Kuelekea Dira Mpya ya Maendeleo 2050: Natamani Tanzania iwe namba 4 kwa uchumi Afrika na kuzipita Algeria, Morocco, Angola, Kenya na Ivory Coast

Huu ni uongo. Wakati wa JK ndio tulipigwa Gap na Kenya. Before 2005 tulika nao sawa. Wote tulikua na GDP ya $18bil.
But kutoka 2006 Hadi 2015 Kenya walitoka $18b Hadi $70b, wakati Tanzania tulitoka $18b hadi $47b.

Wakati wa magu, Kenya walitoka $70 mpaka $109b
Tanzania tulitoka $47b mpaka $70b
.
Tulifanha uzembe hapo kwa JK wakatupita mbali sana, but kuwafikia inawezekana

Uache pia UONGO
 
Huu ni uongo. Wakati wa JK ndio tulipigwa Gap na Kenya. Before 2005 tulika nao sawa. Wote tulikua na GDP ya $18bil.
But kutoka 2006 Hadi 2015 Kenya walitoka $18b Hadi $70b, wakati Tanzania tulitoka $18b hadi $47b.

Tuache UONGO.
Gdp bila population ni Misleading figure, Angalia per capita walikua wametuzidi, pia hizo data zako hazibadilishi chochote nilichosema mimi.
 
Inakisiwa kuwa mwaka 2050 Tanzania itakuwa na watu 141 milioni. Watu hao wakiwa na kipato cha US $ 4700 itabidi nchi iwe na GDP ya US $ 662,700,000.00. Ningependa kujua wanatarajia uchumi utakuwa unakuwa kwa kiasi gani kila mwaka.

Amandla...
 
Gdp bila population ni Misleading figure, Angalia per capita walikua wametuzidi, pia hizo data zako hazibadilishi chochote nilichosema mimi.
😂😂😂
Mkuu mambo mengine ni aibu ndogo ndogo tu. Anyway lengo halikua kukubadilisha imani yako but niliweka sawa ili usi-mislead wengine
 
Gdp bila population ni Misleading figure, Angalia per capita walikua wametuzidi, pia hizo data zako hazibadilishi chochote nilichosema mimi.
Nakubalina na wewe na itafika mahala hata kama una GDP kubwa lakini population haiongezeki utakwama kama kina Japan,Canada,Ulaya karibu yote na Sasa China Ina wasiwasi Kwa population kuanza kushuka.

GDP bila population growth ni scam
 
Inakisiwa kuwa mwaka 2050 Tanzania itakuwa na watu 141 milioni. Watu hao wakiwa na kipato cha US $ 4700 itabidi nchi iwe na GDP ya US $ 662,700,000.00. Ningependa kujua wanatarajia uchumi utakuwa unakuwa kwa kiasi gani kila mwaka.

Amandla...
Lengo ni GDP iwe &700bln na Ili kufikia size hiyo ya Uchumi inatakiwa tusipungue growth rate ya minimum 7% over the entire projected period
 
Uongo uko wapi hapo? Huoni Gap iliongezeka awamu ya Mwendazake?

Mwisho kama awamu yote ya JK uchumi ulikuwa Kwa wastani wa 7% na tukapigwa Gap unategemea nini awamu ya 5 ambayo uchumi ulikuwa below 7%?

Mwisho takwimu nilizonazo zinaonesha JK na Mkapa walifanya vizuri kuliko Mwendazake na umewahi ripotiwa mara nyingi tuu na media
 
Lengo ni GDP iwe &700bln na Ili kufikia size hiyo ya Uchumi inatakiwa tusipungue growth rate ya minimum 7% over the entire projected period View attachment 3174910View attachment 3174911
Asilimia 7 tuna fika $7000 Gdp per capita, makadirio ya juu (toka $1200 ya sasa) asilimia ~5 on average tunafika hio ~4700.

Kwa Gdp ya sasa hata tukiongezeka kwa 7% hatufiki hio 700B usd unless tuzaliane mno.
 
Lengo ni GDP iwe &700bln na Ili kufikia size hiyo ya Uchumi inatakiwa tusipungue growth rate ya minimum 7% over the entire projected period View attachment 3174910View attachment 3174911
Asilimia 7 tuna fika $7000 Gdp per capita, makadirio ya juu (toka $1200 ya sasa) asilimia ~5 on average tunafika hio ~4700.

Kwa Gdp ya sasa hata tukiongezeka kwa 7% hatufiki hio 700B usd unless tuzaliane mno.
 
Kuna Nchi ngumu sana Kuzipita, Kama Algeria soon Watakuwa na Uchumi mkubwa Africa wana Miradi ambayo haijapata Tokea Africa, na wanakua kwa kasi sana.

Ila Nchi kama Kenya it's doable, Soon tunawapita.
Unajua Kenya walitupita sana wakati ndo madalali wa bidha zetu kama Tanzanite, na bidha za mazao shambani. Sasa alivyokuja Mzee Magu, akavunja hiyo ndoa ndo maana kweli tukiwa serious, ni rahisi kuipita Kenya kiuchumi kwasababu kwenye masoko sasa hivi tunakwenda direct na Kenya sio tena Dalali wetu. Hahahahaaa
Pia kuuza vitu vyetu kutumia Technology imesaidia yaani minada na kushindanisha wanunuzi .
 
Unasema sioni gap liloongezeka wakati wa mwendazake?

Kenya tulikua nao saaa kwa kipindi chote Cha mkapa. Gap wameanza kutupiga wakati wa JK. Wakati wa mwendazake ni muendelezo wa gap ambalo walishatupiga.

Tuliza akili, wakati JK anaingia Kenya tulikua nao sawa, wote tulikua na GDP $18bil. Kuanzia 2006 hadi 2015 Kenya walitoka hiyo $18bil mpaka $70bil, wakati Tanzania tulitoka $18bil Hadi $47bil. Hapo ndio tulipopigwa gap

Uchumi wetu ulikua unakua kwa wastani wa 7%?? Ni mwaka mmoja tu wa JK ndio tulifika 7%, ilikua 2011, bahati mbaya mwaka uliofata 2012 tuliporomoka hadi 4%

Mkapa na Jk walifanya vizuri kiuchumi kuliko magufuli? Hii ni kweli kabisa japo hakukua na utofauti mkubwa sana(hapa usibishe maana najua haujui mambo mengi)

Nilichopinga kwako mzee wa matango pori ni kusema Kenya tulikua tunaenda nao sawa wakati wa JK na wakatupiga gap wakati wa magufuli (huu ndio uongo niliopinga, Kenya walitupiga gap kubwa wakati wa JK.
 
Unaielewa concept ya population versus GDP? Usikurupuke kama mambo hujui bora utulie

Twende taratibu, wapi ilipo athari ya population kubwa au ndogo kwenye ukuaji uchumi? Na pop growth rate ipi nzuri kwenye ukuaji wa uchumi? Again usikurupuke
 
Wakati ChoiceVariable unatamani hayo yatokee, unafanya nini ili yafikike?
Unazalisha, unauza, unaajiri.....?
 
Jadili hoja wewe nyumbu na msukule wa Mwendazake
Wewe kubwa la machawa mlamba makalio wa Samia hakuna Cha maana unachojua kwenye hii topic uliyoleta hapa, unachokiwaza hapa ni ndoto za alinacha... Na hakiwezi kutokea kamwe mathalan nchi hii itaendelea kuwa chini ya utawala wa maccm
 
Wewe kubwa la machawa mlamba makalio wa Samia hakuna Cha maana unachojua kwenye hii topic uliyoleta hapa, unachokiwaza hapa ni ndoto za alinacha... Na hakiwezi kutokea kamwe mathalan nchi hii itaendelea kuwa chini ya utawala wa maccm
Wewe ukiitwa mpumbavu itakuwa ni stahiki Yako.

Mambo ya Uchumi sio ya watu wenye akili fupi kama pua Yako.

Malengo yameshawekwa ni $700bln by 2050 na inaweza kuwa zaidi ya hapo na kuweka Tanzania top 5.
 
Na Ile utumie wisely lazima upange.
Unafikiri uchumi unakuzwa kwa kupandisha bei ya vifurushi vya internet na kuongeza ongeza ovyo tu matozo yasiokuwa na kichwa Wala miguu pasipokujali Hali za wanainchi etiii???

Au unafikiri Uchumi unakuzwa kwa kukabidhi rasilimali za taifa kwa wageni kiholela holela tu kwa mikataba ya kimangungo?

Nikujuze tu Tanzania kuwa na GDP ya $700b kufikia mwaka 2050 ni jambo lisilowezekana hata kidogo...

Hadi kufika 2050 kwanzia Sasa ni miaka 25 tu imebaki, leo hii GDP ya Tanzania Iko kwenye $79b Ina maana ndani ya miaka hiyo 25 tuwe na ongezeko la $621b hili kufikia hiyo forecasted GDP.

Sasa tuje katika uhalisia Kuna sera gani hasa za kiuchumi zilizopo ambazo zinazo tuhakikishia sustainable economic growth ya $621b kwa muda wa miaka 25?

Maana hili tukuze uchumi wetu kwa kiwango hicho na kwa muda huo itabidi tuwe na economic growth rate ya 11% kwa mwaka, Sasa kwa mazingira yapi yatakayotufanya uchumi wetu uwe na Kasi ya ukuaji wa 11%?

Kuna sera gani hasa ambazo Zina stimulate domestic investment maana wawekezaji wa ndani ndio wajengaji wakuu wa uchumi popote pale duniani, Sasa hii serikali ya Samia imefanya nini kuwapa hamasa wawekezaji wa ndani mpaka dk hii?

Najua unategemea population itatubeba, ila nikujuze tu ukiwa na population kubwa ambayo wengi wao ni walalahoi hawana purchasing power ya maana ni kazi Bure tu kwenye uchumi.... Maana hakuna mwekezeji atakayethubutu kuweka hela zake sehemu ambapo wanainchi wengi hawana hela.

Inaaminika kwamba hadi kufika hiyo 2050 Tanzania itakuwa na population ya watu wasiopungua 100m of which ni advantage kiuchumi, lakini kama hatuta weka mazingira sahihi ya kiuchumi tutakuwa kama Nigeria tu au Bangladesh, population kubwa ila haiendani na uchumi uliopo kwenye nchi husika.
 
Ujinga wako wa kutokujua sera na mipango ya Nchi iliyopo usitake kuwajumuisha wengine.

Sio lazima kuwa na ukuaji wa 11% Bali 8% inatosha sana.

Turudi Sasa kwenye sera zilizopo ambazo Mimi nazifahamu Baadhi yake
1.Universal Health coverage,Afya ndio msingi na hapa tayari sera ya bima ya Afya Kwa wote ipo na utekelezaji wake uko hatua Kwa hatua.

2.Tanzania inalenga kuwa kinara wa Kuzalisha mazao ya Kilimo Africa na pia kuondoka kabisa importation ya mazao ambayo tunaweza zalisha mfano Ngano,Mafuta ya kula,mbegu,korosho ,mbolea nk ,agenda 10/30 ni reference.
-As we speak Jumla ya hactares 500k plus zinajengwa na Serikali ya Samia ,Toka uhuru Kuna hactares 900k tuu

3.Tumeweka lengo la Utalii kufikia watalii walau 5mln by 2025 na kuongeza kadiri ya uboreshaji wa Huduma,lazima tuvute watalii mil.15 by 2050.
-Ujenzi wa miundombinu ya Utalii unaendelea hasa Southern Circuit Kwa kujengwa viwanja vya ndege na Huduma zingine.

4.Tunalenga kutumia sekta ya Madini kutuvusha huko,Tanzania ni Nchi ya 5 Africa Kwa kuwa na Madini mkakati mengi ambayo ndio hata drive Dunia , uwekezaji unaendelea sio tuu huko Hadi kweli Madini ya Chuma.

5.Tanzania imeanza kununua dhahabu kama njia ya kukabiliana na forex na kuyumba yumba Kwa Shilingi

6.Kwenye uwekezaji ndio usiseme,hiyo figures unavyoona hapo 2/3 ni domestic investments ila Kwa kuwa wewe ni mbumbumbu na mjinga ndio zinaongea huo upuuzi wako wa unaodai Mali ziko Kwa wageni.
-Sio tuu tunafanya promotion ya uwekezaji Bali Serikali ya mama imeunda Tume ya Kupitia kero za Kodi ,tozo nk lakini by we speak Mama amefuta zaidi ya tozo 375.

7.Kwenye Miundombinu, Serikali imeamua kuwekeza sawa sawa huko Vijijini Kwa Kupeleka Barabara za uhakika,maji na umeme.Mambo hayo yatawezesha uwekezaji kufanyika popote.

8.Serikali ya mama imebadili mitaala ya Elimu na kuunda mitaala ambayo inajilita kwenye Elimu ya umahiri hususani fani za amali kuanzia shule ya Msingi Hadi Vyuo Vikuu,utekelezaji unaendelea.

9.Kwenye Nishati tayari malengo yamewekwa ambapo by 2034 tuwe tumeachana na mambo ya Kuni na Miata about 80% itumie Nishati safi ya umeme na gesi nk na utekelezaji unaendelea.
-Umeme hautakuwa tatizo tena tuna vyanzo mseto vinaendelezwa vya maji, geothermal,jua ,upepo nk

10.Mabiresho ya sheria Ili kusapoti biashara ni suala mtambuka linaendelea.

View: https://x.com/AnnaSarungi/status/1867125113398948335?t=TFLJzEv-nnSZQyKbxcSeHw&s=19
Hayo yote coupled with population growth tunaenda kuishangaza Dunia.
 
Malengo yameshawekwa ni $700bln by 2050 na inaweza kuwa zaidi ya hapo na kuweka Tanzania top 5.
Ndoto za alinacha hizi, unafikiri uchumi unakuzwa kwa matarumbeta na mapambio mnayomuimbia huyo bibi eti?

Kubwa Jinga wewe hata elimu ya hiki unachokiongea huna zaidi ya kuropoka tu na kuleta uchawa wa kis.enge ki.senge.

Tangu mwaka 2000 uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa wastani wa 6.5%, kutoka kwenye GDP ya $14b mpaka leo hii $79b ambapo ni sawa na GDP growth ya 464% kwa muda wa miaka 24...

Sasa wewe ukiongelea GDP $700b kutoka kwenye $79b una maanisha tuwe na GDP growth ya 886% kwa muda wa miaka 25, yaani Ina maana kwamba Kasi ya ukuaji ya uchumi kuelekea 2050 iwe ni mara mbili ya Kasi ambayo tumekuwa nayo kwa miaka 24 iliyopita.

Sasa na Mimi nakuja kukuuliza kwa sera zipi mlizonazo hili mfanikishe Hilo??

Kwamba Mwigulu na boss wake mipango ndio wataumiza vichwa waje na mbinu ya kuukuza uchumi wetu kwa rate ya 11% Kila mwaka??

Nakuhakikishia hivi, kwa aina ya viongozi waliopo kwenye taifa hili ambao wametanguliza mbele matumbo yao kuliko maslahi ya taifa, Hilo haliwezekani na halitowezekana ng'oooo!!!

Nyie endeleeni kumsifia Samia tu hapo huku kwa sifa ambazo Hana, ila uchumi unaelekea chini kwa Kasi sana bila yoyote kati yenu kujua.
 
Wewe nyumbu Wacha upumbavu,kama huna akili ni wewe na kama hujui au huoni mipango na utekelezaji wake hiyo ni shida Yako .

Hakuna muujiza hapo tutakua na kuzidi hapo,Tanzania Ina fursa zote za kufika na kuvuka hiyo target Kwa sababu mipango imewekwa na utekezwaji unafanyika..

Mwaka huu 2024 tuna GDP ya $85bln ,tunapoanza utekelezaji wa Dira Mpya ya 2025 kuanzia Bajeti ya 2025/2026 tutakuwa na GDP ya zaidi ya $90bln.

Njia ya kuelekea kwenye Neema hii hapa 👇 👇

View: https://x.com/AnnaSarungi/status/1867183048271270293?t=cnMWN5XmHJF9j0SQ4F_NLw&s=19
 
Hapo awali nilikwambia mipango si matumizi, Kuna tofauti kubwa sana Kwenye kutunga sera au kuandaa mipango na kusimamia hiyo mipango walau ilete matokeo ya kile kilichokusudiwa hata kwa 80%.

Na pia Kuna tofauti kubwa katika ya kutunga sera nzuri na sera sahihi na madhubuti zinazoendana na uhalisia wa mazingira husika yaliyopo.

Hakuna mtu wa CCM mwenye uwezo wa kufanya hayo yote uliyoorodhesha hapo.

1. Kuhusu bima ya afya kwa wanainchi wote, hapa serikali ya CCM ilishashindwa siku nyingi sana sababu ya urasimu usiokuwa na kichwa Wala miguu kwanzia kwa wanainchi wenyewe mpaka hospitals za watu binafsi.

2.Moja ya wizara ambayo huwa Ina sera nzuri miaka yote ila hazitekelezeki hasa kutokana na watu walioshikilia wizara hiyo pamoja na bajeti ni wizara ya kilimo. Yaani unataka uachane na ku import mazao ya chakula halafu eti unatenga bajeti isiyozidi Tsh.300b eti ndio iende ikafund shughuli zote za kilimo kwenye taifa la watu 61m si utani huo? Huo mpango wa Bashe hautawezekana na mtaendelea kuimport mpaka mfuta ya kula.

Na pia ni Aibu kubwa sana kujinasibu eti mna mpango wa kutanua hectares za kilimo zifike 900k tu na wakati tunaambiwa nchi hii Ina Arable land Zaid ya hectares 5.5m

3.Kuhusu sekta ya utalii ngonjera zenu huwa ni zile zile tu, hoo Tuna mpango wa kuongeza idadi ya watalii wafike 5m, na wakati Sasa hivi hata watalii 2m tu ni wa kutafuta, kwanza Kuna kipi Cha maana mlichoboresha kwenye sekta ya utalii? Hotels Bado ni zile zile tu huduma za afya ni zile zile, Kuna kipi hasa Cha kukufanya wewe unaamini hadi kufika hiyo 2050 mtakuwa na influx ya watalii 5m?

4.Kuna kitu ambacho mtanzania hatakiwi kabisa kuongelea basi ni madini na nikionaga mtu anaongelea madini kama source ya kututoa hapa tulipo nakuona kama ni kichaa yaani mtu aliyechanganyikiwa... Hayo madini mikoa yanayopatikana ndio inaongoza kwa umasikini hapa Tanzania, unawezaje kumshawishi mtu mwenye akili timamu kwamba hayo madini Bado ni Mali ya watanzania na sio Mali ya wawekezaji waliongia mikataba ya miaka mia na serikali ya CCM?

5. Kununua dhahabu kama njia ya kukabiliana na fluctuation ya currency huko ni kushindwa namna ya kumanage balance of payments.

6.katafute machawa na wajinga wenzio ndio uwadanganye kuwa serikali ya Samia ina jali kuhusu local investors, hakuna raisi mpuuzi na WA ovyo ambaye anajali Zaid wageni kuliko wazawa kama hicho kibibi Cha kizanzibar

Kuhusu hizo tozo unazosema eti mazifuta si ndio tuliambiwa kwamba kama hatuzitaki tuhamie Burundi na tutake tusitake lazima tutalipa tozo.. unaandakia nini wewe mjinga?

7. Hii serikali ya Samia kama umeshindwa kutatua tatizo la maji hapa hapa dar tu ambapo ndio mji mkuu wa kibiashara nchini ndio itaweza kuondoa tatizo la maji huko vijijini?.. yaani hapa Dar es salaam tu Kuna wanatumia maji ya mitaloni kupikia mpaka leo hii ndio aje aondoe tatizo la maji huko Nyansamba na kwingineko? Tok unrealistic plans.

8,9 na 10 ni porojo na blah..blah tu za kisiasa ambazo kwa yeyote mwenye akili timamu anajua haziwezi kufanyika hata kwa asilimia 10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…