Pasco, umejitahidi kufanya analysis yenye ushawishi, lakini kuna baadhi ya mambo ambayo naona haukuyatilia maanani (sijui kwa ushabiki au ni oversight tu). Kwanza, kwa ujumla, shida ya tanzania sasa hivi sidhani kama ni mtu mzuri wa kuongoza. tatizo kubwa linbaloikabili Tanzania hivi sasa ni mifumoya kiongozi ambayo haifanyikazi vile inavyotakiwa. Labda suala hili ndilo linalotutias giza na kuanza kuwajadili watu badala ya issues kwa sababu lenyewe linahusiana na personality pia.
Mkuu Mpitanjia, haya usemayo ni kweli tupu, mimi sikuyatilia maani sio kwa oversight wala sio kwa ushabiki, bali kwa uhalisia, hili la shida halisi ya Watanzania sip pesonalities, ni mifumo, huu ndio ukweli halisi, ila wenye kuujua ukweli huu ni the elite group ambao hata kura sidhani kama huwa wanabiga!. Watanzania wote waliobaki ambao ni waliowengi, huwa hawachagui sera, wala hawachagui chama bali wanachagua mtu!. Nenda kwenye data Alaysis ya uchaguzi wa 2010, utashangaa watu wa Vunjo wamemchagua Lyatonga kwa kura nyingi kwenye ubunge, na watu hao hao wakamchagua JK kwenye urais!. EL akisimama na yoyote, hakuna yoyote mwingine wa kushindana naye, watu waangalia sura tuu na hivi nywele zake ni nyeupe kama za Nyerere ndio kabisa, vizee vyote vitamchagua as if Nyerere amerudi!.
Lowassa au mtu mwingine anaweza kuonyesha quality za kiongozi mzuri lakini uongozi ni teamwork ambayo inapaswa kusaidiwa na mdumo mzuri. hapo yanaweza kuibuka matatizo mawili makubwa ambayo yanaweza kumfanya Lowassa ashindwe akishinda. Lwanza atakuwa na tiumu ya watu kutoka CCM ambako tayari kuna madonda makubwa na kpiga vita kwa hatari sana. Pili, huku akiwa na tiumu ambayo inatafunana ndani kwa ndani, atakumbana na mfumo ambao umegota kuanya kazi. Kwa kiasi kikubwa hata Kikwete ameshindwa kutokana na sababu hizimbili kuu.
Tanzania ilipofikia, haihitaji uongozi wa team work, inahitaji uongozi wa kijeshi type, you must do your job or fall out!, Kagame type, watu sasa they don't need a leader to show them the way, they need a ruler to rule, kunyoosha kwanza mambo nchi hii itoke kwenye mess we are in ndipo baadaye tutafute leaders!. JK ameshindwa simply because ni "dhaifu" period!. EL sio dhaifu!, he will rule with iron hand just to put things right on the track back again, ndipo tuendelee kubembelezana!.
Kwa hali ilivyohivi sasa CCMinapaswa kufa na kuzaliwa upya, na izaliwe mpya kweli, ikiachana na ya kale yote. Hili ni jambo ambalosidhani kama linaweza kutokea lenyewe na sioni uwezo wa Lowassa kulifanyahili litokee.Lakini pia kwa kiasi fulani Lowassa ameonyesha dalili za kuendeleza malumbano ya kutafunana kwa sababu ajalikana kuwa nimtu wa visasi.Mbaya zaidi, wakati wakiendelea kutafunana ndaniya CCM, huko nje Chadema, CUF na ADC nazo zitakuwa zikiendelea kuwatafuna. Unadhani Lowassa anaweza kweli kukabiliana na hali hii hasa ukizingatia wasi wasi wakokuwa afya yake inaweza kuwa na mushkeli?
EL is the man for that, kwa vile yeye ni CCM, na ni CCM imemtenda, he is the one and only, anayeweza kuinyoosha CCM na kushikisha adabu!, kwanza ataifumua yote na kuvunjilia mbali mitandao yote dhalimu!. Watu kama Six, Mwakiembe na wale waliojiita makamanda, kuna wengine watafuta pa kukimbilia na for sure kuna watakao ozea Segerea stating with Six na Mwaki, unless waikimbie nchi!.Kwenye chaguzi zote za nyuma, CCM was the determinant factor, ilikuwa inajiamulia, inataka kumsimamisha nani, Uchaguzi wa 2015, CCM sio determinant tena, kwa sasa determinant factor ni Chadema, its the one that ai calling the shots na CCM inapelekwa pelekwa kama inavyokimbizwa sasa, hata sina uhakika kama watu kama kina Nape wanalala usingizi!.Kufuatia kasi ya M4C, hakuna ubishi CCM imekalia kuti kavu na iko mkao wa kifo, hivyo kuelekea 2015, juhudi za CCM sio kutafuta kiongozi bora, bali kuangalia jinsi ya kijuokoa au kujinasua na kifo kilichoko mbele yake ambacho ni dhahiri!. Mkombozi pekee anayeweza kuinusuru CCM na kifo cha mende, is one and only EL!, hivyo CCM is left with no options, to live or let die!. Ikichagua kuishi, lazima imchague EL, vingenevyo 2015 ni bye bye CCM!.