Elections 2015 Kuelekea 2015: Nyota ya James Mbatia yaanza kung'aa kwa kasi

Elections 2015 Kuelekea 2015: Nyota ya James Mbatia yaanza kung'aa kwa kasi

Seif al Islam

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
2,156
Reaction score
639
Hii ni baada ya kuiumbua CCM na wabunge wake ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hoja yake mujarabu kuhusu udhaifu wa sekta ya elimu hususani kutokuwepo kwa mtaala maalumu wa kufundishia kwa kukosa umakini na busara spika wa bunge kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa ccm|9wasiowaza vyema) waliiondoa hoja ile kijanja janja na kumtukana mbatia.mungu si athumani muda si mrefu matokeo ya kidato cha nne yalitoka yakionyesha kufeli kwa wanafunzi asilimia 60 na zaidi.

Wachambuzi nwa mambo wanaeleza kuwa matokeo haya yaliiabisha CCM kwa kiwango kisichoelezeka huku yakimpandisha chati mbatia kwa viwango visivyotarajiwa na juhudi za kufifisha ukubwa wa aibu hii kwa kuunda kamati na kumjumuisha mbatia ziligonga mwamba na sasa kamati imemaliza kazi bila majibu ya maana.

Kitendo cha mbatia kugomea kujiunga na kamati hii ndicho hasa kilichozidi kumpandisha chati na kuonekana mzalendo wa kweli.

Kama haitoshi baada ya jengo la kule posta kuanguka mbatia alienda kushiriki kama mhandisi katika zoezi la uokoaji wa watu waliofikiwa mle ndani ya kifusi.

Kwa ujumla matukio haya yamempandisha chati ya kisiasa mbatia(so chama chake) na wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa anaweza kuitumia hali hii kama turufu ya yeye kugom,bnea uraisi 2015 kwa lengo la kuipandisha chati nccr-mageuzi inayoonekana kupoteza mwelekeo.
 
Hivi kuna mtubana ndoto za kuwa mbatia atakuja kuwa rais wa nji hii?

Sawa ameiumbua serikali lakini some dreams a way too big.
 
Sidhani kwamba anayoyafanya anasukumwa na ndoto za kutaka urais wa 'nji' hii. Wanaotaka washaanza kusema mbona? Na wengine washakaribia kutoana 'manundu'!

Hata hivyo, akiamua kugombea ni haki yake, ilimradi anatimiza kile ambacho katiba ya JMT inakitaka kwa mtu anayegombea urais. Uamuzi mwingine utabaki kwa NCCR kumpitisha, Tume ya Uchaguzi kumpitisha, na hatimaye wananchi watafanya uchaguzi wao kama watakavyoona.

Ngoja tuendelee kuifuatilia hiyo 'nyota' unayosema inang'aa, labda inaelekea mahali kama ile ya 'Mamajusi wa mashariki'.
 
CCM wanajua wana tishio kubwa sana 2015, nalo ni Chadema (isomeke Dr Slaa). Kwa kuhangaika wanajaribu sana ku-create another Dr Slaa ( wa kuchonga) ili 2015 azigawe kura za upinzani (Soma Dr Slaa). Walianza kwa Zitto lakini naona wameona ngoma haikolei, sasa wanahamia kwa Mbatia. Hawatafanikiwa!!!
 
Sidhani kwamba anayoyafanya anasukumwa na ndoto za kutaka urais wa 'nji' hii. Wanaotaka washaanza kusema mbona? Na wengine washakaribia kutoana 'manundu'!

Hata hivyo, akiamua kugombea ni haki yake, ilimradi anatimiza kile ambacho katiba ya JMT inakitaka kwa mtu anayegombea urais. Uamuzi mwingine utabaki kwa NCCR kumpitisha, Tume ya Uchaguzi kumpitisha, na hatimaye wananchi watafanya uchaguzi wao kama watakavyoona.

Ngoja tuendelee kuifuatilia hiyo 'nyota' unayosema inang'aa, labda inaelekea mahali kama ile ya 'Mamajusi wa mashariki'.
Urais? Mnaota mchana kweupe nyie. Mbatia hata ubunge hatapati, labda udiwani.
 
ccm wanajua wana tishio kubwa sana 2015, nalo ni chadema (isomeke dr slaa). Kwa kuhangaika wanajaribu sana ku-create another dr slaa ( wa kuchonga) ili 2015 azigawe kura za upinzani (soma dr slaa). Walianza kwa zitto lakini naona wameona ngoma haikolei, sasa wanahamia kwa mbatia. Hawatafanikiwa!!!

brilliant pbservation by ypou.
 
Kwa watu wanaofuatilia siasa kwa umakini huyu jamaa ni jembe;sio mnafiki,hana tamaa,ni msema kweli,anajuwa kujenga hoja,si mbabaishaji,tatizo ni kabila.
 
Wapi HUKO? Mkutano wao HUKO KASULU JUZI ulihudhuriwa na Watoto na BAISKELI TU... Sasa Hiyo NYOTA unazungumzia ya CCM? oh yeah Anavuna MATUNDA aliyoyapanda ndani ya CHAMA TAWALA... Hata MIMI ningefanya HIVYO CHAMA kilikuwa hakina PESA za kulipa Viongozi wake hadi MWENYEKITI sababu kilikuwa hakina KURA NYINGI hakina VITI MAALUM hapo ULAJI hakuna... Sasa GHAFLA unapata SHANGINGI la BURE na BENDERA kweli NYOTA imekunyookea...

Umeandika HII kwasababu ya UKWELI au Sababu ya USHABIKI?
 
kwa watu wanaofuatilia siasa kwa umakini huyu jamaa ni jembe;sio mnafiki,hana tamaa,ni msema kweli,anajuwa kujenga hoja,si mbabaishaji,tatizo ni kabila.
Tatizo la mbatia ni umamluki. Sio kabila wala nini ila ni chama chao kujigeuza "kuwadi" wa CCM
 
Naomba Dr Slaa akichukua urais 2015 amkumbuke kwenye ufalme wake kwa kumpa uwaziri wa elimu.
 
Wapi huko? Mkutano wao huko kasulu juzi ulihudhuriwa na watoto na baiskeli tu. Sasa hiyo nyota unazungumzia ya ccm? Oh yeah anavuna matunda aliyoyapanda ndani ya chama tawala. Hata mimi ningefanya hivyo chama kilikuwa hakina pesa za kulipa viongozi wake hadi mwenyekiti sababu kilikuwa hakina kura nyingi hakina viti maalum hapo ulaji hakuna. Sasa ghafla unapata shangingi la bure na bendera kweli nyota imekunyookea.

Umeandika hii kwasababu ya ukweli au sababu ya ushabiki?

Ni uchambuzi wa kisayansi na wala sio ushabiki.
 
kwa watu wanaofuatilia siasa kwa umakini huyu jamaa ni jembe;sio mnafiki,hana tamaa,ni msema kweli,anajuwa kujenga hoja,si mbabaishaji,tatizo ni kabila.
Undercover politicians wanaotumiwa na magamba kuidhoofisha cdm wananisikitisha sana.unakuta mwanasiasa mzima anapiga kelele na kujifanya mzalendo kumbe ni mchumia tumbo tu.wanawafanyia watanzania usanii na kujifanya wako karibu na jamii kumbe wana hidden agenda.time will tell.

Hata south africa kuna waafrika vibaraka walikuwa wanatumiwa na makaburu kuwahujumu weusi wenzao lakini wakati uliongea.vyama rafiki na magamba naviogopa kama ukoma.

Itafahamika tu nani ni nani.hawa wasanii watafeli tu.zaidi ya cdm sioni chama na wanasiasa wa ukweli kuleta mageuzi nchini.watawadanganya watu fulani wakati fulani lakini hawawezi wadanganya watu wote wakati wote.uelewa mdogo wa kisiasa kwa watanzania ni tatizo kubwa.

Magamba yametake advantage hiyo muda mrefu lakini cdm ndiyo kiboko yao.
 
ni uchambuzi wa kisayansi na wala sio ushabiki.

Huo UCHAMBUZI wa KISAYANSI Ulikuwa Huru? Ulipata Maswali ya kiudadisi? Au ndio wa NCHI YETU unajua hakuna UHURU wa WAANDISHI wa HABARI yoyote hawezi kuuliza PROBING QUESTION.

Mfano: Ni Sababu GANI RAIS aliamua kumteua JAMES MBATIA kuwa MBUNGE? Haudhani Rais Anapaswa kutoa sababu kwa Walipa kodi? Lakini Ana NGUVU hatakiwi kuulizwa. Hata wakati huu wa VYAMA VINGI vya KISIASA.

Haya, ELIMU nchini kwetu pamoja na kuwa ya KIMASIKINI haijawahi kufeli kwa Wanafunzi kiasi hiki; JAMES MBATIA kuchaguliwa kwenye KAMATI ni HESHIMA sio MATESO; Yeye ni alisha wahi kuwa MKUFUNZI wa SHERIA CHUO KIKUU nadhani Mawaidha yake yangesaidia... Kujiondoa ni ili kupata Umashuhuri? ina Maana pia kupata huo UBUNGE ni njia moja ya KUTAFUTA HUO UMASHUHURI ambao alikuwa hana kama MWENYEKITI wa NCCR-MAGEUZI?

Yeye Kwenda kwenye JENGO lililobomoka hakusaidia chochote yeye alisomea SHERIA na hata HIVYO alijazana pale na hakuokoa KIUMBE CHOCHOTE wote wamekufa na yeye yuko pale; zaidi ya kula CHAKULA KITAMU CHA HOTELI YA SERENA

KAMA angeokoa WATU TUNGEMPA SIFA... alijijaza na kutoa USHAURI kwa watu ambao sio Waokoaji... SHAME SHAME

Haya sasa baada ya KASULU na Baiskeli afanye MKUTANO MWINGINE ati ana nini tena? OH Wachambuzi wanampa NYOTA --- Mwambie aende pale Jangwani... na Wachambuzi wake... SIASA zetu tunaziamasisha Maofisini... hakuna anayelipenda JUA...
 
Yeye ndio amekutuma umsemee? Siku zote mfadhiliwa hawezi kumkashifu mfadhili wake. Huyu mtu ni CCM "C". Lakini pia hoja ulizoziwasilisha hazina uzito kwa kiwango ulichompamba.
 
Huo uchambuzi wa kisayansi ulikuwa huru? Ulipata maswali ya kiudadisi? Au ndio wa nchi yetu unajua hakuna uhuru wa waandishi wa habari yoyote hawezi kuuliza probing question.
Mfano: Ni sababu gani rais aliamua kumteua james mbatia kuwa mbunge? Haudhani rais anapaswa kutoa sababu kwa walipa kodi? Lakini ana nguvu hatakiwi kuulizwa... Hata wakati huu wa vyama vingi vya kisiasa.

Haya, elimu nchini kwetu pamoja na kuwa ya kimasikini haijawahi kufeli kwa wanafunzi kiasi hiki; james mbatia kuchaguliwa kwenye kamati ni heshima sio mateso; yeye ni alisha wahi kuwa mkufunzi wa sheria chuo kikuu nadhani mawaidha yake yangesaidia... Kujiondoa ni ili kupata umashuhuri? Ina maana pia kupata huo ubunge ni njia moja ya kutafuta huo umashuhuri ambao alikuwa hana kama mwenyekiti wa nccr-mageuzi?

Yeye kwenda kwenye jengo lililobomoka hakusaidia chochote yeye alisomea sheria na hata hivyo alijazana pale na hakuokoa kiumbe chochote wote wamekufa na yeye yuko pale; zaidi ya kula chakula kitamu cha hoteli ya serena

kama angeokoa watu tungempa sifa... Alijijaza na kutoa ushauri kwa watu ambao sio waokoaji... Shame shame.

Haya sasa baada ya kasulu na baiskeli afanye mkutano mwingine ati ana nini tena? Oh wachambuzi wanampa nyota --- mwambie aende pale jangwani... Na wachambuzi wake... Siasa zetu tunaziamasisha maofisini... Hakuna anayelipenda jua.
Ndo mana nimekuambia umaarufu huo ni wake na sio kama chama chake.
 
Mh. Mbatia sikumpa uzito sana kutokana na kuteuliwana Rais, lakini kwa sasa huwezi amini ni miongoni mwa wabunge wachache sana ninaowaheshimu sana.

Lakini pia hatuwezi kupuuza tetesi kuwa jamaa ni ajent
 
Sijawahi kumwamini huyu bwana wala kufikiri kuwa ni kiongozi anayefaa katika "NNJI HII" !
 
Back
Top Bottom