Kuelekea game na Wydad: Wajibu wa benchi la ufundi kwa Onyango!

Kuelekea game na Wydad: Wajibu wa benchi la ufundi kwa Onyango!

nakubaliana na mleta mada, Onyango ni bonge la beki na amekua akisaidia sana Simba, pia akuna mbadala wa Onyango pale Simba ukiacha pacha wake Inonga.
 
Wakuu,

Beki kisiki Josh Onyango amekuwa ni mhimili wa ulinzi Simba lakini amekuwa akifanya makosa yanayofanana mara nyingi. Josh akiachwa kwenye kasi akili yake ni kucheza rafu bila kuangalia eneo alilopo na uwezekano wa kupata msaada.

Bado hatuna beki bora kuliko Onyango na mapungufu yake kwasasa ni wajibu wa benchi la ufundi nje ya kuangalia mfumo ni lazima kuwe na special assignment kurekebisha makosa ya Onyango. Tuna mabeki bora duniani waliocheza kwa umri mkubwa na wasio na kasi kubwa lakini wamefanya vizuri zaidi.

Wachezaji waliopo ndio wataotumika, bado inawezekana kabisa tukafanya vizuri kama tuki focus vizuri kwenye kuandaa Wachezaji kama timu na individually.

Ushauri,
Simba waajiri special consultancy team wenye experience kwenye defence mechanisms. Hii iwe ni project fupi kwaajili ya hatua hii ya robo fainali. Makocha Robertinho na Mgunda wamecheza kama washambuliaji enzi zao! Nahisi kwenye ulinzi wa kupambana na timu kama Wydad ni muhimu washauriwe na independent consultant.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Huna kipya Cha kufanya Kwa mda huu we subiria Mungu nisaidie
 
Ingekuwa Yanga hashiriki kwenye Kombe la Shirikisho Simba wangemwazima Ibrahim Bacca wa Yanga jamaa hana maskhara, kama mwaka 1998 Yanga walivyowatumia Wachezaji Monja Liseki na Alphonce Modest wa Simba.
Sheria za enzi za giza 🤣
 
Simba hana uwezo wa kuwatoa Wydad huyo Onyango acheze au asicheze, watafute tu namna ya kuunda timu upya baada ya kumaliza mechi za robo fainali. No way out.
 
Wydad Casablanca ni kaka yake Raja Casablanca
Ebu jaribu kuwaza kitakachotupata. Ikiwa mdogo mtu katupiga ndani nje, je, kaka yake si itakuwa balaa! Tujiandae tu kisaikolojia kuwa kwa hapa Simba watakuwa wameumaliza mwendo!
 
Back
Top Bottom