Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

jina la mkoa ulioanza nao linaweza kutuletea jambo
 
Kwani huamini kwamba mawaziri wanajichanganya, Mhe Rais anabadili kauli, na NIDA wanakesha ofisini, ili kumaliza tatizo la 'ile hela tuma kwa namba hii'?
 
Sikiliza hii
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Roho mbaya tu.
Hakuna lingine
 
Je,kuna relationship yoyote Kati ya zoezi la kusajili line kwa alama za vidole na uchaguzi mkuu 2020?
Mwenye maono aniamshe tafadhali
 
Hili zoezi linatakiwa lifanyike ndani ya miaka 3.
Mm siwezi kupoteza siku nzima niko kwenye foleni ya nida bila mafanikio yeyote.
Wacha wazime, potelea pwetee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, wakati naongea na ndugu yangu mmoja leo akaniambia amefanikiwa kumaliza process za uandikishaji wakamwambia asubiri baada ya wiki mbili kupata namba za NIDA lakini wakati anaweka doubt yake kuwa leo line yake itazimwa wakamwambia nunua ya TTCL hizo zitaendelea kupewa huduma.

Wakuu kuna ukweli hapa?
 
Kwa akili za Magufuli kupenda kuua sector binafsi ilo linawezekana maana anapenda sana Monopoly angalia kwenye fastjet ndio utaelewa.
 
Kwani kabla ya usajili huu wa National ID, Lain za TTCL zilikuwa zinatumika bila kusajiliwa? Au leo ukienda kununua hiyo lain ya TTCL unaweza kuitumia bila kuisajili?
 
Dah hii mbeleko ni baaab kubwa
Jr[emoji769]
 
Kuna madogo wapo kitaa wamemaliza shule ya msingi na wanapiga misheni town wanategemea simu wapigiwe na mabosi wao wapewe michongo ya kazi je hawa hawaruhusiwi kumiliki simu kama zamani?

Maana nasikia watakaosajilia wengine watakamatwa ni kinyume na sheria hii imekaaje wanasheria? Je kumiliki simu mpaka uwe na miaka 18 kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…