Kuelekea Casablanca, Simba twende namna hii!

Ouatarra sidhani kama yupo na timu,Simba inabidi wawe wengi sehemu ya kiungo wamzunguke yule Jezi namba 5 anaitwa Jabran kama walivyofanya juzi wakikaba yule WAC wanakosa nguvu mechi nyingi alizokabwa yule inaisha kwa kufungwa au ushindi wa kubahatisha mnaweza kuangalia mechi za AS vita zote mbili,na Ya Js kabylie kule algeria na ya Simba Tz,uzuri ambao ni ubaya kwa WAC hawana njia mbadala ukishika kiungo chao
 
Ngoja tuwasaidie kwenye game, tunawapa Aucho, Bangala na Morrison au mnaonaje?
 
Ni kweli nimepata taarifa muda si mrefu Quattara hayupo. Hapo Kennedy itabidi a take cover
 
Watara ,Onyango wote wazito.Hiyo mechi waarabu watakua na mashambulizi ya hara kuliko kawaida.
Kikosi changu hiki hapa.

Ally Salim
Onyango Kapombe Baka

Mwenda Kibu Mzamiru Kanoute Tshabalala

Chama
Baleke

3-5-2 fulani yenye kubadilika
Kapombe ni mshapu,atasogea juu kujaza wingi wa viungo wakati wa kushambulia na pia wakati wa kushambuliwa atakua juu ya mabeki Hawa wawili wa kati kuwakinga.
Chama pia atabaki kati kujaza viungo huku Kibu akiwa anasaidia kukaba kati na kusaidia mashambulizi ya kushtukiza.
 
Hata mwende kinyumenyume, kupigwa kuko palepale.
 
Onyango ana faida na hasara zake nikianza na faida onyango mzuri hewani ali win mipira mingi ya juu na kuondoa mipira mingi,ikumbukwe WAC walipata kona 8 na tunavyojua waarabu walivyo wazuri mipira ya juu ila walishindwa kufanya lolote, udhaifu wa onyango hana kasi ila mechi ya WAC anaweza asipate kipimo kwani uchezaji wa WAC sio wakasi kama ndugu zao RAC hivyo anaweza akasaidia ukizingatia striker wao aliyekosa mechi ya kwa mkapa Msenegal junior Buly sambu ana mwili mkubwa hana kasi sana na onyango anapenda mpira wa nguvu ni advantage kwetu
 
Waarabu wakiwa kwao sio watu wazuri. Hadi nimeukumbuka wimbo wa BABA JEAN BAI BAI
 
Waarabu wakiwa kwao sio watu wazuri. Hadi nimeukumbuka wimbo wa BABA JEAN BAI BAI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…