kuwasilisha.Pasco.UP DATE 1.Kufuatia maswali mengi kuhusu Chadema wabadilike nini, naomba kumnukuu mmoja wa great thinkers wetu humu jukwaaniNB. Kwa maswali yoyote kuhusu haya mambo ambayo Chadema inahitaji kubadilika, naomba uyaelekeze moja kwa moja kwenye thread husika!.
Mkuu Pasco,
Mimi hapo sijaona chochote ulichoeleza maana unachanganya watu na hili ndilo tatizo ambalo pengine unalo wewe na rafiki yako Mchambuzi.
Hivi mambo yote yanayoendelea hivi sasa dhidi ya CHADEMA huyaoni?- yaani propaganda, ukandamizaji unaofanywa na Polisi na mambo mengine ya kuhakikisha CHADEMA inapatwa na misukosuko kwenye shughuli zake za M4C?
Unapotosha kwamba CCM au CHADEMA wanapendwa kwa ajili ya umaarufu hilo ni kosa la kiufundi. Vyama hivi vina sera zake na ni sera za kila chama ndizo zinazoangaliwa na wapiga kura na si vinginevyo.
Lakini kwa kuwa wafuasi wengi wa CCM wamekuwa wakifaidika na mfumo mbovu uliojengwa kwa miaka 50 iliyopita, wamekuwa wakisaidia kudhoofisha mawazo mbadala na leo hii wengi wanaona makosa ya wafuasi hao wa CCM.
Kama unavyoona rushwa imeota mizizi, uchumi umeshikiliwa na wageni na ni mbovu uliojaa mianya mingi ya kutoroshea fedha za watanzania nje ya nchi, pesa za watanzania zimehifadhiwa benki za Switzerland (bilioni 300 hizo) kwa njia zisizo halali, jeshi la polisi halifanyi kazi zake za kutumikia jamii bali kuishughulikia jamii hiyo.
Suala la ajira limekuwa tatizo na leo hii unaona vijana wengi wametapakaa mijini wakiwa wazururaji na wakiishi maisha ya kubahatisha, ajira hazina usawa bali ni ni nani unamfahamu na matokeo yake unaona vijana wengi watoto wa wenye nazo ndio wameingizwa kwenye ajira hasa zile za watoa ahsante kwa CCM.
CHADEMA "are doing things right" kwa kutumia busara kukabiliana na vurugu za vyombo ya serikali ambayo kazi yake mpaka sasa imeonekana kwenye maeneo mbali likiwemo eneo la Iringa ambapo mwandishi marehemu Mwangosi aliuwawa na Polisi.
CHADEMA itaendelea kupata msaada zaidi wa namna ya kukwepa athari hizi hasa kwenye kuelekea uchaguzi wa 2015.
Kuhusu CCM kushinda chaguzi zake kihalali hio pia sio sahihi ukizingatia matokeo ya uchaguzi mwaka 1995, 2000, 2005 2010 yote yalikuwa yakitoa malalamiko kwamba kulikuwa na mapungufu katika zoezi zima la kuhesabu kura.
Hivyo hapo ungekuwa na wazo labda pawepo kituo kikuu (nerve centre) ambacho kitajumuisha wawakilishi wa vyama vyote vya upinzani ambao watakuwa wakipokea matokeo ya kutoka kila kituo cha upigaji kura nchini kote. Nikikuwa nafikiria kwamba Switzerland wataporudisha zile pesa zetu zilizoibiwa, basi pesa hizo zitumike kujenga mfumo wa upigaji kura wa kipekee kabisa kuwahi kuwepo Afrika na uwe unatoa matokeo yasiyopigiwa kelele.
Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama vile ni mbali, unless wamsimamishe their one and only jewel!.
Hapo naona unamaanisha kwamba labda CCM itamsimamisha mheshimiwa rafiki yako EL ili aje akinusuru kuweza kushinda uchaguzi mwaka 2015. Hilo pia ni kosa kufikir EL anaweza kufanya chochote akiwa CCM. Si unaona pesa anayotumia kufanya PR ya nguvu? Je umejiuliza pesa hiyo inatoka wapi? fanya utafiti lakini hiyo pesa yote ipo mahali na inatoka kidogokidogo.
Nilikuwa nafikiri, ili EL aweze kutimiza ndoto zake za kuwa raisi ni budi ahamie CHADEMA na awe mgombe mwenza, lakini hilo haliwezekani kwani EL ana DNA ya CCM na haitakuwa jambo la busara kuhamia CHADEMA. Isipokuwa ikiwa atashinda ubunge kupitia CCM na tukawa na bunge mseto basi anaweza kubahatisha uwaziri.
Kwahio mkuu Pasco na mwenzio, kazi ya "spin doctor" hamuwezi kabisa na hiki ulichoandika hamna chochote kipya.