Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Hahahaha hawa Iceland hawakubali kufa kifo cha mende.
 
Hawakujipanga,aliweka vijana wengi ambao hawana experience na mechi za kimataifa. Kingine kocha hana sifa za kutosha ingawa wanag'ang'ania mwingereza mwenzao. Juzi Kevin Kegan alikua anaulizwa mwingereza yupi anafaa kuwa kocha akasema hakuna,kama timu wanataka ifike mbali watafute kocha ambae sio mzawa. Vyombo vya habari vinawapaisha tu huku hamna kitu.
 
Reactions: BAK
Britich wana wivu sana,wameona wapoland wanapiga kazi na wanatajirika,wakaanza kulalamika wageni wanachukua kazi zao,mpaka wameamua kupiga kura za leave Eu,nakuambia hata hili la wachezaji ipo siku watapiga burn wachezaji foreignerz,utaniambia.Sema tu kwa vile team zao nyingi kwa sasa zimenunuliwa,ila watapunguza idadi ya wachezaji wageni kama sio kufuta kabisa,wa England wana wivu sana
 

Uingereza wameharibu kwa kuibinafsisha Premier league yao.

Ukifanya hivyo huwezi kuwa na timu nzuri ya taifa maana timu zote zina mameneja wa kigeni na wachezaji wa kigeni yaani watano wa kigeni na watano wa Uingereza.

Wakitaka kuwa na timu nzuri ni kuwatayarisha wachezaji wao mahili kama beckam ambao wao nao wameamua kuwa na biashara zingine baada ya kustaafu au kuwa pundits ili wakae pembeni na waanze kupiga kelele.

Uingereza ina wachezaji mahili sana lakini hakuna mfumo mzuri wa kuwaandaa kwa international level.

Germany, Italy, France na Spain hazina mameneja wageni na wachezaji wageni wanadhibitiwa katika ama Bundesliga, Serie A, League 1 na La Liga au katika academy za chipukizi.

Ni mfumo wa uendeshaji wa mpira ndio hauko sawa kama vile TFF tu.

Nchi lazima iwe na identity ya mpira wake na ndio twaona hizo nchi nilizozitaja zikionyesha hilo.

Uingereza wanacheza sana individually na sio kama timu.

Na hilo ni kosa la meneja ambae nae hana mbinu nzuri za ufundishaji.
 
Sio kabisa..Wao kama wameshindwa kuzalisha wachezaji wazuri wasilaumu clubs zikichukua wachezaji nnje ya UK.
 
Umesema vyema mkuu
 
Leo yatatokea yale ya Germany vs Brazil

Not close. Ungesema MK Dons vs Manchester United endapo Iceland ingekuwa inaongoza 5-1 ningekubali. Brazil, Germany na France wapo katika anga tofauti kimpira ukilinganisha na Iceland.
 

Quota waliweka tayari miaka miwili imepita wakasema ni 5 English, na 5 Foreigners.

Watu kama Arsene Wenger akasema angalau ajitahidi kufufua vipaji vya wachezaji wa Uingereza kwa kuwakusanya Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Theo Walcott, Calum Chambers, Alex Oxlade Chamberlain na Carl Jenkinson.

Roy Hodgson akawaacha Theo Walcott, Jenkinson na hata Jermain Defoe wa Sunderland na Danny Drinkwater wa Leicester kwa sababu ambazo hazikueleweka.

Lakini watu kama Theo Walcott na Jermain Defoe wana uzoefu wa mechi za kimataifa na wamecheza huko nyuma kwenye WC.

Hivyo wakati mwingine mimi naona tu kwamba siasa nazo zinachangia kuzorota kwa timu ya Uingereza.
 
Inasemekana idadi ya Foreigners kila timu inayoshiriki BPL itapunguzwa ingawaje hili linapingwa sana na baadhi ya makocha akiwemo wenger na aliyekuwa kocha wa MANU Sir Alex Ferguson ambao wanasema litaifanya BPL idorore. Tusubiri tuone yatakayojiri.

 
France wana blacks 8 wako uwanjani..Nawakubali sana,hawana ubaguzi kama wengine
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…