Kilichowapotezea Croatia ni kukazania kumzuia Ronaldo asitafute vyumba na akiende sana mbele.
Luka Modric na Ivan Rakitic wanacheza na Ronaldo pale Bernabeu hivyo kwa kuwa wanamfahamu vizuri na mtindo wa uchezaji wake wao wakawa wanamchunga yeye tu na kuzuia supply ya mipira isiende kwake.
Portugal kuona hivyo wakawa hawana jinsi na ikabidi wawe wanapokea mashambulizi kwa kujaribu counter attack lakini wakawa pia nao wanazipoteza.
Lakini walipomwingiza Renato Sanchez ambae ndie alietolea pasi Nani ambae akampa Ronaldo kujaribu kufunga hiyo ilikuwa ni hatua ya kujaribu kumaliza game na imefanikiwa hivyo ni uzoefu tu.
Yaani hapo watu watatu Sanchez, Ronaldo na Nani ndio wamefanikisha goli lililofungwa na Quaresma.