Wanabodi,
Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Kipima Joto cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulifikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.
Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.
1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.
Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yatu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.
Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.
Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.
Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.
Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa puli wa Mtanzania!.
Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is no one!.
Mwenye masikio na asikie!.
2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.
Najua wapinzani wa ukweli, watakuja na hoja za dhabi kubwa ya Lowassa ni Richmond, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipo Simbiaon capacity charge ile ile ya dola 152 kama richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanya moto, tumerika maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.
3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.
Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulani kama kumsukuma mlevi!.
Mwisho.
Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM itaukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Lowassa ili kuweza kujiokoa?, itakubali kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji, kwa kutegemea katiba impya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all people all times?!.
Asante.
Pasco.
NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.