Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

kama naiona Chadema itakavyopeta 2015. Mnamweka mwizi ndo awe rais? Wewe pasco na wasiwasi na thinking capacity yako!
Mkuu Chimunguru, huna haja ya kuwa na wasiwasi na thinking capacty yangu, kwa kifupi iko very low ila hii ndio level ya wapiga kura wetu.

Hakuna kitu kizuri kama kuwa ma matumaini na matarajio makubwa kuwa 2015 ni Chadema, itatinga ikulu ya magogoni, nilichotoa hapa ni angalizo kuwa kuwa iwapo CCM itamsimamisha EL uchaguzi wa 2015, nyie Chadema na wote wenye matarajio kama yako, Ikulu mtaishia kuisikia kwenye bomba!.

Kwa vile wengi humu mmehamanika na great expectations za ikulu, ikitokea mkaokosa, mtaishia kukata tamaa na hivyo kuwa tayari kwa lolote, hivyo angalizo hili ni kuwaandaa watu kama nyinyi kwa kama ni EL, 2015 ni CCM tena!.
 
Mkuu, Mpita njia, JK ni populist leaders, ma populist leaders wote wanapenda sana sifa kwa kuimbiwa nyimbo za shangwe na mapambio hata kama nathing is realy done!. EL yeye ni action oriented leader anayetaka kuona na kuhakikisha the work is done.

Kwenye ile team ya Boys II Men, EL alimu outshine JK vibaya sana!. JK akitembelea mahali, hupokelewa kwa shangwe na kupewa taarifa ya maendeleo yenye maneno mazuri kwenye makaratasi with nothing on the ground, yeye huridhika na taarifa na kuendelea na ziara, tena anapangiwa very tight schedule, ili asione ukweli!. EL alipokea taarifa na baada ya hapo alilazimisha kwenye site to witness with his own eyes na hapo ndipo tofauti ya viongozi wasemaji na watendaji.

Ilifikia point, huko mikoani wakisikia JK anakuja, hawana wasiwasi, wameshamjua anapenda nini, anatayarishiwa ile kitu roho inapenda, akifika ni hutuba tuu za kwenye makaratasi jioni ni mambo yetu yalee..kazi kwisha!. Lakini wakisikia anayekuja ni EL, huko kunakuwa na mtafutano, watu hawalali, maana jamaa sio mchezo!, japo na yeye pia kama binadamu, mambo yetu yale naye anayakwakwe, lakini angalau kazi inaokekana japo nae pia ni kazi na dawa!.

Katika mazingira kama haya, bwanamdogo una mu outshine boss wako, nini kitatokea?, ni kuwa flushed out!. Na baada ya kumflush EL, wengi mmeshuhudia jinsi serikali ya JK ilivyo flop!.
 
mimi naona kuwa sera na nia ya dhati ya kuitekeleza hiyo sera ndio muhimu zaidi. sera ni lazima itokane na wanachi wenyewe yaani watanzania. Tanzania ina watu wengi sasa ukisema kuwa EL ndio pekee anayeweza unakuwa kama unafanya kampeni. hiyo ni subjectivity.
jambo la maana ni sote tujadili kuwa tanzania tunataka nini hasa kilimo au elimu kwanza n.k. matokeo ya mijadala yetu ni kuwepo kwa sera. hapo tutaweza kumchagua mtu atuongoze kupitia sera hizo kufikia malengo yetu. mtu si hoja kwanza. EL si mtume wala si nabii hata ufikie kusema ni yeye pekee.
 
Sasa Pasco hapa ndipo tatizo jingine la Lowassa litakapotokea. Sysyem ya uongozi iliyopo hivi sasa imezoea kwua na kiongozi mpenda sifa, nao wakabibea kwenye kusifian kwa sababu walijua kuwa hicho ndichom kipimo cha utendaji kazi wao. Kuna tatizo la jumla yanapokuja mabadiliko, hasa mabadiliko ya ghafla. Kutoka kuwa kiongozi bingwa wa kusifia, hadi kuwa kiongozi mchapa kazi ili kuonyesha matokeo ni jambo gumu kwa aina ya watu, si tu viongozi, tuliopo Tanzania leo hii. Ndio maana awali nilisema kuhusu 'team work'. Lowassa anaweza akaingia na udikteta wake na hapo ndipo matatizo yake yataka[poanzia kwa sababu ya ukinzani (si upinzani) atakaokumbana nao.
lakini, hilo ni kama akiingia. Kuna wengiw aliopo katika mfumo wa uongozi hivi sasa wanaofahamu hulka ya Lowassa, nakuhakikishia, hawa wanaweza kuungana ili kuhakikisha shindi kwa sababu wanajua chini yake hawataweza. Sijui ni kwa nini unaona kwua njia ni nyeupe kwa Lowassa katika mazingira kama haya
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzamifu, kama ni kujadili, tumeshajadili sana humu, yote usemayo ni kweli, ili amini usiamini, kwa tuliyofika sasa, Watanzania, hawachagui seri, chama, itikadi wala ilani!, Watanzania wanachagua mtu!, EL ni maoni yangu kama mtu pekee, ila na wewe kama unaye pia mlete tumjadili, nilichosema mimi, kwa hapa tulipofikishwa sasa, EL hana mpinzani ndani na nje ya CCM, he is the one and only!.
 
Kwa kweli huu ni zaidi ya ushabiki. 2015 watu wengi hawataki CCM no matter anagombea nani? Ukitaka kuhakikisha jinsi watu wanavyoichukia CCM nenda sehemu yeyote public hata unaponunua gazeti jifanye unaisifia CCM utaona macho ya watu. Utatamani ukimbie.
 
Mkuu Mpita Njia, hili, hili wewe unaloliona kama ni tatizo kwa EL, hiyo ndio strength yake!. Kikweli jamaa akiingia, kuna viongozi wanaweza mpaka kula bakora mbele ya wake zao!. We have had enough of the nonsense, we now need a no nonsense man! EL is the one and only kwa upande wa CCM!.
 
Mkuu Mpitwanga, usemayo ni kweli, angalau wewe unasikilizia sauti za watu hizo sehemu public jinsi wanvyoichukia CCM, mimi nimezama field na kushuhudia jinsi Chadema inavyopendwa, mikutano yake inafunga funika bovu!, tatizo tukija kwenye sanduku la kura, hatuwaoni hao watu unaowasema, wengi ni wasemaji wazuri na walalamika wakubwa huko kwenye vijiwe vya kahawa, lakini sii wapiga kura hao!. Hao wanaolalamikia CCM ni furahisha genge tuu, wengi wao midomoni ndio Chadema, lakini mioyoni ni CCM, haswa kwa kuzingatia wengi wao pia ni kulipa fadhila za T-shirt, kofia na ile shibe ya siku moja!.

Ila pia chuku kubwa kwa CCM ni shauri ya udhaifu wa JK, kwa vile EL sii dhaifu, akisimama yeye, ile chuki yote dhidi ya CCM itayeyuka na kugeuka upendo kwa CCM na utashangaa jinsi CCM itakavyoshinda kwa kishindo mwaka 2015 but only if itamsimamisha EL, vinginevyo bila EL, tutashuhudia anguko kubwa la CCM kwa kufa kifo mende huku kinajiangalia!.
 
Mkuu pasco mimi pia nimekuelewa nami kwa sehemu naona EL anakidhi kwa kiwango fulani kwa mtazamo wangu lakini wavumao baharini ni papa lakini wengine wamo. ndo nikasema hebu tuone kwanza tunataka nini kama alivoshauri mwalimu mwaka 1995. tunataka rais awe mtu mweye sifa zipi awe rais. watu ambao kisirisiri wanafanya vitu sasa hivi ili kutushawishi kuwa wanafaa kkugombea urais ndani ya CCM wanatakiwa waangaliwe kwa makini sana. wanaweza kuwa hatari baadae.
 

Mkuu Bigirita, mtazamo wako ni wa kisomi zaidi na umekweenda deep, mimi nazungumza lugha ya wapiga kura!, wapiga kura wetu, hawapigii kura system, hawapigii kura vyama, hawapigii kura sera, wao wanapigia kura mtu!, nikauliza na ninauliza na kuuliza tena, kama CCM ikimsimamisha EL,who else can dare challenge him?, ndio maana nimesema, uchaguzi wa 2015, kama CCM ni EL, then matokeo ni CCM tena, EL ndani ya CCM hana mshindani, na nje ya CCM, hana Mpinzani!.

Hizi hoja za EL hasafishiki hazina mashiko!, kwani Wapiga kura wanachagua wasafi?. JK alipoingia na kuchaguliwa kwa 80%, aliikuwa na usafi gani?!. Watanzania wanachagua sura tuu, hapo ulipo, hebu funga macho, imagine unaiona sura ya EL kwa CCM, hebu ifikirie sura gani ya nani mwingine anaweza kusimama nae akachaguliwa?.


Mimi nawazungumzia Watanzania hawa wanaochagua sura kuwa kama kwa uchaguzi wa 2015, sura ya CCM ni EL, then matokeo ni CCM Tena!.
 
Pia naona elimu ya urai yafaa kutolewa kuanzia sasa. vyama hiari, vyombo vya habari, majukwaa ya kijamii, asasi mbalimbali vianze kutoa elimu ya uraia kupitia majukwaa yao kwa kasi ili kupitia elimu hiyo ifikapo 2015 wanachi waweze kushiriki wote kufanya uamuzi sahihi. kwa kweli umefika wakati wa kuzaliwa upya. tunataka maendeleo, tunataka maelewano, amani na utulivu zaidi tunataka haki na kila mtu atimize wajibu wake . hatutaki ufisadi kamwe!
 
Mkuu Mzamivu, ni kweli wavumao bahari ya CCM ni papa, na wengine wapo, hao wengine wavumao CCM, hao ni papa usingizi, EL ni papa upanga!. Hoja ya kutoteuliwa EL ni moja tuu, nayo ni kuhusu afya yake na hapa ndipo kifo cha mende kwa CCM kitaifika huku kinajiangalia!.

Hao wanaofanya kisirisiri, wanasumbuliwa tuu na njaa zao, ukimuondoa EL, then Membe, tena Membe mwenyewe as Membe sii lolote sii chochote bila back up ya EL!, CCM itapigwa chini kama kuupuliza unyoya!.

Ile enzi ya Mwalimu ya kuwapima wataka urais kwa vigezo, imepita, kwa sasa concentration ya CCM sio jinsi ya kuendelea kutawala, bali jinsi ya kujiokoa, kwa hiyo mgombea wa CCM ajae ni mtu atakayeweza kuikoa CCM, nothing more, nothing less!.

Kufuatia mimi kutokuwa na chama na sifungamani na chama chochote, nimekuwa nikipigia kelele haja ya sisi wana jf kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kuwa pamoja na mabaya yote ya CCM, pia kuna mazuri ambayo CCM imelifanyia taifa hili!. Sambamba na mazuri hayo, pia hakuna ubishi, CCM imeoza na kunuka rushwa huku viongozi wake wakigubikwa na ufisadi wa kutisha!, lakini ndani ya CCM hili hili lililooza na kunuka rushwa na ufisadi, bado kuna viongozi wachache wa CCM ambao ni watu safi, waadilifu na hawana uchafu wala tuhuma zozote za ufisadi na hawana hata chembe ya harufu ya rushwa!.

Mfano wa watu safi ndani ya CCM na wasio na mawaa yoyote, wenye sifa za kutwaa uongozi wa taifa hili ni Dr. Ali Mohamed Shein, huyu ni muadilifu wa hali ya juu, asiye na uchu, kashfa, tamaa au tuhuma yoyote iwe ya ukware, rushwa, ufisadi au majungu yoyote!. Tena kwa kuzingatia bara tumeshatoa rais kwa mara mbili mfulilizo, safari hii ilipaswa kuwa ni zamu ya Zanzibar!. Mtihani pekee ni jee mtu safi huyu, anachagulika?. Jee anaweza kuikoa CCM na kifo kinachoinyemelea?!. Panga pangua, hakuna yoyote mwingine ndani ya CCM anayeweza kupangua mawimbi ya M4C zaidi ya EL!. hivyo 2015 ni ama EL ama CCM..Puu!, chini!.
 
Kiukweli, hiki ndicho kilichopaswa kufanywa hata kabla ya kuingia mfumo wa vyama vingi na ndicho sasa kinachofanywa na M4C, kuwafunguo macho Watanzania, na ni kwa kuizingatia kasi ya M4C, Watanzania wameamka na 2015, wataipiga chini CCM bila huruma, mkombozi pekee wa CCM dhidi ya kipigo hiki ni EL!.
 
Mkuu Fareed, mimi nimemwita EL ni waziri mkuu mtaafu, kwa vile hivyo ndivo anavyokuwa addresed officially, msamiati wa "Waziri Mkuu Mjiuzulu", au Waziri Mkuu Mjiengua" bado haujawa adapted, ukipitishwa, tutamuita kwa title yake stahiki!.

Kama ni kweli, EL amepenyeza watu wake humu jf na kuwapa pesa ili wampambe, na ikatokea mimi ni mhitaji wa hizo pesa, jee kuna ubaya wowote kwa mimi kumpamba ili nipate huo ujira?.

Naungano na wewe kuwa "upumbavu mkubwa kujaribu kumtakasa fisadi"!, ila nakuomba kuwa mkweli, mpumbumbavu zaidi ni mimi ninayeyaelezea mema ya mtu anayenyoonyesha vidole tuu vya ufisadi, lakini hana tuhuma zozote za ufisadi mbele ya sheria, hana kesi, yoyote, wala hajawahi hata kuitwa na kuhojiwa kwa jambo lolote kuhusiana na ufisadi!.

Lakini kuna mafisadi ya kiukweli ambayo ni majizi, yalikwapua mifwedha kibao kule BOT kwenye kasfa ya EPA, tena mifisadi hii ilikamatwa readyhanded, sio tuu haikushitakiwa, bali ilibembelezwa, kurejesha walivyokwiba and life goes on, jee mpumbavu hapa ni nani, anawatetea wasio na hatia kwa kunyooshewa tuu vidole, au analiyeyasamehe majizi yaliyokamatwa readyhanded?!.

Tuna viongozi wenye kesi za ufisadi mahakamani, JK alidiriki kupanda jukwaani kuwanadi kuwa hao ni watu safi na kuwaomba wananchi wawachague, jee mpumbuvu ni yupi, huyu anayesema humu jf kuwa EL hana kesi yoyote ya ufisadi popote, au mtetezi wa fisadi mwenye kesi kabisa mahakamani, huku kesi haijaisha, unamsimamisha jukwaani na kumnadi kuwa ni mtu safi?!.

Nimesema mara kibao humu, kama EL ni mchafu kwa ufisadi, CCM wote ni mafisadi, na kati yao mwenye afadhali ndio EL!. Kama ni kweli EL ni mtoaji rushwa mzuri, CCM yote imeoza kwa rushwa, hivyo kwa maoni yangu, ni heri ya mtoaji rushwa ambaye hatimaye utakiona alichokifanya kukuletea maendeleo kuliko asiyetoa rushwa na hana chochote afanyacho kuleta maendeleo na kama kipo, basi hakionekani!.

Chagua moja , "someone who is good for nothing"?, au "someone who is bad, but does something good for the people?!

Mimi nimemchagua a bad guy EL who can do good, na wewe endelea kuwachagua hao hao good for nothing!.
 
Mtoa mada hii sio mara ya kwanza kuiweka Mada ya E.L. kuwania Urais, sijamsikia yeye mwenyewe akisema hicho kitu ila tumeona yaliyotokea Arumeru Mashariki, Nafahamu 1995 ulikuwepo na yaliyotokea Chimwaga uliyaona, JK Mrisho alikuwa wa karibia mwisho kuchukua fomu za kugombea, na matokeo Mkapa akashinda Lowassa alikuwepo mengine yapo hapo chini
Ila nataka niwakumbushe hasa waandishi wa Habari mbona muda bado? na Vyama
(CCM) wana njia zao za kumpata mgombea, kwa wakati huu wapo katika Ngazi ya NEC ambayo ni kutoka kila Wilaya hao ndio wanaweza kuamua nani Rais ajaye kama ni msafi ni wao wala sio Wananchi, au WanaJF Jina likipita hapo ndipo muanze kumkampenia na itakuwa labda May 2015 lakini leo ni kutafuta tuanze kuchangia na uhasama wakati mnajua LOWASSA alishawapiga mkwara kuwa atakayemsema vibaya atakula naye sahani moja, lakini hakusema atakayemsema vizuri atampa nini ila naona wiki hili mmecharuka sana hapa JF
[post=4540994] BOFYA[/post] kuna pdf za KIM KARDASH ambazo nimezipenda km unaweza kuzisoma ok ila nachotaka kukueleza Bw Pasco ni kuwa hata Waandishi wa habari huwa hamtaki kujibu hizi tuhuma km ni za kweli au la sasa Watanzania kuelekea 2015 sio mambumbumbu kuanza kuwapigia kampeni. mapema hii
 
Last edited by a moderator:
Duh...!, Mkuu Ukwaju, umemaliza kila kitu!. Sina tena kitu cha kuchangia, nimebaki speechless!.

Namumuomba mode, aifunge hii thread, hapa ndio mwisho wake!.


Natoa wito kwa wachangiaji wengine mlioguswa, nawaombeni tusichangie tena uzii huu, baada ya kuzosoma hizo nondo, nawaombeni kuthibitisha kwa sasa ni hands down, nikisubiria tukaribie darajani, ndipo tujadiliane tutavuka vipi!.

Alamsiki.

Pasco.
 
Inaniwia vigumu kila nikitazama safu ya Chadema kumpata wa kumliganisha uzito na huyu bingwa wa uzito wa juu katika medani za siasa ya Tanzania.


Nashindwa kupata jibu ni mwana siasa yupi ndani ya chadema ambae atasimama haswa na kuwakinaisha Watanzania wamchaguwe badala ya Lowassa iwapo ataamuwa kugombea kiti cha Urais Tanzania?


Maana najuwa Mbowe hana hamu tena baada ya kugaragazwa vibaya sana na Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2005.

Slaa nae choka mbaya, hana jipya zaidi ya majungu na siasa zisizo na mpango, hata ujumbe kwa Mwema ni ushahidi tosha kuwa kaishiwa kisiasa.

Nilidhani Zitto ataweza kwa kuwa ni damu changa lakini napata mashaka kuwa siasa za ukanda za chadema zitampa fursa ya kugombea, dalili zote zinaonesha chadema wa kanda ya kaskazini hawamtaki kabisa. Kwa hiyo huyu nnamtoa kwenye kinyan'ganyiro.

Shibuda hata akipitishwa kugombea akiambiwa Lowassa anagombea atakataa kuchuana nae.

Ka Mnyika, haka bado sana, hata ubungo inamshinda na sijui kama atashinda tena hata akigombea Ubunge huko. Kwishnei.

Halima Mdee, huyu hana ubavu, huyu akisikia Lowassa anagombea labda ajitafutie umaarufu tu - kwa hiyo huyu nje.

Nani mwingine?

Natamani Lowassa atangaze mapema kugombea 2015 angalau chadema waanze kujitayarisha mapema na mgombea ambae uchaguzi hautokuwa boring, maana hao wote juu Lowassa atawaonea tu.

CCM inatisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…