Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Pesa watakayoipoteza serikali na mitandao kwa kushuka kwa mauzo ya airtime na charges za miamala ya simu itawarudisha kwenye mstari.
 
Makuwadi wa sheria za kipumbavu utawajua tu...

Hivi mtu unasajili laini kwa fingerprints kitambulisho cha uraia cha kaz gani?

Funga laini funga kila kitu.. its about time.. mateso wanayopata wananchi kwa kitu ambacho si cha lazima sana ipo siku wataelewa maana yake na ku revenge.
 

Ni ajabu sana!
 
Sio watu wote wanaochukua vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kusajili simu. Unaweza kutumia kutembelea Kenya bila kuwa na passport, kurasimisha kiwanja au kusjili kampuni.
Kinaruhusiwa kweli kwendea Kenya bila passport
 
Na nyie kijani hua mnalalamika?ni mwiko kulalamika we lumumba,endelea kusifu na kuabudu atakuja jiwe kukutetea
Nyumbu mkubwa
Wapi nimeandika mi kijani..? Hizi ndo akili za kuazima
 
Ndio lengo lake huyu ntarahamwe.
 
Hili zoezi ni la kipumbavu haijawahi tokea,wataweka vipi dead line wakati si wananchi wote wana vitambulisho vya Nida?Kupata Kitambulisho chenyewe unaweza hata zimia kwenye foleni.Kwanza sidhani kama kuandikisha line ndo kitu mtanzania anahitaji ili aishi.Mtanzania anahitaji Maji safi na salama,Kazi,huduma bora za jamii kwa ujumla.
 
Sijui kama kumbukumbu zangu zinaniangusha kuhusu hili suala la usajili wa namba za simu. Ninavyokumbuka mimi, awali mwanzoni mwa mwaka 2019 TCRA walitoa ratiba yao ya kuishia Desemba. Serikali ikawakemea kuwa muda walioweka ulikuwa mfupi! Sawa. Tukategemea kuwa mashauriano yatafanyika ili muda uongezwe. Mwezi Novemba, 2019 katika kikao cha mwisho cha Bunge serikali kupitia waziri mwenye dhamana na vitambulisho vya taifa akatoa kauli bungeni kuwa simu hazitazimwa. Wananchi wengi wakapumua. Majuma matatu baada ya kauli ya waziri ikatoka kauli ya Rais kuwa simu zitazimwa kama TRCA walivyopanga lakini kwa hisani yake kama kiongozi mkuu anaongeza siku 20 hadi Januari tarehe 20! Pamoja na kwamba tatizo la msingi ni NIDA kauli hizi za serikali zimewavuruga sana wananchi. Wananchi wengi walikuwa wanasubiri maelekezo kupitia kwenye ofisi zao za mitaa na vitongoji kuhusu vitambulisho au namba za NIDA. Ghafla zoezi likageuka operesheni ya zima moto ambapo wanaacha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kuhangaikia kupata namba ya NIDA!. Hapa kuna tatizo kubwa sana la kiuongozi.
 
kwa kweli hata mimi nina mpango wa kutumia kitambulisho changu kusajili laini za ndugu wa karibu wote ambao hawana no au Id ya Taifa
 
Yaani sisi dah! Kuna kitu kweli tunaweza kukifanya kwa weledi kabisa kabisa kikaenda kitaalamu bila figisu figisu? Kwa nini inakuwa hivi lakini?

Hapa utakuta watu wameiba mpaka basi. Watu weusi sisi tuna matatizo sana wallahi.
 
Tcra wao naona hawana communication nzuri na NIDA!

Watu tulijiandikisha toka mwaka jana, lakini waliopata namba ni wachache, sisi wengine eti tusubirie awamu ya pili!

Walojiandikisha miezi miwili iliyopita wameshapata namba ila sisi wa toka mwaka jana tunaambiwa subiria awamu ijayo. Na bado line zetu wanataka kuzipiga nyundo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya kusajiri line na kumpatia ndugu asiyeweza kusajiri kutokana na factors mbali mbali nadhani halina shida.

Mfano wazee wetu huko vijijini unaacha kuwasajiria line unadhani watafikiwa lini na nida ili kupata vitambulisho kama hata hapa mjini ni shida.

Ukizingatia ni kupitia simu tunawasiliana na kuwasapoti hao wazee wetu kwa kuwatumia pesa kupitia hizo simu wanazoenda kuwazimia, kesho kutwa kama kweli.
 
Nchi hii shagalabagala na viongozi wake wote ni shagalabagala
 
Nasikia nyerere aliwahi kushauri rais asitoke usukumani sijui nani alimpendekeza huyu mchattle
 
Hii nchi kila kitu ni vululuvululu

Hakuna kitu kinachofanywa nchi hii kikanyooka, kiasi kwamba mtu ukasema naam hapa kuna weledi makini unetumika hapa.

Kuandaa mazoezi na operesheni mbalimbali za kijamii, kiichumi na kisiasa inahitajika vichwa makini vilivyotulia kuyaaandaa, siyo kukurupuka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…