Asalaam Tanzania na nje ya Tanzania..Karibu katika burudani ya soka ya kiwango cha juu kilichothibishwa na Shirikisho la Kabumbu Barani Afrika
CAF, kutoka kwa
Simba SC, WanaLunyasi, Mnyama Mkali Mwituni
Kuelekea Ligi Mabingwa Afrika, Jumapili Agosti 25, 2019 Mabingwa wa Nchi
Simba SC, wanawakaribisha
UD Songo, kunako Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya sare ya kutofungana katika mechi awali ilipigwa nchini Msumbiji.
Kocha
Patrick Aussems, amesema Simba SC wapo tayari kufanya kila inavyowezekana katika mchezo huo kufanikisha ushindi dhidi ya UD Songo ili kuweza kufuzu hatua inayofuata.
"Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo. Tunatakiwa kuwa makini tunajua tunakutana timu nzuri na mchezo utakuwa mgumu lakini TUNAJIAMINI". Amesema kocha Patrick Aussems.
β’β’β’Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana
WanaSimba, Wanachama, Mashabiki Kindakindaki na mdau wa kabumbu, maandalizi yote kuelekea mchezo huo yamekamilika, kwahivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi kuishangilia mwanzo mwisho Simba SC, ambao wataupiga mpira mwingi mno..UD Songo watautafuta mpira kwa Tochi.
Usikose Ukaambiwa..WeAreSimba SC, NguvuMoja This Is Next Level.View attachment 1189396View attachment 1189397