Truth Teller
JF-Expert Member
- Aug 20, 2016
- 1,623
- 2,892
Hii Game Simba Anapoteza.Zimebaki siku chache kabla ya Simba SC kushuka dimbani kuwavaa USGN kutoka Niger katika pambano la kuwania alama tatu muhimu ili kuweza kutinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Ili Simba SC iweze kushinda mchezo dhidi ya USGN mambo haya yafanyike haraka ili kuepusha yaliyotokea kwenye mchezo muhimu sana kwa kufungwa 3-1 na kuondoshwa kwenye Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.
1. Simba SC waingie na mpango wa kuchagua kuwa direct kushambulia huku wakiwa na mbinu ya kuzuia kwanza eneo la USGN ili kuwanyima uhuru wa kuanzisha mashambulizi kutoka chini.
2. Simba SC wasikubali kufunguka kirahisi, na maamuzi yafanyike kwa haraka sana katika kuutoa mpira katika zone yao, USGN wakifanikiwa kuvunja mstari wa pili wa Simba wa wachezaji wanne ambao unazuia njia ya pasi, itakuwa ni hatari sana Simba SC.
3. Umakini uwe silaha muhimu kwa Simba SC pale wanapopoteza mpira wakati wa kutengeneza mashambulizi, yapasa kuzuia kwa shape ya 4-4-2 au 5-4-1 kuziba njia ya pasi za USGN na kufunga half spaces zote kwa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wanaozuia eneo la Simba SC.
Kwa maandalizi yote yanaendelea nina imani Simba SC kuibuka na ushindi ijapo kuwa mpira ni dakika 90, lakini bila shaka Viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote watatimiza majukumu yao kiweledi huku mchezaji wa 12 ambaye ni Shabiki akijitokeza kwa wingi kwenye Dimba la Benjamin Mkapa ili kuipasupport Simba SC wakipeperusha vema bendera ya Nchi ya Tanzania.
Kwako Mshabiki na Mdau wa Soka nini kifanyike kuepusha kufurushwa kwenye Kombe hili la pili kwa Ukubwa Barani Afrika... Karibu...!
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
KWA Matuta.
Kocha awafunde kupiga penalty la sivyo watapoteza
Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app