Elections 2015 Kuelekea 2015: Nyota ya James Mbatia yaanza kung'aa kwa kasi

Elections 2015 Kuelekea 2015: Nyota ya James Mbatia yaanza kung'aa kwa kasi

Undercover politicians wanaotumiwa na magamba kuidhoofisha cdm wananisikitisha sana.unakuta mwanasiasa mzima anapiga kelele na kujifanya mzalendo kumbe ni mchumia tumbo tu.wanawafanyia watanzania usanii na kujifanya wako karibu na jamii kumbe wana hidden agenda.time will tell.

Hata south africa kuna waafrika vibaraka walikuwa wanatumiwa na makaburu kuwahujumu weusi wenzao lakini wakati uliongea.vyama rafiki na magamba naviogopa kama ukoma.

Itafahamika tu nani ni nani.hawa wasanii watafeli tu.zaidi ya cdm sioni chama na wanasiasa wa ukweli kuleta mageuzi nchini.watawadanganya watu fulani wakati fulani lakini hawawezi wadanganya watu wote wakati wote.uelewa mdogo wa kisiasa kwa watanzania ni tatizo kubwa.

Magamba yametake advantage hiyo muda mrefu lakini cdm ndiyo kiboko yao.
Hata jua litoke magharibi kwenda mashariki cdm hakiwezi kushika nchi .hakuna watanzania wenye akili timamu wachague chama chenye ukabila. Hapa msaliti atakuwa mchaga ambaye hasapoti chama cha kabila lake.hicho ni chama chenu usitulazimishe tukipende .
 
Sijawahi kumwamini huyu bwana wala kufikiri kuwa ni kiongozi anayefaa katika "NNJI HII" !

Huyu Mbatia ni aina fulani ya wanasiasa wanaotengenezwa na watawala kujaribu kugilibu watz. Mbatia huyu watawala (ccm) wanajaribu kumtengenezea umaarufu kwa watz kwa malengo ya kisiasa huko usoni. Ni mwanasiasa wa kichina!
 
ndo mana nimekuambia umaarufu huo ni wake na sio kama chama chake.

Oh... Hapo sasa nitakuelewa... Kwahiyo SIO MSAADA kwake au kwa ChAMA CHAKE... Labda avuke MPAKA aende KENYA - Lakini HUKO lazima Uwe kwenye FAMILIA kubwa; Kabila Kubwa...
 
Mh. Mbatia sikumpa uzito sana kutokana na kuteuliwana Rais, lakini kwa sasa huwezi amini ni miongoni mwa wabunge wachache sana ninaowaheshimu sana.
Lakini pia hatuwezi kupuuza tetesi kuwa jamaa ni ajent

Mkuu Mjuni Lwambo, kama wewe huja-comfirm kuwa kuwa Mbatia ni ajent, moyo wa Mbatia unamsuta kuwa yeye ni ajent.
 
Huyu Mbatia ni aina fulani ya wanasiasa wanaotengenezwa na watawala kujaribu kugilibu watz. Mbatia huyu watawala (ccm) wanajaribu kumtengenezea umaarufu kwa watz kwa malengo ya kisiasa huko usoni. Ni mwanasiasa wa kichina!

Mkuu JBITUNGO, ina maana mheshimia Mbatia ni bidhaa ya bei rahisi na feki lakini inayopambwa kisawasawa na maccm?
 
Urais? Mnaota mchana kweupe nyie. Mbatia hata ubunge hatapati, labda udiwani....

Taratibu mkuu, wala usitetemeke, mwenyewe hajasema anagombea. Wala mimi katika post yangu sijataja kwamba anastahili kugomea. Nilichoeleza tu ni kwamba ni haki yake akitaka, huna na sina mamlaka ya kumnyang'anya haki hiyo. Akigombea, kushinda au kushinda yote ni matokeo, waamuzi wapigakura.
 
Huyu Mbatia ni aina fulani ya wanasiasa wanaotengenezwa na watawala kujaribu kugilibu watz. Mbatia huyu watawala (ccm) wanajaribu kumtengenezea umaarufu kwa watz kwa malengo ya kisiasa huko usoni. Ni mwanasiasa wa kichina!

Kwa hiyo watawala ndio waliomtuma akaseme ukweli kuhusu ubovu wa elimu, ndio waliomtuma ajiltolee huko alikosaidia? Endeleeni kutunga nadharia, lakini wanaosoma hapa wanajua lengo lenu.
 
Kwa watu wanaofuatilia siasa kwa umakini huyu jamaa ni jembe;sio mnafiki,hana tamaa,ni msema kweli,anajuwa kujenga hoja,si mbabaishaji,tatizo ni kabila.

Kwani Mbatia kabila gani, na kabila lake lina tatizo gani?
 
Taratibu mkuu, wala usitetemeke, mwenyewe hajasema anagombea. Wala mimi katika post yangu sijataja kwamba anastahili kugomea. Nilichoeleza tu ni kwamba ni haki yake akitaka, huna na sina mamlaka ya kumnyang'anya haki hiyo. Akigombea, kushinda au kushinda yote ni matokeo, waamuzi wapigakura.

hana haki kwa sababu hana uwezo
 
Washikaji Mbatia ana haki ya kufanya hivyo si mnakumbuka alivyofanywa Mtwara? Washkajihapahakuna kuhama kwenye njia,hapa hakuna kulala mpaka walale wao:bange:
 
Huo UCHAMBUZI wa KISAYANSI Ulikuwa Huru? Ulipata Maswali ya kiudadisi? Au ndio wa NCHI YETU unajua hakuna UHURU wa WAANDISHI wa HABARI yoyote hawezi kuuliza PROBING QUESTION...
Mfano: Ni Sababu GANI RAIS aliamua kumteua JAMES MBATIA kuwa MBUNGE? Haudhani Rais Anapaswa kutoa sababu kwa Walipa kodi? Lakini Ana NGUVU hatakiwi kuulizwa... Hata wakati huu wa VYAMA VINGI vya KISIASA...

Haya, ELIMU nchini kwetu pamoja na kuwa ya KIMASIKINI haijawahi kufeli kwa Wanafunzi kiasi hiki; JAMES MBATIA kuchaguliwa kwenye KAMATI ni HESHIMA sio MATESO; Yeye ni alisha wahi kuwa MKUFUNZI wa SHERIA CHUO KIKUU nadhani Mawaidha yake yangesaidia... Kujiondoa ni ili kupata Umashuhuri? ina Maana pia kupata huo UBUNGE ni njia moja ya KUTAFUTA HUO UMASHUHURI ambao alikuwa hana kama MWENYEKITI wa NCCR-MAGEUZI?

Yeye Kwenda kwenye JENGO lililobomoka hakusaidia chochote yeye alisomea SHERIA na hata HIVYO alijazana pale na hakuokoa KIUMBE CHOCHOTE wote wamekufa na yeye yuko pale; zaidi ya kula CHAKULA KITAMU CHA HOTELI YA SERENA

KAMA angeokoa WATU TUNGEMPA SIFA... alijijaza na kutoa USHAURI kwa watu ambao sio Waokoaji... SHAME SHAME...

Haya sasa baada ya KASULU na Baiskeli afanye MKUTANO MWINGINE ati ana nini tena? OH Wachambuzi wanampa NYOTA --- Mwambie aende pale Jangwani... na Wachambuzi wake... SIASA zetu tunaziamasisha Maofisini... hakuna anayelipenda JUA...

Tusidanganyane, Mbatia hajawahi kufundisha sheria chuo kikuu, wala hakusomea sheria. Kama unamchukia mchukie kadri uwezavyo lakini usiseme uongo juu yake.
 
Hii ni baada ya kuiumbua CCM na wabunge wake ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hoja yake mujarabu kuhusu udhaifu wa sekta ya elimu hususani kutokuwepo kwa mtaala maalumu wa kufundishia.kwa kukosa umakini na busara spika wa bunge kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa ccm|9wasiowaza vyema) waliiondoa hoja ile kijanja janja na kumtukana mbatia.mungu si athumani muda si mrefu matokeo ya kidato cha nne yalitoka yakionyesha kufeli kwa wanafunzi asilimia 60 na zaidi.

Wachambuzi nwa mambo wanaeleza kuwa matokeo haya yaliiabisha CCM kwa kiwango kisichoelezeka huku yakimpandisha chati mbatia kwa viwango visivyotarajiwa na juhudi za kufifisha ukubwa wa aibu hii kwa kuunda kamati na kumjumuisha mbatia ziligonga mwamba na sasa kamati imemaliza kazi bila majibu ya maana.

Kitendo cha mbatia kugomea kujiunga na kamati hii ndicho hasa kilichozidi kumpandisha chati na kuonekana mzalendo wa kweli.

Kama haitoshi baada ya jengo la kule posta kuanguka mbatia alienda kushiriki kama mhandisi katika zoezi la uokoaji wa watu waliofikiwa mle ndani ya kifusi.kwa ujumla matukio haya yamempandisha chati ya kisiasa mbatia(so chama chake) na wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa anaweza kuitumia hali hii kama turufu ya yeye kugom,bnea uraisi 2015 kwa lengo la kuipandisha chati nccr-mageuzi inayoonekana kupoteza mwelekeo.

Mhhhhh still ni kibaraka wa CCM kiana katengenezwa kupunguza umaarufu wa CHADEMA lakini wananchi walio wengi wanalijuwa hili...............
 
Tusidanganyane, Mbatia hajawahi kufundisha sheria chuo kikuu, wala hakusomea sheria. Kama unamchukia mchukie kadri uwezavyo lakini usiseme uongo juu yake.

Nimefananisha na Mtoa Mada kumuita MHANDISI... Na Mimi namuita Mhadhiri wa CHUO KIKUU... reverse Quality... Kwanini unasema ninamchukia ? kumpinga mtu ni kumchukia?
 
Wapi HUKO? Mkutano wao HUKO KASULU JUZI ulihudhuriwa na Watoto na BAISKELI TU... Sasa Hiyo NYOTA unazungumzia ya CCM? oh yeah Anavuna MATUNDA aliyoyapanda ndani ya CHAMA TAWALA... Hata MIMI ningefanya HIVYO CHAMA kilikuwa hakina PESA za kulipa Viongozi wake hadi MWENYEKITI sababu kilikuwa hakina KURA NYINGI hakina VITI MAALUM hapo ULAJI hakuna... Sasa GHAFLA unapata SHANGINGI la BURE na BENDERA kweli NYOTA imekunyookea...

Umeandika HII kwasababu ya UKWELI au Sababu ya USHABIKI?
kishabiki zaidi alafu nahisi ni mbatia mwenyewe using fake ID,SISI tunajua kuwa mbatia anatumiwa na ccm kugawa kura 2015
 
Kwa ajili ya kupunguza kura za upinzani ndio maana tukampa ubunge wa kuteuliwa na tukamwambia afanye ju chini kujiimarisha ili mwisho wa siku Ccm ing'ae baada ya wapinzani kugawana kura.
 
CCM wanajua wana tishio kubwa sana 2015, nalo ni Chadema (isomeke Dr Slaa). Kwa kuhangaika wanajaribu sana ku-create another Dr Slaa ( wa kuchonga) ili 2015 azigawe kura za upinzani (Soma Dr Slaa). Walianza kwa Zitto lakini naona wameona ngoma haikolei, sasa wanahamia kwa Mbatia. Hawatafanikiwa!!!

ASANTE SANA MKUU KWA KUTAMBUA HILO.
Huu ni mkakati wa CCM, HAKUNA LOLOTE!
 
Back
Top Bottom